CUF sasa yajikosha; kuwapokonya kadi za chama hicho madiwani na viongozi wote wakisaidia CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF sasa yajikosha; kuwapokonya kadi za chama hicho madiwani na viongozi wote wakisaidia CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 18, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  SIKU moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukituhumu Chama cha Wananchi (CUF) kuwa ni mamluki wa Chama Cha Mapinduzi wenye lengo la kukichafua na kujenga uhalali wa kuzuiliwa kwa maandamano ya chama hicho, chama hicho jana kimetoa kauli ya kujikosha mkoani hapa.
  Katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Makorola, CUF ilitangaza kuwavua uanachama kwa kuwapokonya kadi za chama hicho madiwani na viongozi wote vigeugeu watakaobainika wakikisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM) .
  Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Mipango na Chaguzi wa CUF Taifa, Shaweji Mketho, wakati kwa ajili ya maandalizi ya ziara ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Prof. Ibrahim Lipumba.
  Alisema kuwa kazi kubwa ya viongozi hao waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu mwaka 2010 ni kuhakikisha wanafanya kazi ya kuwatumikia wananchi pamoja na kukijenga chama hicho na si vinginevyo .
  Hivyo alisema ni lazima madiwani wa CUF kufanya kazi pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF) ili kuhakikisha kuwa Mkoa wa Tanga unapiga hatua katika maendeleo na wananchi wake wanaendelea kuunganishwa na viongozi hao badala ya kutenganishwa kwa ubinafsi wa baadhi ya viongozi.
  “...Napenda kuwaasa wote ambao wamekuwa viongozi kupitia CUF kuwa kazi kubwa ni kufanya kazi waliyopewa na wananchi katika kuhakikisha wanawaletea maendeleo si vinginevyo ...Chama hakitakuwa tayari kuwavumilia wale wote ambao watabainika kwenda kinyume na matakwa ya wananchi pamoja na chama .....lazima ikibainika kiongozi awaye yeyote anakwenda kinyume hatutasita kumpokonya kadi yetu na kumvua uanachama,” alisema.
  Kwa upande wake Mbunge wa Mwindau alisema katika kuufanya Mkoa wa Tanga kuwa ni mkoa wa kimapinduzi ya siasa na wananchi wake kuwa wamoja lazima viongozi wa CUF kuacha kuendelea na kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010 kwa kipindi hiki na badala yake wanapaswa kutambua kuwa uchaguzi umemalizika na sasa ni wakati wa kufanya kazi kwa pamoja pasipo kuwatenga wana CCM ama wana CHADEMA na vyama vingine. Mwindau alisema kuwa viongozi wa vyama vyote kwa sasa wanatakiwa kushirikiana na wananchi katika kukuza maendeleo badala ya kuendelea kuwatenga wananchi kwa itikadi za kisiasa. Hata hivyo katika hatua nyingine mbunge huyo alishangazwa na hatua ya wana CCM kutofika katika mikutano ya hadhara ya CUF, mikutano ambayo inaitishwa kwa ajili ya kuibua miradi ya kimaendeleo katika maeneo yao.
   
Loading...