CUF: Wabunge 10 kufukuzwa; Maalim Seif adaiwa kudidimiza chama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF: Wabunge 10 kufukuzwa; Maalim Seif adaiwa kudidimiza chama!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 17, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  November 17, 2011
  Mtanzania
  Imeandikwa na Khamis Mkotya, Dodoma


  • Yumo Hamad Rashid Mohamed
  • Maalim Seif adaiwa kudidimiza chama
  • Wajumbe wa Baraza Kuu roho juu

  Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa, chanzo cha mgogoro huo ni hatua ya wanachama kutoridhishwa na mwenendo wa chama chao.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu, wanachama na viongozi wa ngazi za chini, wamekasirishwa na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana ambayo yamekishusha chama hicho kutoka nafasi ya pili hadi ya tatu.


  Wanachama hao, wamekuwa wakihoji ni kwa namna gani chama hicho kimepoteza uongozi wa Kambi ya Upinzani katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  Pia wamekuwa wakitaka kujua ni kwa sababu gani kura za Mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Lipumba, zilishuka katika uchaguzi huo kwa kuwa alipata kura 600, 000 sawa na alizopata mwaka 1995 alipogombea kwa mara ya kwanza.


  Kabla ya uchaguzi wa mwaka jana, kambi ya upinzani bungeni ilikuwa ikiongozwa na CUF na pia chama hicho kilikuwa chama kikuu cha upinzani nchini.


  "Kama unavyojua, kambi ya upinzani bungeni hivi sasa inaongozwa na CHADEMA, lakini kabla ya uchaguzi wa mwaka jana, kambi hiyo ilikuwa ikiongozwa na CUF,


  …Sasa wanachama wamekuwa wakihoji sababu za chama kufanya vibaya namna hiyo hadi kunyan'ganywa nafasi ya kuongoza kambi ya upinzani bungeni.


  "Si hilo tu, CUF ndiyo kilikuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania, hivi sasa nafasi hiyo imechukuliwa na CHADEMA, hili si jambo dogo la kulifumbia macho.


  "Kimsingi ukitazama hali ya chama chetu kwa sasa inasikitisha, chama huku bara kinashuka siku hadi siku, kinazidi kupoteza umaarufu.


  "Mfano mzuri ni uchaguzi mdogo wa Igunga, CUF ilipata kura 2,000 kutoka kura 11, 000, hii ni aibu.


  "Kwa muda mrefu wanachama na baadhi ya viongozi wa chini, wamekuwa wakihoji sababu zilizokifikisha chama mahali hapa, lakini viongozi wa ngazi ya juu hawatoi majibu," kilisema chanzo hicho.


  Wanachama na viongozi wa ngazi ya chini, sasa wanadaiwa kutokuwa na imani na viongozi wa ngazi ya juu, hususani Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.


  Maalim Seif, ambaye kwa sasa ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), anadaiwa kuwa na kiburi na kwamba viongozi wasiokubali msimamo wake, amekuwa akiwageuza maadui zake kisiasa.


  Inadaiwa kwamba, Maalim Seif, hivi sasa ameanza mkakati wa kupita katika matawi mbalimbali kuwashawishi wanachama wa baadhi ya majimbo wawakatae baadhi ya wabunge ambao wamekuwa na msimamo tofauti na wake kuhusu uendeshaji wa chama.

  Katika wabunge hao kumi waliopo katika mpango huo, mlengwa namba moja ni Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, ambaye anaonekana tishio kwake iwapo wanachama wataamua kufanya mabadiliko ya uongozi.


  Hamad ambaye alikuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni kwa miaka kumi, ni miongoni mwa viongozi ndani ya chama hicho waliowekewa kalamu nyekundu kutokana na msimamo wao.


  "Kutokana na kelele hizi za wanachama za kuhoji, mpango uliopo sasa ni kuwafukuza wabunge kumi, wajumbe tisa wa Baraza Kuu na viongozi wengine ndani ya chama.


  "Hawa ni wale wenye msimamo usiyoyumba ndani ya chama na siku zote wamekuwa na dhamira ya kutaka kukinusuru chama.


  "Siwezi kuwataja hawa wabunge, lakini mlengwa namba moja ni Hamad Rashid
  Mohamed.


  "Maalim Seif anafanya hivyo kwa sababu anamuona Hamad ni threat (tishio) kwake anaweza kuchukua nafasi yake, kwani Hamad anakubalika pande zote mbili hivyo ni rahisi kuwa katibu mkuu," kilibainisha chanzo hicho.


  Taarifa za chanzo hicho zinadai kuwa Maalim Seif alikwishamuandaa siku nyingi mrithi wake ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu, ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar.


  "Maalim Seif anaendesha mkakati huo wa kutaka kuwasambaratisha mapema viongozi wenye ushawishi ndani ya chama ili aweze kufikia malengo ya kumkabidhi chama Jussa.


  "Maalim Seif tangu awe Makamu wa Kwanza wa Rais, amekuwa hafanyi kazi za kukijenga chama, yeye yupo ‘bize' na kazi za Serikali.


  "Maalim Seif amehodhi Katiba ya chama kwani Katiba inampa nguvu kubwa kuliko mwenyekiti, Mwenyekiti wa CUF yupo kama bendera inayofuata upepo tu, hana nguvu.


  "Mfano ni kwamba, uamuzi wa chama chetu kuingia katika maridhiano ambayo baadaye tuliingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, chama hakikushirikishwa, ulikuwa ni uamuzi wake binafsi.


  "Baraza Kuu la Uongozi katika CUF ndiyo NEC na Kamati Tendaji, ndiyo kama vile Kamati Kuu (CC) ya CCM, lakini hakuna chombo hata kimoja katika hivi vilivyoshirikishwa .


  "Hata hivyo, baadaye hoja hiyo ililetwa katika kikao cha Baraza Kuu la Uongozi wakati utekelezaji waka umeanza kufanyika," kilisema chanzo hicho.


  Wanachama hao wanamtuhumu Maalim Seif, kuwa ndiyo mchawi wa maendeleo ya chama hicho, kwani amekuwa kikwazo na hivyo kukifanya chama hicho kishindwe kufikia malengo yake ya kisiasa.


  "Uchaguzi wa mwaka 2005, CUF haikupata wabunge bara, hivyo Baraza Kuu la Uongozi lilipitisha uamuzi kuwa wabunge wote ambao walikuwa ni wa Zanzibar tu wawe walezi katika majimbo ya bara ili kujenga chama.


  "Lakini, hoja hiyo Maalim Seif aliipinga katika kikao cha Kamati Tendaji. Hii maana yake ni kwamba, mkakati wa CUF ni Zanzibar na wala si bara, huku bara chama kipo kama daraja tu," kilisema chanzo hicho.


  Chanzo hicho kilizidi kuweka wazi kuwa, hoja hizo ziliibuka tena katika mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi uliofanyika Novemba 3-4, mwaka huu katika Ukumbi wa Hoteli ya Lamada uliopo Ilala, Jijini Dar es Salaam.


  Inaelezwa kuwa Maalim Seif, aligeuka mbogo katika mkutano huo baada ya baadhi ya wajumbe kuhoji ni kwa namna gani chama hicho kimeshuka na kupoteza mvuto mbele ya wananchi.


  HAMAD RASHID AJIBU MAPIGO
  Hamad Rashid Mohamed alitafutwa na alipozungumza na MTANZANIA alikiri kuwapo kwa mpango huo aliouita wa kijasusi.

  Katika mazungumzo yake, Hamad alithibitisha kuwa ipo ajenda ya uasi inayoandaliwa dhidi yake pamoja na wanachama wengine 19, wakiwamo wabunge kadhaa.


  Hamad, alisema tayari amekwishamwandikia barua Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, kumueleza juu ya mpango huo wa kijasusi.


  Katika barua hiyo ndefu, ameelezea masikitiko yake namna asivyoridhishwa na mwenendo wa chama hicho kwa sasa na kwamba mahusiano baina yake na Katibu Mkuu, Maalim Seif si mazuri, hatua inayofanya aundiwe njama hizo.


  Alisema Maalim Seif, anampa nguvu kubwa katika shughuli za chama Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa.


  Mbali ya Hamad, wabunge wengine wanaoweza kutimuliwa ni Mbunge wa Lindi Mjini, Salum Khalfan Barwany na Mbunge wa Mkanyageni, Habibu Mohamed Mnyaa.


  Wengine ni Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa, Mbunge wa Chambani, Salim Hemed Khamis na Mbunge wa Mtambile, Masoud Abdallah Salim


  Barua hiyo ya Novemba 12, mwaka huu yenye kichwa cha habari kisemacho: YAH. Viongozi 19 kuandaliwa ajenda ya uasi ndani ya chama kwa madhumuni ya kuwazuia kugombea uongozi wa juu wa chama.


  Hata hivyo katika barua hiyo, Hamad amemweleza Profesa Lipumba kuhusu nia yake ya kugombea nafasi ya ukatibu mkuu wa chama mara uchaguzi wa ndani utakapowadia.


  "Naomba urejee kikao chetu chini ya uwenyekiti wako tulichofanya Zanzibar, Masons Hotel baina yangu, Makamo Mwenyekiti na Katibu Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, kilichozungumzia pamoja na mabo mengine, sababu zilizonifanya kuandika kijitabu nilichokiita ‘YALIO JIRI' ambacho nilikiandika baada ya kubaini njama zilizopangwa za kuniua kisiasa.


  "Katika kikao hicho, baada ya mazungumzo ya muda mrefu, uliniuliza je, katika hatua tuliyofikia tufanye nini kukinusuru chama chetu na kujenga mustakbali wa chama chetu?.


  Pili, tuitishe kikao cha pamoja cha Wabunge na Wawakilishi, wewe ulisema utakua haupo, jukumu hilo la kuandaa program hiyo, ukamkabidhi Katibu Mkuu na kumuagiza Makamu asimamie; Hadi leo program hiyo haijafanyika," ilisema sehemu ya barua hiyo.


  Kuhusu nafasi ya ujumbe wa Baraza Kuu la Uongozi, Hamad alisema ameacha kuingia kutokana na viongozi wake kutoonyesha iwapo kweli anahitajika.


  "Nilikuandikia ili kuthibitisha ujumbe wangu, hadi leo sikupata majibu ya barua
  ikinielekeza kuwa mimi bado ni mjumbe wa Baraza Kuu Taifa, kutokanana tafsiri yako ya Katiba;


  "Hivyo, nimeshindwa kuhudhuria vikao na hasa nilipoona hata waliokuwa wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mhe Abuubakar Khamis Bakari, Khalifa Suleiman na Masoud Abdulla Salim, wameondolewa katika kamati kwa kuwa wao waliingia katika kamati kwa mujibu wa nafasi zao za Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Uwakilishi na mawaziri vivuli katika Bunge.


  "Hivyo kauli ya kuwa mimi ni mjumbe wa Baraza siyo sahihi kutokana na uthibitisho huo. Lakini zaidi kauli aliyoitoa Katibu Mkuu Pemba siku ya Sikukuu ya Eid Al Hajj kuwa Mhe.Abuubakar yeye hakunung'unika alipofukuzwa.


  "Hiyo inathibitisha kuwa, mimi sikuwa natakiwa tena ndani ya Baraza na uongozi wote wa chama, ndiyo maana hadi leo hukunijibu barua yangu wala kuagiza kuwa nijibiwe.


  "Hilo halinipi shida hata kidogo, maana malengo nayafahamu vyema tokea wakati tunagombea nafasi ya ubunge ndani ya chama.


  "Baada ya Katibu Mkuu kukutana na Wenyeviti na Makatibu wa Wilaya Pemba na baadhi viongozi waandamizi wa chama, Wete Pemba, aliwapa kazi viongozi hao waandae vikao vya Kamati Tendaji na mikutano mikuu ya wilaya ili kuwajulisha viongozi tuhuma hiyo inayoitwa ya uasi ndani ya chama.


  "Pia aliwashutumu viongozi hasa wabunge wakongwe na baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu Taifa ambao walitoa hoja zao ndani ya kikao halali cha Baraza Kuu juu ya udhaifu wa utendaji, matumizi mabaya ya fedha na kudhoofika kwa chama hasa bara kutokana na Katibu Mkuu kushindwa hata kufanya mkutano mmoja wa kampeni bara wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana


  "Wakati mimi pamoja na kuwa na uchaguzi katika jimbo nilifanya mikutano ya kampeni Tanga, Mbeya, Pwani na Dar es Salaam, ikiwa pamoja na kushindwa vibaya uchaguzi wa Igunga, licha ya kutumia Sh milioni 300.


