CUF: Nassor Ahmed Mazrui Naye Atakiwa Kijisalimisha Polisi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Jeshi la Polisi limeendelea na kamatakamata ya wapinzani wa vyama vinavyounda Ukawa katika maeneo mbalimbali likieleza sababu tofauti za kijinai zinazohusishwa na masuala ya kisiasa.

Mpaka sasa wabunge wa upinzani waliokamatwa ni; Halima Mdee (Kawe), Mwita Waitara (Ukonga) na Peter Lijualikali (Kilombero), wote wa Chadema na baadhi ya madiwani wa chama hicho katika Jiji la Dar es Salaam.

Vilevile, imeelezwa kuwa Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea alikuwa anatafutwa kuunguanishwa na wenzake.

Pia, baadhi ya wanasiasa wa CUF Zanzibar wamekamatwa na kuhojiwa kwa madai ya kuwatusi viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Viongozi wa CUF waliohojiwa na polisi mpaka sasa ni Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Omar Ali Shehe na Kiongozi wa Mkakati wa Ushindi, Mohamed Sultan Mugheir ‘Eddy Riyami’ ambaye yuko nje kwa dhamana.

Mbali na viongozi hao, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui jana amepatiwa barua ya wito na Polisi Zanzibar ikielezwa kuna mambo yanamhusu.

Hii ni mara ya pili kwa Mazrui kuitwa polisi tangu kufutwa kwa uchaguzi wa Oktoba 25, huku CUF ikidai kuwa huo ni mwendelezo wa mkakati maalumu dhidi ya viongozi wa chama hicho.
 
Attachments

  • 3.jpg
    3.jpg
    12.6 KB · Views: 28
Hii nchi hii...uvumilivu una ukomo wake tu....

tena ogopa sana watu wakimya
 
ni kama uganda tu et tanzania kuna amani ccm inaichafua inchi muda si mrefu
 
Majambazi wanaendelea kufanya kazi yao kwa kuwa polisi wamepewa kazi ya kudhibiti upinzani, ccm ni janga kuliko njaa.
 
Back
Top Bottom