Cuf - tunaipongeza chadema kwa kuunda serikali ya pamoja arusha. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Cuf - tunaipongeza chadema kwa kuunda serikali ya pamoja arusha.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtutuma, Jun 21, 2011.

 1. m

  mtutuma Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
  CUF – TUNAIPONGEZA CHADEMA KWA KUKUBALI KUUNDA SERIKALI YA PAMOJA – ARUSHA”
  Imetolewa na Mhe. Julius MtatiroNaibu Katibu Mkuu - Bara Juni 21, 2011 CUF – Chama Cha Wananchi tunakipongeza Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kuridhia kuunda serikali ya pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM) na Tanzania Labour Paty (TLP) Katika Manispaa ya Jiji la Arusha. Katika makubalino hayo CHADEMA Kimemtambua Mhe. Gaudance Lyimo (CCM) kuwa ndie Meya wa Jiji la Arusha, halikadhalika Mhe. Diwani Estomih Mala (CHADEMA) kuwa Naibu Meya kuanzia sasa hadi 2014, atakapomwachia nafasi hiyo Diwani wa TLP, Mhe. Michael Kihuyo. CUF inaamini kuwa Maridhiano haya yameonyesha kuwa CHADEMA sasa wanaelekea katika ukomavu wa kisiasa na kwamba siasa za uhasama, chuki, uchochezi na mauaji hazina tija kwa maendeleo ya Taifa letu. Lakini jambo muhimu zaidi ni kuwa CUF inasimamia kuwepo kwa serikali ya pamoja pale ambapo tutakabidhiwa dola, tutaunda serikali ya kumshirikisha kila mtanzania mwenye uwezo na kipaji cha kuongoza bila kujali jinsia yake, dini yake, kabila lake, uwezo wake wa kiuchumi alionao wala itikadi yake, hivi ndivyo manifesto yetu katika kila uchaguzi inasimamia na hivi ndivyo CUF inaamini.
  HAKI SAWA KWA WOTE
  Posted by;Mohammed Mtutuma,Msaidizi Maalum wa Naibu Katibu Mkuu,CUF – Tanzania Bara.
   
 2. Paulo

  Paulo JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Acheni unafiki na Uzandiki nyie C.U.F. Mnadhani kwa kupongeza umoja uliofanywa na vyama vitatu Arusha kutahalalisha serikali ya mseto mliyounda na CCM Zanzibar? Kama kweli manifesto (Ilani) yenu sii ya kisanii basi mngeweka kipengele kwenye hoja zenu wakati wa maridhiano kule Znz kwamba serikali ya kule iwe ya Kitaifa (ijumuishe vyama vyote vilivyoshiriki kwenye uchaguzi) na sio serikali ya mseto (kwa maana ya vyama viwili tu..CUF & CCM) kama mlivyofanya. Pili, kama taarifa yenu kwenye vyombo vya habari ililenga kupongeza CDM basi msingeambatanisha na mipango yenu ya chama katika taarifa hiyohiyo kama mlivyofanya. Hii inaonesha mmekosa media ya kutangaza sera zenu mkaona upenyo pekee ni kupitia CDM kwa mlango wa hila eti mnawapongeza. Shame on you C.U.F
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  unafiki ni dhambi mbaya sana.haya aliyoandika mtatiro ni unafiki mtupu.
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Tuwachunguze labda wameamua kubadilika!!
   
 5. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  CUF...BIG UP.....YOU LEAD THEY FOLLOW....!
  Mlionyesha njia...wao wanafuata
   
 6. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,093
  Likes Received: 505
  Trophy Points: 280
  Voice of the voiceless
   
 7. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Huu upuuzi wa kitu kinachoitwa muafaka mimi binafsi sikubaliani nao. Kibaya zaidi muafaka wa Arusha umeniacha na maswali mengi ambayo nilitegemea cuf kama chama wangezungumzia/wangeulizia!
  1. Nini wamekubaliana kuhusu Mary Chatanda ambaye ndiye chanzo cha mgogoro.
  2. Vp kuhusu kesi iliyoko mahakamani ambayo ilitokana na huo mgogoro.
  3. Ni kwann wamempa diwani wa TLP nafasi ya kuwa Naibu meya wakati yupo pekeyake kati ya madiwan wote wa kuchaguliwa.
  4. Sisi wananchi wanatufafanuliaje huo muafaka. Au ndio imeishia hivyo.
  Sisi kama watz tunatakiwa tukijikwaa kwenye jiwe, hatutakiwi kuliokota tu jiwe na kulitupa. Tunatakiwa kujua sababu hasa za kujikwaa ili siku nyingine tusijikwae hata kama jiwe lipo.
   
Loading...