  "Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu waliochangia ajenda ya hali ya kisiasa wote waliitwa vibaraka wangu na kwamba mimi eti napewa pesa na mhe Pinda (Waziri Mkuu, Mizengo Pinda) kwa ajili ya kuiua CUF.


  "Viongozi hao ni Mheshimiwa Khalifa Suleiman, Habib Mnyaa, Masoud Salim, Salim Hemed, Salum Khalfan Barwany, Rakesh, Doyo, Masoud Abdulla, Kirungi, Shoka Khamis,Yaasin, Masoud n.k.


  "Kilichonifanya nikuandikie ni kukutaarifu vitendo vinavyofanywa na Makamu wako (Machano Khamis Ali), Katibu Mkuu na wasaidizi wake na sisi wanachama 19 kututangazia uasi ndani ya chama eti mimi nataka kugombea ukatibu mkuu (ambao kwa chama chetu ni utume) na eti Mhe. Barwany (Mbunge wa Lindi Mjini) anataka kugombea uenyekiti ambao pia nao ni utume ndani ya Chama chetu).


  "Pamoja na mvutano mkali uliotokea katika kikao hicho hasa kutoka kwa wajumbe wa Jimbo langu la Wawi ambao wanaelewa kiini na ukweli wa mipango ya Naibu Katibu Mkuu Jussa Ladhu na wenzake wakipewa nguvu na Katibu Mkuu.


  "Hivyo, walikataa hoja hii hasa kwa vile mimi sikupewa nafasi ya kujieleza; lakini viongozi wa wilaya waliamua kuitisha Mkutano Mkuu wa Wilaya ili kutimiza agizo la Katibu Mkuu (mimi hadi leo sijaalikwa).


  "Kukuthibitishia kuwa mpango huu ulivyoandaliwa kijasusi na kuzidi kukiua chama, Naibu Katibu Mkuu Jussa Ladhu ambaye kinyume cha Katiba amepewa Ukatibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, leo tarehe 12.11.2011 kwa kutumia viongozi wa Blue Guard, ameitisha kikao cha Blue Guard na kuwapa kazi ya kuzunguka nchi nzima kuchafua majina yetu," alisema.


  Hamad aliendelea kueleza katika barua hiyo.


  "Fedha ya walipa kodi na michango ya wabunge na wawakilishi inatumika kwa kuua chama badala ya kuendeleza chama.


  "Wilaya za Bara, sasa ni miezi sita hawajapelekewa pesa zao za kila mwezi, wajumbe wakihoji wanaitwa WASALITI wa Chama. Mhe, Mwenyekiti, nakuandikia taarifa hii fupi kwa madhumuni ya kukupa fursa ili upate angalau muhtasari wa YANAYO JIRI huku katika chama unachokiongoza.


  "Wala si kwa madhumuni ya kuomba shufaa, kwani haya nilikwishayaeleza katika kijitabu changu cha yaliyojiri ambacho uliniomba nisiendelee kukisambaza, lakini huenda nikakisambaza zaidi ili Watanzania waujue upande wa pili wa shilingi,".


  Katika barua hiyo, Hamad alimalizia kwa kusema. "Mhe. Mwenyekiti, hakuna asiyejua na kutambua mchango wa Maalim Seif Sharif Hamad katika mustakabali wa kisiasa Zanzibar na Tanzania kwa jumla namna alivyotoa mchango wa kuhakikisha nchi inabaki katika amani.


  "Ni dhahiri anafaa kuheshimiwa na kuenziwa ili mradi mwenyewe aamue kupewa heshima hiyo, kama alivyoamua Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela na hayati Mwalimu Nyerere," alisema Hamad.

   
 2. only83

  only83 JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Msiba wa CUF upo karibu...
   
 3. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  na bado upinzani wakweli utatokea CCM kumeguka na Tayari imeshameguka kwa kuzaa chadema kaaaaaazi kweli kweli
   
 4. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Hivi ni kweli kabisa hawa cuf hawaoni mbaya wao ni nani, au wameamua kufumba macho na kuziba masikio wasione kinachoendelea hivi sasa huko bungeni kwenye kupitisha mswada wa sheria ya katiba
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Hamad Rashid yuko sahihi CUF Maalim Seif ni mungu mtu.
   
 6. Sordo

  Sordo JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CUF lazima wasmbaratike maana wameshapoteza nguvu ya kisiasa baada ya kufunga ndoa na magamba
   
 7. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #7
  Nov 17, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Kifo cho kiko karibu na hawana siku nyingi tutawapiga chepe rasmi. CUF walipoteza uimara baada ya ndoa ya lazima na Ccm. Ndoa imeanza kuwa shubiri wanaona rangi mbaya wameanza kuhaha.
   
 8. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ccm wajanja sana waliwatega wakategeka vizuri neno ccm b haliwezi kuondoka na michango yao ya kuponda vyama vya upinzani bungeni wakati wao pia wanajiita wapinzani ni kituko badala ya kupambana na chama tawala wao wanafanya collabo na ccm kupambana na chadema hakika cuf haiko salama,maalim seif ndio yule anakula bata! Ukimwambia ccm mbaya anakuelewa,,,,,,,,!
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sitaiamini hii habari mpaka mwandishi aje na upande wa Maalim seif anasema. Huwezi kumtuhumu mtu namna hii halafu usimpe nafasi ya kujitetea, hata kama hatataka kujibu
   
 10. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  "Kilichonifanya nikuandikie ni kukutaarifu vitendo vinavyofanywa na Makamu wako (Machano Khamis Ali), Katibu Mkuu na wasaidizi wake na sisi wanachama 19 kututangazia uasi ndani ya chama eti mimi nataka kugombea
  ukatibu mkuu
  (ambao kwa chama chetu ni utume)
  na eti Mhe. Barwany (Mbunge wa Lindi Mjini) anataka kugombea
  uenyekiti ambao pia nao ni utume ndani ya Chama chetu).
  Hapo red: hii ndiyo sababu chama hakibadilidishi viongozi wajuu Sasa hawa watakuwa mitume hadi lini ?????????
   
 11. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  mhh CUF Hoiiii, labda matatiro agombee ukatibu mkuu
   
 12. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mitume wanaendelea kuwa mitume hata wakifa wanaitwa mitume............hawaitwi marehemu!!
  Imekula kwao.
   
 13. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,290
  Likes Received: 598
  Trophy Points: 280

  Wakati hiyo ndiyo hali halisi ndani ya CUF, Rashid anapata ujasiri wa kuisema CDM kuwa ni chama cha kifamilia na kifalme. Poor Hamad!

   
 14. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #14
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Huo ni mwanz tu ,wanacheza na nguvu ya umma
   
 15. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ife tu hiyo CUF ili tubaki na CUF original CCM. CUF wamekuwa photocopy ya CCM. Ya nini basi kuhangaika na photocopy ilihali original CUF ipo ambayo ni CCM?
   
 16. s

  sawabho JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Hawa wanajenga nyumba moja. Kwa nini wanagombea fito? Nyumba ikiwa imara si ndio itakuwa raha yao wote?
   
 17. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Haa ndio malipo ya uasi wanaofanyia watanzania katika mjadala wa katiba
   
 18. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hamadi akifukuzwa ataenda ccm
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Toka wawe CCM B naona wapemba wamesha wachoka sasa.
  Kibaya zaidi Dr.Shein ndo anakazania kweli zao la karafuu kuinua kipato kwa wapemba yeye Sharif ananawili tu Unguja hata usemi wake wa sawa sawa siku hizi kasahau kabisa 2015 sio mbali.
   
 20. k

  kitumanga Member

  #20
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kilichobakia ni muungano kamili wa ccm + cuf kuzalisha chama kipya cjui watakiitaje, vinginevyo hakuna cuf tena tz. tuacheni cdm tuendelee kulisongesha cufccm mtaona vumbi 2. “vita vya panzi furaha kwa kunguru”
   
Loading...