CUF sasa watimuana... Lipumba ateua wakurugenzi wapya

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,547
2,000
na Bakari Kimwanga

MAKOVU ya Uchaguzi Mkuu uliopita bado yanakitesa Chama cha Wananchi (CUF), hali iliyokilazimu kikao chake cha Baraza Kuu la Uongozi kuwatema baadhi ya viongozi wa idara mbalimbali.

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho kichofanyika jijini Dar es Salaa kati ya Desemba 10 hadi 11, zinadai mara baada ya kujadili tathmini ya uchaguzi na kugundua mapungufu mbalimbali, Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba, kwa kushauriana na Katibu Mkuu wake, Maalimu Seif Sharif Hamad, walilazimika kufanya madiliko ya wakuu hao wa idara.

Chanzo hicho cha habari kilieleza moja ya agenda ni ile ya kuangalia mahusiano ya nje pamoja na vyombo vya habari na kugundua kukosekana kwa ufanisi wa kutosha miongoni mwa wakurugenzi wa chama hicho.

Katika mabadiliko yanayodaiwa kufanywa ni pamoja na nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu wa chama hicho kwa pande zote mbili kwa Tanzania Bara na Visiwani.

Madiliko hayo mbali na kuzikumba nafasi hizo pia yamefanyika kwa wakurugenzi na hata kufikia hatua ya kuziunganisha idara hizo, ili kuleta ufanisi na uwajibikaji kwa dhati mbele ya wanachama.

Wakurugenzi waliopoteza nafasi zao ni Mbarara Maharagande (aliyekuwa Mkurugenzi wa Siasa), Ashura Mustapha (Habari na Uenezi) na Mazee Rajab Mazee (Naibu Mkurugenzi wa Blue Guard).

Wengine ni Dk. Juma Muchi (Naibu Mkurugenzi Siasa) na Salim Masoud (Blue Guard).

Chanzo hicho kilihabarisha kuwa nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu wa Tanzania Bara iliyokuwa ikishikiliwa na Jaram Bashange sasa itaongozwa na Julius Mtatiro, ambaye ameongezewa jukumu la kurugenzi ya utawala, Ulinzi na Maadili, ambapo awali alikuwa Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria wa chama hicho.

Kwa upande wa nafasi ya Naibu Katibu Kkuu wa Zanzibar nafasi hiyo awali ilikuwa ikishikiliwa na Juma Duni Haji, aliyepata uteuzi na kuwa Waziri wa afya wa Zanzibar, sasa ameteuliwa Mwakilishi wa Mji Mkongwe Ismail Jusa Ladhu, kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Wengine walioteuliwa na nafasi zao kwenye mabano ni Salim Hemed ( Mkurugenzi wa Maandalizi ya Uchaguzi na Oganaizesheni) huku Naibu wake Shaweji Mketo, Salim Mandari (Fedha Mipango na Uchumi) Naibu Zakia Omari na Salim Bimani (Habari Uenezi, Haki za Binadamu na Sheria) huku Naibu wake Amina Ndovu, kutoka mkoani Tanga.

“Unajua ni lazima viongozi hao walikuwa wafanye mabadiliko maana hata uchaguzi uliopita haukuwa na ufanisi wa hali ya juu na hata kuna baadhi ya waliopewa majukumu lakini hawakuweza kufanya vizuri na matokeo yake chama kufanya vibaya,” alisema mtoa habari huyo.

Pamoja na hatua hiyo, kikao hicho kilipitisha jina la Mbunge wa Mtoni Zanzibar Faki Haji Makame kuwa Msaidizi wa Katibu Mkuu kutokana na ombi lililotolewa na Maalim Seif kuomba atafutiwe msaidizi wa kufanya majukumu yake ya Ukatibu Mkuu wa chama baada ya kuteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais.

Habari zaidi zinadai kuwa CUF, ilipanga kuanzisha redio na televisheni yake kabla ya Uchaguzi Mkuu uliopita wa mwaka 2010 lakini wakajikuta wakikwama kutokana na waliopewa kusimamia majukumu hayo kushindwa kuleta ufanisi na tija na hata kufikia kufanya vibaya katika Uchaguzi Mkuu.

Tanzania Daima, ilipomtafuta Naibu Mkurugenzi wa Habari, Mahusiano na Umma, Ashura Mustapha, ili kuthibitisha madai hayo simu yake haikupatika muda wote wala ofisini kwake.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya CUF leo Profesa Lipumba anatarajiwa kuitisha mkutano na waandishi wa habari ili kuzungumzia mabadiliko hayo.
 
PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,124
2,000
hiki chama kinaelekea kaburini tu, washapigwa bao na CCM wakae wakila kachori, bajia na kahawa pale mji mkongwe hawana jipya.
 
NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,668
0

:target::target:
A%20S%20clock.gif
:painkiller:
 
kagumyamuheto

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
286
0
Cuf ni miongoni mwa vyama visivyokuwa na migogoro ya mara kwa mara nchini tanzania. Hii ni kutokana na kuwa na viongozi imara na wenye upeo wa hali ya juu.
 
ngoko

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
573
0
Cuf ni miongoni mwa vyama visivyokuwa na migogoro ya mara kwa mara nchini tanzania. Hii ni kutokana na kuwa na viongozi imara na wenye upeo wa hali ya juu.
Kweli kabisa , baada ya kumng'oa Mapalala kimekuwa na uongozi wenye upeo wa hali ya juu
 
Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
0
Hivi ndani ya Cuf kuna kiti kimoja tu cha uongozi, kwa mtu hasiyekuwa mfuasi wa dini ya islamu. nacho ni naibu katibu mkuu bara!
 
mbongopopo

JF-Expert Member
Jan 24, 2008
1,614
2,000
watajiju mie walimdisi jamaa yangu wa mbali basi wakae naa hiyo cuf yao...sasa sie chadema. mmh ila mie sina time na chama chochote moyoni mwangu
 
HIMO ONE

Senior Member
Sep 6, 2010
128
0
na bakari kimwanga

makovu ya uchaguzi mkuu uliopita bado yanakitesa chama cha wananchi (cuf), hali iliyokilazimu kikao chake cha baraza kuu la uongozi kuwatema baadhi ya viongozi wa idara mbalimbali.

taarifa kutoka ndani ya kikao hicho kichofanyika jijini dar es salaa kati ya desemba 10 hadi 11, zinadai mara baada ya kujadili tathmini ya uchaguzi na kugundua mapungufu mbalimbali, mwenyekiti wa cuf taifa, profesa ibrahimu lipumba, kwa kushauriana na katibu mkuu wake, maalimu seif sharif hamad, walilazimika kufanya madiliko ya wakuu hao wa idara.

chanzo hicho cha habari kilieleza moja ya agenda ni ile ya kuangalia mahusiano ya nje pamoja na vyombo vya habari na kugundua kukosekana kwa ufanisi wa kutosha miongoni mwa wakurugenzi wa chama hicho.

katika mabadiliko yanayodaiwa kufanywa ni pamoja na nafasi ya unaibu katibu mkuu wa chama hicho kwa pande zote mbili kwa tanzania bara na visiwani.

madiliko hayo mbali na kuzikumba nafasi hizo pia yamefanyika kwa wakurugenzi na hata kufikia hatua ya kuziunganisha idara hizo, ili kuleta ufanisi na uwajibikaji kwa dhati mbele ya wanachama.

wakurugenzi waliopoteza nafasi zao ni mbarara maharagande (aliyekuwa mkurugenzi wa siasa), ashura mustapha (habari na uenezi) na mazee rajab mazee (naibu mkurugenzi wa blue guard).

wengine ni dk. Juma muchi (naibu mkurugenzi siasa) na salim masoud (blue guard).

chanzo hicho kilihabarisha kuwa nafasi ya unaibu katibu mkuu wa tanzania bara iliyokuwa ikishikiliwa na jaram bashange sasa itaongozwa na julius mtatiro, ambaye ameongezewa jukumu la kurugenzi ya utawala, ulinzi na maadili, ambapo awali alikuwa mkurugenzi wa haki za binadamu na sheria wa chama hicho.

kwa upande wa nafasi ya naibu katibu kkuu wa zanzibar nafasi hiyo awali ilikuwa ikishikiliwa na juma duni haji, aliyepata uteuzi na kuwa waziri wa afya wa zanzibar, sasa ameteuliwa mwakilishi wa mji mkongwe ismail jusa ladhu, kuwa naibu katibu mkuu zanzibar.

wengine walioteuliwa na nafasi zao kwenye mabano ni salim hemed ( mkurugenzi wa maandalizi ya uchaguzi na oganaizesheni) huku naibu wake shaweji mketo, salim mandari (fedha mipango na uchumi) naibu zakia omari na salim bimani (habari uenezi, haki za binadamu na sheria) huku naibu wake amina ndovu, kutoka mkoani tanga.

"unajua ni lazima viongozi hao walikuwa wafanye mabadiliko maana hata uchaguzi uliopita haukuwa na ufanisi wa hali ya juu na hata kuna baadhi ya waliopewa majukumu lakini hawakuweza kufanya vizuri na matokeo yake chama kufanya vibaya," alisema mtoa habari huyo.

pamoja na hatua hiyo, kikao hicho kilipitisha jina la mbunge wa mtoni zanzibar faki haji makame kuwa msaidizi wa katibu mkuu kutokana na ombi lililotolewa na maalim seif kuomba atafutiwe msaidizi wa kufanya majukumu yake ya ukatibu mkuu wa chama baada ya kuteuliwa kuwa makamu wa kwanza wa rais.

habari zaidi zinadai kuwa cuf, ilipanga kuanzisha redio na televisheni yake kabla ya uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2010 lakini wakajikuta wakikwama kutokana na waliopewa kusimamia majukumu hayo kushindwa kuleta ufanisi na tija na hata kufikia kufanya vibaya katika uchaguzi mkuu.

tanzania daima, ilipomtafuta naibu mkurugenzi wa habari, mahusiano na umma, ashura mustapha, ili kuthibitisha madai hayo simu yake haikupatika muda wote wala ofisini kwake.

kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya cuf leo profesa lipumba anatarajiwa kuitisha mkutano na waandishi wa habari ili kuzungumzia mabadiliko hayo.

ccm b
 
Amalinze

JF-Expert Member
May 6, 2012
6,719
2,000
La Profeseli amewatengua wakurugenzi wote akiwamo Jussa na kuteua wapya.

source Azam TV.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom