CUF sasa yairarua CHADEMA Igunga; Hamad Rashid Mohamed asema CHADEMA sio chama cha kitaifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF sasa yairarua CHADEMA Igunga; Hamad Rashid Mohamed asema CHADEMA sio chama cha kitaifa

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by nngu007, Sep 30, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Majira News


  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Mbunge wa Lindi kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Bw. Salum Baruani akihutubia wananchi wa Kijiji cha Ngwamashimba wilayani Igunga wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa chama hicho, Bw. Leopold Mahona jana.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  *Yadai haijakomaa kisiasa, si cha kitaifa

  Na Peter Mwenda, Igunga

  CHAMA cha Wananchi (CUF) kimewataka wananchi wa Igunga kutokipigia kura Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kuwa si chama cha kitaifa na hakijakomaa kisiasa.

  Hayo yalisemwa na Mbunge wa Wawi, Bw. Hamad Rashid Mohamed, wakati akimnadi mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo, Bw. Leopold Mahona katika viwanja vya Barafu mjini hapa.

  Mbunge aliwahi kuwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni kabla ya Bw. Freeman Mbowe wa CHADEMA kuchukua nafasi hiyo, alidai kuwa chama hicho hakijakomaa kisiasa ndiyo maana kinajihusisha na vitendo vya vurugu ikiwemo kumwaga tindikali, kupiga risasi na mengine na kwamba hiyo inaonesha hakiwezi kuleta maendeleo ya wananchi.

  Alisema chama hicho kina ubinafsi, ndiyo maana kilijitenga bungeni na kuunda umoja wa wabunge wa CHADEMA peke yao tofauti na wakati alipokuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ambapo alishirikisha wabunge wa vyama vyote vya upinzani wakiwemo wa chama hicho bila ubaguzi.

  Alidai sera za CHADEMA hazina tofauti za CCM ambao wanagawa madaraka kwa watoto wao, ndugu na jamaa badala ya kufuata utaratibu wa uongozi katika jamii.

  Bw. Rashid aliyewasili mjini hapa juzi na helkopta ya CUF kujumuika na wabunge wengine wa chama hicho hivyo kufanya idaid yao kufikia 20, alisema chama chake ni cha kitaifa ambacho kina viongozi pande zote za muungano.

  “Makamu wa Rais Zanzibar ni Katibu Mkuu wa CUF, sisi wabunge wa Zanzibar tumekuja kwa gharama zetu kumsaidia mwenzetu aingie bungeni kuwakomboa watu wa Igunga, niambieni CHADEMA kuna kiongoi gani Zanzibar,” alihoji Bw. Rashid.

  Alisema wananchi wa Igunga wakitaka maendeleo ya kweli wamchague, Bw. Mahona kuwa mbunge kwa kuwa wana kila sababu ya kufanya hivyo ili kubadilisha maisha yao.

  Naye Meneja Kampeni wa mgombea wa CUF, Bw. Antony Kayange, alisema wapiga kura wasipoteze muda kukipigia kura CCM kuwa wanakumbuka kumleta Waziri wa Ujenzi, Bw. John Magufuli kuwaongopea.

  Alisema anawadaganya kujenga daraja la mto Mbutu ambalo limeahidiwa kujengwa miaka mingi iliyopita bila ahadi hiyo kutimizwa.

  “Huyu Magufuli amekuwa madarakani kwa miaka 11 mbona hata siku moja hakufikiria kuja Igunga angalau kuona kero za wananchi, leo anakuja kudanganya kujenga daraja la Mbutu huo ni uongo, msikubali kurubuniwa kupigia kura CCM,” alisema Bw. Kayange.

  Naye Naibu Katibu wa CUF Tanzania Visiwani, Bw. Ismail Jussa, alisema wananchi wa Igunga wasikubali kudanganywa na vyama vingine kwa kuwa wataendelea kukabiliana na matatizo waliyonayo bila kupata ufumbuzi.

  Alisema katika majimbo ambayo CUF inaongoza yana maendeleo makubwa kutokana na kuwa na uwezo mkubwa kujenga hoja za wananchi na kuziwasilisha serikalini kufanyiwa kazi.

  Mgombea ubunge Bw. Mahona akiomba kura kwa wananchi alisema kamwe hatakimbia jimbo lake kama wanavyofanya wabunge wengine bali atatumia muda wake mwingi kuwatumikia wananchi wa Igunga.


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  CHADEMA waliweka wabunge Zanzibar lakini hawakuchaguliwa ndio sababu hiyo CHADEMA sio chama kitaifa?

  Kwahiyo CUF kimekuwa chama cha kitaifa 2010 baada ya kupata mbunge Lindi?

  Hawajui kuwa Chadema wana wabunge 3 wa kuteuliwa toka Zanzibar na Pemba? si Utaifa huo?
   
