Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Naibu Katibu Mkuu wa CUFZanzibar.
Chama cha Wananchi (CUF), kimeeleza kuchoshwa na vitendo vya hujuma dhidi ya mali na ofisi zake.
Kauli hiyo ya CUF imetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alipotembelea ofisi za chama hicho zilizovunjwa na baadhi ya mali kuchomwa moto katika maeneo ya Dunga Kiembeni mkoani Kusini Unguja.
Mazrui na ujumbe wa viongozi waandamizi wa CUF, walifanya ziara ya dharura kukagua uharibifu na kubaini hasara iliyotokea.
Inadaiwa ofisi hizo zilivunjwa na watu wasiojulikana, Jumanne jioni wiki hii na kufanya uharibifu wa vitu mbalimbali vilivyokuwamo ndani na nje.
“Tumekuwa kimya kwa muda mrefu, hizi ni njama za makusudi dhidi yetu, sasa tunasema hatutaweza kuvumilia vitendo hivi vya kihuni na vya kihalifu wanavyotendewa viongozi na wafuasi wetu visiwani Zanzibar,” alisema Mazrui.
Mkurugenzi huyo alisema tayari wametoa taarifa katika Kituo cha Polisi Dunga na askari walifika kukagua uharibifu uliofanyika. Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui