CUF waandamana na kutaka tume za uchaguzi zivunjwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF waandamana na kutaka tume za uchaguzi zivunjwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Oct 1, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CHAMA cha Wananchi (CUF) jana kilitekeleza azma yake ya kuzipinga Tume za Tanzania na Zanzibar( Nec na Zec) kwa maandamano na kusisitiza kuwa tume hizo zivunjwe, ili ziundwe tume mpya huru zitakazowajibika kwa misingi ya demokrasia.

  Maandamano hayo yalipokewa na msajili wa vyama vya siasa, John Tendwa.
  Awali waandamanaji walikuwa wamejiandaa kuelekea kwenye Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa , lakini walilazimika kubadili njia baada ya askari hao kufunga barabara eneo la Mnazi Mmoja na kuwaamuru kwenda Kidongo Chekundu jambo ambalo lilitekelezwa.

  Katika mkutano wao wa hadhara uliofanyika viwanja vya Kidongo Chekundu baada ya maandamano yaliyoanzia Makao Makuu ya chama hicho Buruguni Dar es Salaam saa 5:00 asubuhi, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Juma Duni Haji, alisema hakuna mbadala wa madai yao zaidi ya tume hizo mbili kuvunjwa.

  Alisema tume hizo hazifai na ni lazima zivunjwe kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010 na kuundwa tume zingine huru zitakazofanya kazi katika misingi ya demokrasia.

  “Mheshimiwa msajili wa vyama ambaye pia ni mlezi wa vyama, hakuna mbadala wa madai yetu isipokuwa ni kuvunjwa kwa tume zote mbili na kuundwa kwa tume mpya za uchaguzi zenye misingi ya demokrasia,” alisema Duni.

  Alisema hakuna kufuli isiyo na ufunguo na kwamba kama haina ufunguo hiyo si kufuli na kama umepotea, wananchi watavunja mlango waingie ndani.

  “Tume hii inateuliwa na Rais aliyepo madarakani ambaye pia ni mgombea wa urais nchini, anaweza kumvua madaraka mjumbe yeyote wa tume pale atakapoona kuwa ana tabia mbaya. Haya ni madaraka makubwa kwa rais,” alisema Duni.

  Akizungumza baada ya risala hiyo, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema wanadai tume mpya zilizo huru na misingi ya demokrasia kwa sababu ni kichocheo cha haki.

  “Tunadai tume huru yenye misingi ya demokrasia kwa sababu, demokrasia ni nyenzo ya kuleta haki na maendeleo katika jamii, lakini tume zilizopo si huru wala hazina uwezo wa kusimamia chaguzi huru,” alisema Profesa Lipumba.

  Alisisitiza kwamba tume hizi hazifai, na hawazitaki tena, badala yake wanataka tume mpya. .

  "Leo Dar tumeanza, Morogoro wanajibu kesho (leo) na tutafanya hivyo kwa nchi nzima,” alisema.

  Naye makamu mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis alisema kuwa siku zote haki haiombwi na wala haipatikani kwenye sahani bali, inatafutwa, aliwataka wananchi kuitafuta haki yao kwa gharama zote.

  “Ndugu zangu haki haiombwi, bali inatafutwa, tusidanganyike na asikudanganye mtu kwamba, haki yako utaipata katika kisahani. Haki inatafutwa, kazi kwenu,” alisema.

  Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alisema chama chake kimeitisha maandamano hayo kwa niaba ya Watanzania wote.

  “Kama serikali ina nia ya dhati kukuza na kuendeleza demokrasia nchini, tunahitaji mambo mawili; Katiba mpya yenye misingi ya demokrasia na tume huru za uchaguzi ambazo zitakuwa na uwezo wa kuendesha na kusimamia uchaguzi huru na wa haki,” alisema Maalim Seif na kuongeza:

  “Tumechoka kutuchagulia viongozi wasio na uwezo wa kuongoza, tunataka Watanzania wawe na maamuzi na uhuru wa kuchagua viongozi wanaoona kuwa wanaweza kuwaongoza na sio tume ifanye hivyo,”

  Alibainisha kuwa, chanzo cha vurugu duniani kote ni kwa wananchi kuona kuwa wananyimwa haki zao ambazo wanastahiki kupata katika nchi zao.

  “Mwalimu Julius Nyerere alisema kuwa, yale yanayotokea katika nchi za wenzetu tusione kwamba hayawezi kutokea Tanzania.
  Naitahadharisha serikali ikiwa itaendelea kujifanya kiziwi na kuendelea kuzitia mfukoni haki za wananchi, uvumilivu wa Watanzania unaweza kuyoyoma wakati wowote kuanzia sasa,” alisema Maalim Seif.

  Katika hatua nyingine, Maalim Seif alisema serikali imekosa uvumilivu kwa kumkamata mbunge wa chama hicho, Nuru Awadh Bafadhili kwa kuwa ilitakiwa kufanya hivyo baada ya ushauri wa spika.

  “Unamkamata mbunge, eti kwa kosa la kumkashifu rais, haya uliza hivyo alivyokashifiwa, eti ameambiwa anachekacheka.

  Akizungumza katika mkutano huo Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa alisema amepokea risala yao na kuahidi kuifanyia kazi.

  “Lakini pia mwenyekiti na katibu mkuu kisheria ninyi ni wajumbe wa Baraza la Ushauri la Vyama vya Siasa ambalo litaanza kazi zake Oktoba mwaka huu, hivyo haya tutayafikisha na kujadiliwa katika baraza hilo,” alisema Tendwa na kuongeza: “Baraza hili halina kawaida ya kuishauri serikali bali litatoka na agizo kwa serikali.”

   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni kweli Kikwete huwa anachekacheka na zaidi anapozungumza akiwa anafuraha ndani ya moyo wake ,japo haijulikani ni kitu gani hicho kinachomfanya awe hivyo kwani hata Hilary Clinton nae anayo tabia hiyo tena Hilary ndio mwisho kabisa anaweza akaangua kicheko kikubwa sana na mliopo mkabaki kushangaa.
   
Loading...