eliesikia
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 787
- 758
Madai ya KATIBA mpya na TUME HURU ni madai ya upinzani wote.. Lakini wengine wameshachoka ndio maana CUF, NCCR wameamua kuwaachia CHADEMA ambao wamepata bahati ya kuwa wengi bungeni na sasa harakati na matunda ya CHADEMA yataonekana kuinufaisha kambi nzima ya upinzani na wananchi.. Pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu ambao wote wanadai hili.....
Kutoka bungeni ni sahihi katika siasa??? Njia hii ni ya kiungwana au maandamano ndio uungwana????
1. Rejea kule CUBA wabunge walishawahi kutoka wakati Fidel Castro anaongea kwa minajili ya kutokubaliana nae na utawala wake wa kijeshi...
2. Marekani walishwahi kutoka nje kwenye mkutano baada ya kiongozi wa Iran kuanza kuongea kwa minajiri ya kutokubaliana nae
3. Iran waliwahi kutoka nje kwa minajiri ya kukataa Marekani kuingilia nchi za kiislamu
4. Rejea nchi mbalimbali na nyingine juzijuzi tuuu wametoka nje kuonyesha kutokukubaliana, India, Malaysia(mwaka 2008 kuhusu DNA bill ), Pakistan, Japan, South Africa(Zuma insult), Zambia(Electroral bill), Kuwait, Gambia, iraqi(residaa reelect), Sri Lanka na nchi nyingine nyingi...
TAFAKURI:
Kama wewe ni mtu wa kawaida na una uelewa mkubwa wa siasa kutoka nje ni siasa pia kwa kuwa unaonyesha jinsi gani unataka meza ya maelewano iharikishwe... Mimi nakwambia hivi kama CUF wasingekuwa watawala Zanzibar wao ndio wangeongoza msafara.. Kwa kuwa madai ya tume isiyo huru hata wao Pamoja na Lipumba wamekuwa wakilalamikia toka 1995...
Hata hao NCCR nao waliwahi kufungua kesi mahakamani kudai tume huru ya uchaguzi... Kusema kweli sio jambo la kushangaza kabisa...
Kilichotokea pale ni lazima kila mtu na jamii ya kimataifa itamshauri Jk kuingia meza ya makubaliano ili uchaguzi ujao uwe huru na wa haki.. JK asiteue tena refa wa uchaguzi kama tulivyozoea...
CUF, NCCR, TLP, UDP kama wanaongea siasa bila vitendo ni ajabu sana... Wakati mwingine ni lazima uonyeshe uhitaji wa hali ya juu wa kile unachokitaka na si vinginevyo...
Kuna watu wanadai njia iliyotumika si sahihi??? Waniambie wanayoona ni sahihi ni ipi!!! Kama una hoja mbadala toa si kupondea ya mwenzako.. Mimi naona hapa kuna umbwe kubwa la fikra na ukungu mkubwa wa kufikiri... Watu wengi kwa sababu ya ushabiki tunakuwa masikini wa mawazo mbadala.. Kama CHADEMA wamekosea nieleze njia gani ni bora toka 1990 ilipoanza mikakati ya katiba mpya pale Karimjee nadhani ambapo National committee for Constitutional Reform(NCCR) iliundwa..
Tuachie mawazo mbadala na harakati zitendeke.. CHADEMA walituma watu wa IT kuchunguza mtambo wa NEC siku hiyohiyo ukagoma mbele yao.. NEC ikawaihidi watawa feedback ukitengenezwa.. Cha ajabu walipata barua ya tar 28 okt ikafika 8 novemba.. Kwa nini NEC walifanya hivi??Jibu mwenyewe.
Mimi naomba CCM na JK wachukulie haya kwa mustakabali wa nchi yetu.. Kikwete kama atakubali Constitution Reform basi atakumbukwa zaidi kuliko watangulizi wake.. Na mataifa ya nje yatampongea kama mwenzie Mwai Kibaki.. Asiangalie kama CCM itaanguka au laaah... Kwa kuwa ameahidi vitu na anao uwezo wa kutekeleza basi CCM itabaki lakini vinginevyo lazima wataanguka... Wasiogope kwa minajili hiyo lakini watende haki... Siku zote haki humweka mtu huru!!!
Nawasilisha
Eliesikia