Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,172
UCHAGUZI mkuu uliomalizika mwishoni mwa mwezi wa kumi ulikuwa wa upande mmoja, badala ya ushindani kama ilivyodhaniwa, watawala walitumia mamlaka zake kuibeba CCM ishinde Hili ni tamko la Chama cha Wananchi (CUF) baada ya kufanya tathmini ya uchaguzi mkuu uliomalizika mwishoni mwa mwezi Oktoba katika kikao chake cha baraza kuu la Uongozi
CUF imesema baada ya tahthimini yake, imeona na kuridhika kuwa mazingira ya uchaguzi hayakuwa shirikishi na kwamba vyama vya upinzani vilivyoshiriki uchaguzi, vilifanya hivyo kwa hofu ya kumsusia nguruwe shamba na sio kushinda.
Kufuatia madhaifu na mapungufu mbalimbali yaliyopo chama hicho kimesema bila mabadiliko ya katiba na kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi, vyama vya upinzani haviwezi kuishinda CCM na vikiendelea kushiriki katika uchaguzi vitakuwa wasindikizaji.
Akitoa tathmini hiyo kwa gazeti hili Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Julius Mtatiro aliyekuwa akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wake Profesa Ibrahim Lipumba, anasema Tumeamua kwa dhati kusimama kidete kudai katiba mpya, pamoja na tume huru ya uchaguzi ili tutakaposhiriki uchaguzi mwingine wowote tuweze kushiriki katika mazingira huru yasiyo na upendeleo kwa chama chochote
Anasema kupatikana kwa katiba mpya kutawezesha kuwa na Tume huru ya Uchaguzi na ambayo itatoa fursa kwa vyama vyote kutoa maoni yao hasa wakati wa uchaguzi, maoni anayosema yatasaidia kuondoa kasoro mbalimbali zinazolalamikiwa na vyama vinavyoshiri katika uchaguzi.
Miongoni mwa kasoro zinazolalamikiwa na ambazo CUF imeziainisha ni uwepo wa wasimamizi wote wa uchaguzi, tangu mwenyekiti wa NEC mpaka wasimamizi wa majimbo na kata kuteuliwa na rais ambaye wakati huo huo yeye (rais) na chama chake wanashiriki katika uchaguzi huo.
Anasema kwa vyovyote vile wasimamizi hao hawawezi kwenda kinyume na maagizo watakayopewa mwajiri wao ambaye ni kwa wakati huo anakuwa mshiriki au mgombea na kwamba kwa mazingira hayo uchaguzi hauwezi kuwa huru na vyama vya upinzani haviwezi kuishishinda CCM.
Kauli yao kuhusu matokeo
Anasema mbali na kasoro hizo, tathmini waliyofanya wameridhika pia kuwa kulikuwa na mapungufu makubwa katika suala zima la kufanya majumuisho ya kura za wagombea wake ambapo anasema kura za mgombea urais wake profesa Ibrahim Lipumba ziliibwa na wagombea wake wa ubunge katika majimbo 12 kunyanganywa ushindi wao makusudi.
Kwa idadi ya kura kutoka kwa mawaka wetu, mgombea wa nafasi ya urais kupitia CUF Profesa Ibrahim Lipumba alipata idadi kubwa ya kura kuliko ile iliyotangazwa na mwenyekiti wa uchaguzi. Tulishtuka kusikia wakitangaza eti, Profesa alipata kura laki sita, sio kweli, Profesa alipata kura nyingi, lakini uchakachuaji ule wote uliwezekana kutokana na mapungufu makubwa yaliyopo kutokana na muundo wa Tume ya Tume ya Uchaguzi ambayo imekuwa kiranja wa ukandamizaji anasema Mtatiro.
Anayataja majimbo ya Tandahimba, Mafia, Sumve, Newala, Masasi, Tunduru, Temeke, Tanga Mjini, Lindi, Mchinga, Kondoa Kaskazini na Mtwara Mjini kuwa ni majimbo ambayo wagombea wake waliishinda CCM mpaka dakika ya mwisho lakini hali ilibadilika pale wasimamizi walipokuwa wakitangaza matokeo ambapo anasema, CUF ilishangaa ikitangazwa kushindwa badala ya kushinda.
Matatizo ndio yale yale, msimamizi anamtangaza mtu waliyeelekezwa kumtangaza, sio mshindi, hii ni hatari na ili kumaliza matatizo ya namna hii, na ili kuondoa malalamiko kila unapomalizika uchaguzi wowote, serikali ikubali kufanya mabadiliko ya katika, sambamba na kuruhusu kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi.
Mtatiro anasema, CUF imeona kuwa Uchaguzi Mkuu uliokwisha, ulitawaliwa na vitisho vya kila aina kwa washiriki wa uchaguzi, viongozi wa vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mbalimbali na anatoa mfano wa wenyeviti wake wawili wa wilaya za Rorya na Meatu ambao walikamatwa wakati wa uchaguzi na mpaka sasa wanashikiliwa na polisi huku wakiwa hawajafunguliwa kesi.
Anasema kauli iliyotolewa na mkuu wa majeshi kupitia mnadhimu wake mkuu Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo ya kuvitaka vyama vya siasa kukubali matokeo baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba na kuonya kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vimejiandaa kikamilifu kupambana na yeyote atakayejaribu kuyakataa matokeo ililenga kuwatisha wananchi na vyama vilivyokuwa vikishiriki uchaguzi.
Anasema, hakukuwa na sababu kwa jeshi la wananchi ambalo linayo majukumu ya kulinda nchi na mipaka yake kutoa kauli zile alizoziita za vitisho na kusema Mkuu wa jeshi anaposema amejiandaa kikamilifu kupambana na mtu, watu, kikundi, chama au taasisi yoyote itakayokwenda kinyume na sheria, unategemea nani ataenda kupiga kura, kwa vyovyote ushiriki lazima utakuwa mdogo kutokana na hofu, na ndivyo ilivyokuwa, umeona idadi ya waliojitokeza kupiga kura imekuwa ndogo kulinganisha na ile ambayo walijiandikisha lakini hawakujitokeza.
Maazimio ya CUF
CUF imeazimia kwa kauli moja. ili kukabiliana na mapungufu yaliyojitokeza na ambayo yanaweza kujitokeza katika chaguzi zinazokuja, tuje na kauli mbiu, kwamba tunaanza mapambano ya kudai katiba mpya sasa.
Tunataka na tunahitaji katiba mpya, tunataka tume huru ya uchaguzi ili tuingie kwenye uchaguzi katika mazingira huru na yenye ushindani ulio sawa kwa kila mshiriki na sio mazingira kandamizi yanayopendelea upande mmoja kama ilivyo sasa anasema Mtatiro.
Anasema CUF inaanza kampeni hiyo ya kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi sasa na kusisitiza kwamba, imani yake ni kufanya kile walichofanya Zanzibar ambapo kwa shinikizo la chama hicho wamefanikiwa kufanya mabadiliko ya katiba na kuwezesha kuunda serikali ya umoja wa Kitaifa iliyokishirikisha chama hicho katika kuunda serikali hali anayosema imeiwezesha Zanzibar kufanya uchaguzi wa amani baada ya kuwa na migogoro na kukosekana kwa amani kwa zaidi ya miaka 15 iliyopita