CUF, na TLP vyama dhaifu na ninyi mnataka kuonana na Kikwete? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF, na TLP vyama dhaifu na ninyi mnataka kuonana na Kikwete?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kabindi, Nov 24, 2011.

 1. k

  kabindi JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 334
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kAMATI KUU YA CCM Imemshahuri Rais kukutana na vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni badala ya CDM kama walivyokuwa wamenuia! najiuliza mengi, hivi na hawa CUF na TLP nao wana hoja ya mapungufu katika Muswaada uliopitishwa Bungeni?! sidhani hivyo maana nahisi kama wawakilishi wa vyama hivyo ni kama wachumia tumbo maana matharani CUF baada ya kuingia kwenye muafaka kule Zanzibar wameendelea kuporomoka na kwa sasa mwenendo wao unatishia uhai wa chama chao! kwa sasa ni chama dhaifu mno! na huyo mrema naye ni aibu tupu! wanakwenda kuvuruga mazungumzo tu! Kumbe njaa ilikuwa inawasumbua! nasikitika sana kuona Prof. Lipumba ana bongo kweli lakini yupo sehemu isiyo sahihi! Hivi nyie CUF na TLP si mliunga mkono kwa kishindo na mpenzi wenu CCM?! Mnataka kwenda Ikulu kusema nini?!
   
 2. m

  maluguthengosha Member

  #2
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kunywa chai.kupiga picha na baba miraji. Kukutana na luhanjo kabla hajastaafu na kuangalia pango la walanguz lilojengwa na wajeruman. Chama cha wananch oyeee
   
 3. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Wanataka kuwatumia Mrema, Cheyo, na baadhi ya wabunge (na makada wengine) wa CUF ili kupunguza makali ya hoja za CHADEMA. Kwa kuwatumia hao itaonekana kama vile mawazo ya CDM ni ya wachache. Tunajua jinsi fedha ilivyo silaha kuku ya CCM. Hao wengine sasa watakuwa wameishakamata mshiko wao na kupewa maelekezo jinsi ya kuvuruga hoja za CDM. Lakini hoja ya kukataa mswaada wa kuandika katiba mpya (siyo kurekebisha) haiwezi kuishia kwenye vyama vya siasa pekee. Lazima irudi kwa wananchi. Kikwete na CCM wakiwa wabishi hiyo Katiba itakuwa ya kwao. Lazima uzuke mgogoro wa kikatiba ambao unaweza kutatuliwa na mahakama ya katiba ambayo mpaka leo Tanzania hainayo.
   
 4. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  CUF hawana sababu ya kukutana na JK kwasababu wao wametoa mchango wao kupitia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na wameunga mkono Muswada wa Serikali Bungeni. Kwa upande wa TLP nao wameunga mkono Bungeni pitia mwenyekiti wao Augustine Mrema. Sioni sababu ya kupoteza muda Rais kukutana na hivi vyama. Cheyo nasikua alikua safari,hata hivyo sioni kama ana msimamo tofauti na CCM kwasababu haujawahi msikia akizungumzia Katiba Mpya kama moja ya vipaumbele kwa UDP na pili chama chake kimebakia chama cha kifamilia,ataongozana na akina nani kwenda Ikulu?
   
Loading...