 3. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huyo hamadi bila kuitaja chadema hawezi kujenga hoja kwani anajua kwa kuitaja chadema ndio anapata attention.
  Naona marupurupu ya kiongozi wa upinzani bado yanamtoa roho.
  Mwenziye Mbowe hana shida na hayo marupurupu ndio maana hata shangingi alilirudisha.
  Poor hamadi, anazidi kwisha.
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kumjadili Hamad ni sawa na kutaka tuanze kumjadili Nape hapa .Hamad is dead walking mind alidhani CUF na udini inaweza lolote .Hawa ni wa kupuuza .Waache waige kupanda helikopta then wapotee .
   
 5. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mimi ninachoona ni vyama kukosoana bila ya kuwaeleza wananchi mipango ya maendeleo.
  Kukosoa na kulaumu ni rahisi, kwani hutumii nguvu (pengine hata akili) kwa kukosoa bali bla bla bla!
  Nasikitika kuwa vyama vimepoteza muda bure kukosoana, kukashifiana na kupigana badala ya kushughulikia maendeleo.
  Pamoja na yote, nina hakika wana Igunga wana akili za kutosha kumjua nani mbaya wao. Ninachowaomba watumie haki yao ya kura kupata haki yao ya maendeleo.
   
 6. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mfa maji siku zote haishi kutapatapa, hana cha kuwaambia wananchi kuhusu chama chake na jinsi gani kitainua maisha ya walala hoi Igunga? Poor him.
   
 7. p

  politiki JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  CUF inahubiri ukanda na uzanzibari wakati CCM ikihubiri UDINI kuwatenganisha watu kulingana na dini zao wakati chadema wakizungumzia sera na jinsi watakavyowasaidia wananchi katika matatizo yao waliyonayo kama alivyosema ZITTO kuwaondolea kero nyingi ikiwemo kupiga marufuku michango isiyo na manufaa kama walivyofanya singida mashariki kwa Tundu mwana wa Lisu.
   
 8. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hamadi Rashid ni mwehu,wao wamefunga ndoa na ccm,hivyo alitaka cdm nao waingie kwenye hiyo ndoa?Hamadi utaifa unao usema hapo hauelewe. Kwani cdm si wanao wabunge wa kuteuliwa toka nzn? We unataka nini haswa?Fisi maji mkubwa we.mlafi mkubwa sana wa madaraka wewe,toka wakunyime uongozi wa kambi rasmi unachuki sana we kizee cha kale,kula jeuri yako.
   
 9. samito

  samito JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 621
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  CUF maji ya shingo... wanasindikiza tu uchaguzi na wakati kila mtu anajua hawawezi kuchukua... wanapoteza ela za bure tu bora wangeenda kufanya maendeleo huko waliko chaguliwa.. mpambano igunga ni kati ya CCM na CHADEMA.. na CDM ndio kinachopewa nafasi ya juu kuliko vyote
   
 10. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  CUF ni chama cha kidini,ukimuondoa mtatiro ambaye naye naona siku hizi ana SIJIDA,kuna kiongozi gani mwingine ambaye sio muislamu,CUF hawana hata mbunge mmoja wa dini ya kikristu,ni chama cha waarabu.
   
 11. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #11
  Sep 30, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 586
  Trophy Points: 280
  punguza ukali mkuu! anatafuta umaarufu, teh teh teh teh!
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Ndio siasa zetu za Tanzania, mwenzako akimwaga ugali wewe unamwaga mboga!
   
 13. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  hamadi rashid atia huruma, maalim seif naye du! wapemba wenzie wamezama melini kizembe yeye anakata whisky ikulu zenji, hajaongeza uwajibikaji serikali hata chembe!
   
 14. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Maji na mafuta daima ujitenga!jamaa wa CCM B wa pumba hawajambo!
   
 15. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  CUF =CCM siwezi kushangaa wakiungana kuishambulia chadema, sasa huyu naye amekuja kumnadi mgombea au amekuja kuiponda CHADEMA?Hizi ni siasa za kitoto kabisa acheni kulopoka upuuzi, mwageni sera zenye tija kwa wananchi,ongeleeni maendeleo mtawafanyia nini wananchi,ACHENI UJINGA.
   
 16. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wewe wacha uongo waislamu hawanywagi Whisky!!
   
 17. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  hivi zanzbar inawasaidia nini wana igunga.
   
 18. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #18
  Sep 30, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Kwani uongo?Nape alitamka kwa kinywa chake akiwa Mbeya na akina Sita.
   
 19. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #19
  Sep 30, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  uvivu.
   
 20. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #20
  Sep 30, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Huyo anaendelea kuziota posho alizokuwa akipata alipokuwa KUB, ndio maana haishi kumtaja mbowe.

  Hata hivyo cuf kujaribu kupambana na chadema badala ya ccm si habari tena kwa kuwa wao ni wanandoa lazima wapigane tafu.
   
Loading...