CUF wafuata mkia wa CHADEMA kuwaunga mkono maandamano nchi nzima

hakika ukweli kamwe haufichiki..iko siku sheikh akiuwawa na polisi, waislam nao wataingia barabarani..
 
Watawaunga mikono na kuwahamasisha waumini wao

ngoja tusubili tuone maana jana tu wametoa tamko kupinga vijana wa kiislamu kujihusisha na maandamano yanayo ratibiwa na uvccm arusha..hata hivyo jamaa kwa unafiki hawajambo kwahiyo wanaweza wakabadilika saa yoyote
 
Chama cha wananchi CUF kimeamua kuandaa maandamano ya nchi nzima ya kupinga mauaji na unyanyasaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi la polisi hapa nchini, hayo lalielezwa na naibu katibu mkuu wa CUF Julius Mtatilo wakati alipokuwa akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari.

CUF ilidhihilisha kuwa kumbe CHADEMA wako sahihi kabisa jinsi wanavyofanya maandamano yao japo vyama vingine vya siasa vinawapinga,

Haya maandamano ya CUF wameamua kuyaandaa baada ya mtu mmoja kupigwa risasi na polisi na kufa hapohapo huko Tabora na mbunge wa viti maalumu kukamatwa na polisi kwa kusema kuwa anafanya mikmutano bila kibali..
Hayo ndiyo yaliyojili ndugu zangu
Chanzo cha habari ni CLOUDS TV.
This is a stone in the liberation trend of the country!
Siamini mikono yangu!
 
Ni mtazamo mzuri, bt kumbuka wakina seif sasa ni serikali ya mapinduzi. Ukikumbuka hil bac utajua changamoto zilizopo hapo
 
labda hamad R alikuwa amewavumba macho, kwa hiyo baada ya kumtema macho yamefunguka na wanaona wananchi wanaonenewa na cdm wapo right, hawa jamaa wameshtuka mwaka 2015 wasinge pata hata ujumbe wa nyumba kumi huku bara
 
Huu ni mtego mkubwa sana kwa mashehe waliokuwa wanapinga maanadamano. Tuone sasa watawahamasisha waumini kuhudhuria au watawaambia kuto kuhudhuria.

CUF hawajui nafasi yao kwa sasa, si wapinzani si watawala, wachache wamepewa ulaji wameua chama. Huku bara akina Lipumba na Mtatiro wanatafuta pakutokea hawapati.
 
Jaman tz tunahitaji kuitafuta demokrasia kwa jasho otherwise will never be comfortable. Jaman kumbuken black people in amerika, walipigania haki zao ndo mana leo wako happy vile. So its our time
 
Sio CUF, ni Mtatiro ndio ametangaza kuwepo kwa maandamano. At the end atasusiwa maandamano na kubaki peke yake, kama yale aliyotisha ya kupeleka mapendekezo ya CUF ya katiba pale Ikulu
 
Itapendeza sana kama wapenda haki wote watayaunga mkono bila kujali kuwa cuf wamekuwa wakiyapinga maandamano ya Chadema. Hii ni nafasi nzuri sana ya kuwaaibisha wanafiki. MWENYE AKILI TIMAMU HAWEZI KULIITA JUA MBALAMWEZI ETI KWA SABABU TU MNAFIKI ALIYEKUWA ANALIITA MBALAMWEZI AMEANZA KULIITA JUA. Tusio wanafiki lazima tujitofautishe na wazanzibar wanaofurahia mauaji ya Watanganyika kwa sababu tu wakati wa mauaji ya visiwani wengi hawakuwa na mwamko wa kisiasa kupinga waziwazi mauaji hayo!!
 
Hebu tulete stori zenye mantiki humu jamvini,
Suala la CUF kufuata mkumbo wa CDM ni uzushi,
CUF walianza kuandamana kabla CDM haijasajiliwa,
Hata hivyo nimesoma magazeti leo CUF wame-stage maandamano na hawajasema yatafanyika lini na wapi na kwa staili ipi.
Sidhani kama CUF wana siasa za kuandamana nchi nzima ingekuwa hivyo tungesoma kwenye vyombo vya habari.
Poleni wote mnaoichukia CUF, they are holding it.
 
