Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 229
CUF kujifuta, kutangaza kujiunga na CCM
Kuna tetesi kwamba mazungumzo ya sisri baina ya CUF na CCM yamekuwa yakifanyika ili kuungana kwa vyama hivyo.
Muafaka umeshafikiwa na kinachongojewa ni kwa JK kutangaza Baraza lake la Mawaziri ambalo litajumuisha baadhi ya viongozi wa CUF ili kukamilisha, kwa huku Bara, kile kilichoitwa maridhiano kule Visiwani.
Suala hili ndilo limemchelewesha JK kutangaza Baraza la Mawaziri.
Changamoto nyingine iliyozuka ni kupata jina jipya la chama hicho kipya, na hili limewekwa siri hadi siku ya kutangaza.
Mnaokumbuka mwaka 1977 TANU ilipoungana na ASP jina la CCM halikutangazwa hadi siku ya kuzinduzi wa chama kipya – tarehe 5 Februari 1977.
Hili bifu lote la Bungeni kati ya CUF na Chadema, hususan kwa Chadema kushikilia msimamo wake ndiyo limechochea mazungumzo ya kuungana kwa CUF na CCM kwenda haraka.
Habari zinasema iwapo Chadema wangekubali masharti ya CUF na hivyo viongozi wa CUF kuingia ndani ya Kambi ya Upinzani bungeni, basi kuungana kwa vyama hivyo kungesitishwa kwa sababu CCM tayari wangekuwa wamepenyeza ‘watu' wao (yaani viongozi wa CUF) ndani ya Chadema na hivyo kuwawezesha kujua siri na mikakati yote dhidi ya chama tawala.
Nawasilisha.