CUF: Tunampongeza shehe Ponda kwa kujitokeza kipindi hiki ambacho viongozi wengi wa dini na kisiasa wamejazwa woga

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Chama Cha Wananchi (CUF) kimetoa pongezi kwa Sheikh Ponda baada ya jana kuwataka Watanzania bila kujali itikadi zao na imani zao za dini kwa pamoja kushikamana kutetea na kulindwa kwa haki za binadamu, uhuru wa Kidemokrasia na utawala wa sheria.

Sheikh Ponda alisema hayo jana baada ya kumtembelea Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu jijini Nairobi anakopatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi mnamo Septemba 7, 2017 mjini Dodoma.

Kufuatia kauli hiyo wa Sheikh Ponda Chama Cha Wananchi CUF kimempa pongezi kiongozi huyo kwa uthubutu wake wa kusema ukweli na kukemea maovu mbalimbali ambayo yanaendelea nchini.

"Tunampongeza kwa kujitokeza katika kipindi hiki ambacho Watanzania na Viongozi wengi wa dini na kisiasa wamejazwa woga, wale waliokuwa mstari wa mbele kukemea maovu katika awamu zilizopita hivi sasa wamejitia upofu, ububu na uziwi.

Tunampongeza kuelezea Umuhimu na Ulazima kwa Watanzania kuungana pamoja kutetea uwepo wa mfumo wa Haki, Demokrasia na Utawala wa Sheria kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" alisema Mbarala Maharagande

Aidha Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF, Mbarala Mharagande amedai kuwa wao CUF wanatarajia viogozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, wasomi mbalimbali, waandishi wa Habari na wananchi kwa ujumla hawapaswi kukaa kimya bali wanapaswa kukemea mambo mabaya ambayo yanaendelea nchini, huku wakivitaka vyombo vya dola kutekeleza wajibu wao
.

Chanzo: EATV
 
Chama Cha Wananchi (CUF) kimetoa pongezi kwa Sheikh Ponda baada ya jana kuwataka Watanzania bila kujali itikadi zao na imani zao za dini kwa pamoja kushikamana kutetea na kulindwa kwa haki za binadamu, uhuru wa Kidemokrasia na utawala wa sheria.

Cuf.jpg

Sheikh Ponda alisema hayo jana baada ya kumtembelea Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu jijini Nairobi anakopatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi mnamo Septemba 7, 2017 mjini Dodoma.

Kufuatia kauli hiyo wa Sheikh Ponda Chama Cha Wananchi CUF kimempa pongezi kiongozi huyo kwa uthubutu wake wa kusema ukweli na kukemea maovu mbalimbali ambayo yanaendelea nchini.

"Tunampongeza kwa kujitokeza katika kipindi hiki ambacho Watanzania na Viongozi wengi wa dini na kisiasa wamejazwa woga, wale waliokuwa mstari wa mbele kukemea maovu katika awamu zilizopita hivi sasa wamejitia upofu, ububu na uziwi. Tunampongeza kuelezea Umuhimu na Ulazima kwa Watanzania kuungana pamoja kutetea uwepo wa mfumo wa Haki, Demokrasia na Utawala wa Sheria kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" alisema Mbarala Maharagande

Aidha Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF, Mbarala Mharagande amedai kuwa wao CUF wanatarajia viogozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, wasomi mbalimbali, waandishi wa Habari na wananchi kwa ujumla hawapaswi kukaa kimya bali wanapaswa kukemea mambo mabaya ambayo yanaendelea nchini, huku wakivitaka vyombo vya dola kutekeleza wajibu wao.

Na: Mbarala Maharagande
 
Huyu Mzee kipindi kile maaskofu wanauawa Zanzibar na makanisa kuchomwa ye si alikuwa akifurahia.??!!! Sasa leo nini kimemsukuma kukemea uovu au ndio msukumo wa donors wa kiarabu.

Wanataka kuona pesa yao inafanya kazi..maana ile fursa aliyokuwa anaitumia kipindi cha jk, jpm anaishughulikia kurudisha Mali za wakfu..na kamati iliyoundwa na mufti imeshaleta taarifa Tanzania nzima..sasa hana pa kutokea..na donors wanaweka hela alete amsha amsha..bahati yake alijificha..
 
Hao CUF na Ponda walipaswa kuwa gerezani kutumikia vifungo, visivyo na ukomo

Kwa vurugu zilizokuwa zikitokea chini, Zanzibar na Bara

Walizo sababisha kupitia mihadhara na mafundisho yao ya chuki.

Vurugu za udini na vurugu zilizo husiana na muungano.
 
Mjazeni ujinga tu......ila siku yakimfika atakuwa pekee yake
Hizi si zama za kuchekeana...Mponda amekuwa ni mtu wa kukutea HAKI za binadamu kweli au ni chuki zake kwa CCM???aache unafiki

Huyu anatumika na wapuuzi wachache kuleta choko choko na kutetea maslahi yake binafsi...SASA HAPA WAPINZANI NDIO MNATUMIA HII YA KUMTUMIA PONDA KAMA FULSA
msimdanganye......AVUE GWANDA LA KIONGOZI WA DINI AWE MWANASIASA
 
Mjazeni ujinga tu......ila siku yakimfika atakuwa pekee yake
Hizi si zama za kuchekeana...Mponda amekuwa ni mtu wa kukutea HAKI za binadamu kweli au??Huyu anatumika na wapuuzi wachache kuleta choko choko na kutetea maslahi yake binafsi...SASA HAPA WAPINZANI NDIO MNATUMIA HII YA KUMTUMIA PONDA KAMA FULSA
msimdanganye
Yamfike mara ngapi au umesahau
 
Mjazeni ujinga tu......ila siku yakimfika atakuwa pekee yake
Hizi si zama za kuchekeana...Mponda amekuwa ni mtu wa kukutea HAKI za binadamu kweli au ni chuki zake kwa CCM???aache unafiki

Huyu anatumika na wapuuzi wachache kuleta choko choko na kutetea maslahi yake binafsi...SASA HAPA WAPINZANI NDIO MNATUMIA HII YA KUMTUMIA PONDA KAMA FULSA
msimdanganye......AVUE GWANDA LA KIONGOZI WA DINI AWE MWANASIASA
humjui ponda,hana aogopacho..ukimtesa anajua thawabu zinajaa,ukimuua anaenda kutimua madhuvi ya dem wa peponi
 
Back
Top Bottom