mtatiro ana wadhifa gani huko cuf, maana afisa habari ni yeye, katibu yeye, mkurugenzi mipango yeye nakuwa simuelewi kbs huyu dogo au na yeye ni kama mrema na tlp
 
wameona kuwa CCM B pekee haiwalipi umaarufu wao unakwisha na ukiisha CCM watawapa talaka yao
 
huu nao ni ujinga wa kisiasa kama sio upumbavu. hata wakiuawa wayu wangap kwa kuwa tu inaaminika ni wafuasiw a chadema basi cuf hawaandamani kupinga wala hawawaungi mkono chadema katika kupinga, akiuawa mmoja tu anayesadikiwa kuwa mwanachama wa cuf utasikia,,, aaa kumbe chadema wao sahihi!!... mazezeta haya!! ndo yanaamka sasa na kubaini uvunjwaji wa haki za binadamu baada ya mtu wao kuuawa. kumbe hata mtu wa ccm akiuawa na ccm wataamka!

siasa gani hizi hadi watu mtu wako auawe ndo ujue thamani ya binadamu na ukatili wa polisi? ina maana tanzania ya leo chama kinapanua domo lake pale tu mwanachama wao anapouawa?

nashauri chadema wajitokeze katika maandamano yatakayoitishwa na cuf kulaani mauaji haya ili kuonyesha kuwa chadema wanalaani mauaji ya raia yanayofanywa na polisi bila kujali itikadi za kisisa na hapo watadhihirisha ukomavu wao na kupata crediti zaidi katika harakati zao za kutetea haki za binadamu

Nilichogundua ni kua wafuasi wengi wa chadema hawakua wafuatiliaji wa siasa ila sasa ndio wanadhani wameamka wakwanza kumbe watu walishaamka zamani sana.

Hivyo niwaulize wale watu waliokufa zanzibar kipindi cha nyuma,zaidi ya arobaini 1995 na 2001

Chadema haikuapo? mbona walioandamana walikua CUF pekeyao.

Au damu yawale ilikua ya buluu haiumi?

Ama ni kweli waswahili walisema:[muda aamkapo mtu ndio asubuhi yake.]
 
Itapendeza sana kama wapenda haki wote watayaunga mkono bila kujali kuwa cuf wamekuwa wakiyapinga maandamano ya Chadema. Hii ni nafasi nzuri sana ya kuwaaibisha wanafiki. MWENYE AKILI TIMAMU HAWEZI KULIITA JUA MBALAMWEZI ETI KWA SABABU TU MNAFIKI ALIYEKUWA ANALIITA MBALAMWEZI AMEANZA KULIITA JUA. Tusio wanafiki lazima tujitofautishe na wazanzibar wanaofurahia mauaji ya Watanganyika kwa sababu tu wakati wa mauaji ya visiwani wengi hawakuwa na mwamko wa kisiasa kupiinga waziwazi mauaji hayo!!


Mkuu mauwaji ya wazanzibari watu hawakua na muamko au kwakua ile ilikua damu ya kunguni?

Watu hawakua na muamko lakini hata chadema kama chama kilishindwa kulaani mauwaji yale?

Nakumbuka wakati hule watanganyika wengi walituona wazanzibari ni wakorofi ndio maana wanauwawa na polisi sasa yamehamia kenu ndio munajua kutetea haki leo.

Njia yoyote mutakayoipita leo znz ilishapita huko,(matumaini yangu mutajifunza kupitia zanzibar hapo baadae)
 
Chadema ni kama katapila linachonga barabara na wengine wanafuatia,tulivyoanza Chadema kufanya maandamano Cuf walitutupia vijembe sn Leo wanakula kile kile walichokitapika.Chadema go go go peoplesssssssss powerrrrrrrrrrrrrrr .

Kaazi kweli kweli yaani kwako wewe historia na sia za Tanzania zimeanzia 2010 baada ya Dr. Slaa kugombea urais umesahau kuwa CUF ndiyo mwanzilishi wa siasa za maandamano kwenye nchi hii hadi mwenyekiti wake Prof. Ibrahimu Haruna Lipumba (Mnyamwezi) akavunjwa mkono. Na Cuf ikafikia kuitwa ngangari huku polisi wakijiita ngunguri. Ama kweli taifa limepokea wapiga kura wapya wengi sasa nimeamini..
 
Wakati CHADEMA wanaanza maandamano kanda ya Ziwa Lipumba na Mbatia walifanya mikutano kadhaa (wakiongozana) wakipinga na kushawishi wananchi wasiwasikilize CHADEMA,leo wataenda kwa wananchi wale wale kuhubiri wale waliyokuwa wanapinga....haya na tusubiri tuone
 
Back
Top Bottom