dudus
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 22,116
- 49,360
Kaazi kweli kweli yaani kwako wewe historia na sia za Tanzania zimeanzia 2010 baada ya Dr. Slaa kugombea urais umesahau kuwa CUF ndiyo mwanzilishi wa siasa za maandamano kwenye nchi hii hadi mwenyekiti wake Prof. Ibrahimu Haruna Lipumba (Mnyamwezi) akavunjwa mkono. Na Cuf ikafikia kuitwa ngangari huku polisi wakijiita ngunguri. Ama kweli taifa limepokea wapiga kura wapya wengi sasa nimeamini..
Haya sasa! Wameanza kugombea maandamano! Tuliyasisi sisi enzi zile hata tukaitwa sijui nani vile? Sijui Prof. wetu ndie mwanzilishi wa siasa za maandamano! Wizi mtupu! Si juzi mlikuwa mnayapinga nyie kwa ushawishi wa magamba na baadhi ya viongozi wenu wa maisha ya ahera kwamba yanavunja amani, mara hii yamegeuka lulu ghafla?
Hapo kwenye red/bold kama usemavyo ni kweli kabisa taifa limepokea wapiga kura wapya. Waliokuwa wananyonya enzi zenu muflisi za ngunguri na ngangari ambazo hata thinking capacity yenu ilikuwa ndogo ndio vijana na wapiga kura makini na mahiri wa leo na ni viongozi na taifa la kesho. Heko watoto na vijana wa Tanzania. Sasa hivi tunataka hoja za kujenga taifa na sio siasa za shari na udini.