Elections 2010 CUF wafanya unyama Tandahimba!

faithful

JF-Expert Member
Aug 10, 2010
378
33
baada ya matokeo ya ushindi wa ccm kutangazwa tandahimba cuf wapingana na matokeo kwa kufanya vurugu wachoma nyumba na gari la mshindi moto...
hiyo ni demokrasia gani?
 
Huo ni mwanzo tu. Kama NEC wantaendelea kuchelewesha na kuchakachua matokeo then hali inaweza kuwa tofauti sehemu nyingi tu by 2morrow!!
 
Kwenye wizi hakuna demokrasia mambo kama hayo ndio yanayohitajika ,hivi ulitegemea jamaa waibe kura arafu washangae ,safari hii mwizi yatamkuta mauti ,ole wao wezi wa uchaguzi huu ni kipigo kwa kwenda mbele ,hata kama uchaguzi utamalizika lakini usalama wao utakuwa mashakani.Pindipo wakiwa proved wamekwiba.
 
Nec wawe makini sana ktk kuyatangaza haya matokeo. Wasipelekwe pelekwe na ccm, wasimame kwenye haki.
"Vurugu itaanzashwa na chama tawala"
 
Kwenye wizi hakuna demokrasia mambo kama hayo ndio yanayohitajika ,hivi ulitegemea jamaa waibe kura arafu washangae ,safari hii mwizi yatamkuta mauti ,ole wao wezi wa uchaguzi huu ni kipigo kwa kwenda mbele ,hata kama uchaguzi utamalizika lakini usalama wao utakuwa mashakani.Pindipo wakiwa proved wamekwiba.

Je na Shein mtamchomea nyumba yake na gari lake moto? Maana kama JK atashinda kwa lazima bara na Shein atashinda kwa lazima visiwani.
 
HIyo ndio njia ya kuelekea demokrasia ya kweli kwa wapinzani wa kweli kama CUF, sio chadema
 
baada ya matokeo ya ushindi wa ccm kutangazwa tandahimba cuf wapingana na matokeo kwa kufanya vurugu wachoma nyumba na gari la mshindi moto...
hiyo ni demokrasia gani?
hiyo ndo Tanzania yenye amani jamani!??? ccm angalieni haya!
 
Kwenye wizi hakuna demokrasia mambo kama hayo ndio yanayohitajika ,hivi ulitegemea jamaa waibe kura arafu washangae ,safari hii mwizi yatamkuta mauti ,ole wao wezi wa uchaguzi huu ni kipigo kwa kwenda mbele ,hata kama uchaguzi utamalizika lakini usalama wao utakuwa mashakani.Pindipo wakiwa proved wamekwiba.

kwani uliona wakati wanaibiwa?yaani watanzania wanatakiwa kukubali matokeo wanaposhindwa...acheni kuchochea fujo!
 
Yes..thats the way to go.

Kwani ntu unapotaka kuangua madafu kutoka kwa n'nazi wako unahitaji ruhusa ya nani??

Kama haq ipo mmbele yako TAKE IT
 
CCM waache wizi wa kura hivi wanaongoza kwa ridhaa ya nani.....dola au wapigakura..............
 
kwa kukusaidia, democrasia si kuwa mtu wa ndio mzee......... wa kulaumu ni wale wanaokataa sauti ya umma
 
Wananchi wameonyesha kuwa CCM ni chama kinachoongoza kwa mabavu. Kwa matokeo haya, ambayo CCM inayachakachua, inaonyesha kuwa nguvu ya umma ni nguvu ya Mungu.

Iko siku haki itapatikana. Hata Unguja walisubiri sana...na sasa wanakaribia kupata haki.

Roho yangu ni nyeupe, na Inshallah CCM dhamira inawasuta.
 
Si demokrasi kufanya uhalifu kwa kisingizio chochote!!!

Nakubaliana na wewe uhalifu ni uhalifu tu mwizi wa kura ni sawa na mchoma moto gari. Dawa ya watu kama hawa ni kuwafanya wayahame majimbo ambayo hawakubaliki. Yaani wasiwe na amani kabisa labla waishi dodoma.

Huwezi kuhesabia kura zilizopigwa hadharani kwenye mapaja kwa kufichaficha. Ukitaka amani itawale transparency is the best option. Kwa nini watu hawayagomei matokeo ya kwenye mipira?, ni kwa sababu huwa fair games. CCM wanataka kujaribu ujasiri wa watu waliokata tamaa ya kuishi sasa watajuta.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom