Geza Ulole
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 55,120
- 69,554
Wajameni mie nashangaa hawa wenzetu wenye kuongelea muungano wa vyama vya upinzani katika chaguzi na kuishi maisha ya usaliti; Je, watafanya hivi mpaka lini? Hebu tujiulize CUF wanasema ati Upinzani usimamishe mgombea mmoja wakati hawajaonyesha kivitendo hata pale ambapo CHADEMA si Mpinzani yaani katika yale majimbo yaliyo chini ya CHADEMA na ilihali tumeona sehemu kadha wa kadha sehemu ambapo CHADEMA haijasimamisha Wabunge, ilitoa support kwa CUF na hata katika madiwani (pale chama kingine cha upinzani kinapokubalika zaidi)! Sasa huu unafiki unatoka wapi? Juzi hapa CHADEMA kama chama kilichotimiza vigezo vya kuunda upinzani iliwasiliana na CUF wakiwaeleza nia yao ya kutaka kushirikiana, naskia ikatoka command toka visiwani ati waungane na TLP, UDP na NCCR-Mageuzi! jamani at least NCCR-mageuzi naweza sema wanadamu changa ila wanaangushwa na Mwenyekiti wao, ila TLP nao jamani? hata UDP nina wasi pia na Cheyo, ila nashukuru kwa kumpigia Marando! Kuongeza unafki uliokubuhu kwa hawa CUF (CCM B) wakahaidi kumuunga mkono Bw Mabele Marando; cha kushangaza woote wakapigia CCM uspika! Je tunapata picha gani? Mapandikizi kushoto na kulia sio? Jamani nashukuru kwa CHADEMA kuliona hilo...hawa watu wamenunuliwa kaeni nao chonjo! nia yao ni kuwasambaratisha hawana nia dhabiti na wala hawajui maana ya neno upinzani! vijiba vya roho vinawasumbua babu! hata mtoto wa vidudu atakuambia Marando was more qualified kuchukua kiti cha uspika zaidi ya mama Makinda by far ila hawa wenzetu wakaamua kumpigia kura wa CCM A angalieni tu CCM A hawamuangalii mtu usoni wanapotaka kukutoa roho (kukuisraili)... ?? lets wait and see na huo urafiki wa mashaka wa CCM A na B! utaishia wapi? meanwhile endelezeni zile itikadi zenu za jino kunako Pengo waana ile jino kunako jino ni marehemu siku mingiiiiiiiiiiiiiiii!