CUF Wagonga Mwamba, Karume Akataa Kuongezewa Muda Hata wa Siku Moja Ikulu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF Wagonga Mwamba, Karume Akataa Kuongezewa Muda Hata wa Siku Moja Ikulu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Jan 25, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Jan 25, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  SHINIKIZO lililokuwa likitolewa na Chama cha Wananchi (CUF), kutaka Katiba ya Zanzibar ivunjwe ili Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Amani Abeid Karume aongezewe muda wa kuongoza limegonga ukuta baada ya Rais Karume kuikataa hoja hiyo na kuwasihi Wazanzibari wote kumuunga mkono katika hilo.

  Aidha shinikizo lingine la kutaka kuundwe kwa serikali ya mseto Zanzibar limekubaliwa, lakini limetakiwa kufuata azimio la Butiama la kutaka uamuzi huo ufanyike baada ya kuamuliwa na Wazanzibari wenyewe kupitia kura ya maoni.

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Salehe Ramadhan Ferouz, alitoa msimamo huo jana baada ya kumalizika kwa kikao cha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Zanzibar kilichojadili hoja kubwa tatu zinazohusu mustakabali wa Zanzibar kilichokuwa chini ya uenyekiti wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais Karume.

  Katika ajenda ya kwanza ya kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Dk. Ali Mohamed Shein, Rais Karume alitakiwa kutoa taarifa rasmi kuhusu yaliyozungumzwa katika kikao chake na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

  Katika majadiliano hayo, Rais Karume aliweka bayana kuwa Seif ndiye aliyemfuata kutaka mazungumzo naye na walizungumza masuala ya kujenga umoja wa Wazanzibari, kuacha siasa za chuki na kujenga Zanzibar mpya ambapo wajumbe walipokea vyema taarifa hiyo.

  Ajenda ya pili ya kikao hicho kilichoanza saa nane mchana na kukamilika saa moja usiku, ilihusu zilizoitwa kuwa ni tetesi za kutaka Katiba ya Zanzibar ivunjwe ili Rais Karume aongezewe muda wa kuongoza baada ya kumalizika kwa kipindi chake cha pili cha uongozi ambacho kwa mujibu wa katiba hiyo, alitakiwa kupumzika.

  Rais Karume alisisitiza wakati wa kujadili ajenda hiyo kuwa msimamo wake ni kama alivyoutangaza wakati wa sherehe za miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuweka msisitizo kuwa hataki kuongezwa hata siku moja!

  Aidha Karume aliwasihi Wazanzibari wote ambao walikuwa wakishinikizwa na kushawishiwa na CUF kupitia makongamano na maandamano, kumuelewa kuwa asingependelea kuongezewa hata siku moja ya Urais baada ya muda wake kikatiba kumalizika.

  Ajenda ya tatu ambayo imeelezwa kuwa ilichukua muda mrefu kidogo, ni iliyohusu kuundwa kwa Serikali ya mseto. Katika kujadili ajenda hiyo, wajumbe walikubaliana kutoingia kwa undani zaidi kuwa kambi ya upinzani inaiandaa kwa ajili ya kuifikisha katika Baraza la Wawakilishi ili ijadiliwe kwa kina.

  Hata hivyo, ilibidi wakumbushiane maazimio ya mkutano wa NEC ya CCM uliofanyika Butiama mwaka 2008 ambayo yalitaka wananchi wa Zanzibar waamue kuhusu uundwaji wa serikali hiyo kupitia kura za maoni jambo ambalo pia lilikubaliwa.

  SOURCE: HabariLeo
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Amesoma alama za nyakati kuwa hatapata support aliyoitarajia...!

  Lakini pia ameona heshima ni kitu chema, na once ukiivunja hata kidogo, ni gharama sana kuirudisha!
  Bravo Karume...umejenga heshima at least kwa hiyo firmness!
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Jan 25, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180

  Sure!
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Jan 25, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  This is very, very interesting indeed! Yaani thread hii ina mchangiaji mmoja tu?
   
 5. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hayo si ya toka juzi kwenye kikao alipowashushua wazee, hiyo ilikuwa ni danganya totoz ili waondoke basi nothing will change him alichosema juzi karudia kile kile alichosema kwenye sherehe ya mapinduzi kuwa hatavunja katiba.
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Jan 25, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Pole sana kwa majukumu, naona yalikuelemea ukabaki nyuma. Ungewahi na kusoma thread hii hapa, usingeanzisha hii kwa vile jambo hili lishejadiliwa kitambo.
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jan 26, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nashukuru kwa kuni-alert! Have a great day!
   
 8. B

  Bumbwini Member

  #8
  Jan 26, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi nilishasema mapema ccm hawaaminiki hata kidogo,juhudi zote hizi za kuleta maridhiano zinazoletwa na wanaoitakia mema nchi yetu wao ccm wanafanya kama mchezo wa maigizo,hawaaminiki hata dakika 1 hawa,hakuna chochote cha maana wanapoteza muda ili cuf walegeze kamba ukifika uchaguzi wanafanya usanii wao kama kawa na malumbano,fitna na chuki zinarudi palepale,nasisitiza tena ccm hawaaminiki hata kidogo ni vigeugeu wakubwa sana na mifano hai ipo.
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Jan 26, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  CUF wanaogopa uchaguzi kama ukoma! Sijui wataendelea kuogopa mpaka lini? AU kuanzishwe Serikali ya Kifalme Zanzibar ambapo Mfalme atatawala maisha yake yote na akifariki anamrithisha mtoto wake, ambaye naye akifariki mtindo unakuwa ni ule ule?
   
 10. Mwalimu Makini

  Mwalimu Makini Member

  #10
  Jan 27, 2010
  Joined: Dec 5, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CUF walirudi nyuma katika siasa za upinzani Tanzania kwa kutegemea kuwa iko siku watafaidi dezo ya serikali ya mseto.
  Thubutu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...