CUF upande wa Prof. Lipumba wadai Maalim Seif anajiandaa kuhamia ACT-Wazalendo

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
Chama cha Wananchi (CUF) upande wa mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba umedai Maalim Seif Sharif Hamad anajiandaa kuhamia ACT-Wazalendo.

Kimesema Maalim Seif ambaye ni katibu mkuu wa chama hicho kwa sasa yuko mbioni kutimkia ACT.

Wakati CUF upande wa Profesa Lipumba wakiibua madai hayo, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa Maalim Seif, Ahmed Mazrui amelieleza Mwananchi leo Jumatano Desemba 26, 2018 kuwa ndio kwanza anasikia madai hayo na hayupo tayari kuyazungumza.

Mgogoro ndani ya CUF ulianza baada ya Lipumba kurejea katika uongozi mwaka 2016, ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu alipojiuzulu.

Jambo hilo liliibua mgogoro wa uongozi baada ya ofisi ya msajili kutangaza kumtambua Lipumba kama mwenyekiti na kusababisha pande hizo mbili kukimbilia mahakamani na kufungua kesi kadhaa ambazo zinaendelea.

Akizungumza leo Jumatano katika mkutano na waandishi wa habari katibu wa kamati ya ulinzi na usalama wa CUF, Khalifa Suleiman Khalifa amedai vyama sita vya upinzani vilivyokutaka Zanzibar wiki iliyopita moja ya ajenda yao ilikuwa namna gani Maalim Seif atakubaliana na ACT-Wazalendo.

Amesema miongoni mwa makubaliano ni upande wa Maalim Seif uachiwe nafasi zote za uongozi upande wa Zanzibar na Zitto Kabwe ambaye ni kiongozi wa ACT, wachukue uongozi wa Tanzania Bara.

Amedai kuwa hata kama Maalim Seif ataondoka CUF, wataendelea kuwa imara huku akiwataka wote watakaoambatana na katibu mkuu huyo kwenda ACT kutosita kwa sababu uamuzi wao utaheshimiwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Lipumba na Seif wanamatatizo sana...

Kutwa migogoro alafu ndiyo tuwape uRais...

Kama ya chama tu yanawashinda ya kitaifa na kimataifa watayaweza...


Cc: mahondaw
 
Mwanachama wa chama kimoja anapokuwa msemaji wa chama kisichomuhusu. Wanasiasa man akili kweli?
 
Back
Top Bottom