CUF na CHADEMA waungane kuiondoa CCM madarakani - Mtatiro

Wote wanajua 'umoja ni nguvu, utengano udahifu' lakini kumbuka hulka ya mwanadamu niubinafsi na inapofikia kuungana kuna watu watapoteza mkate wao, hapo ndio utasikia wapinzani wanachomekeana kwa faida ya ccm.

Kwa wanaojua historia ya mageuzi watakumbuka harakati zilizofanyika kuunganisha upinzani na ikashindikana. Wengi wetu tunasubiri ccm ijifie yenyewe tatizo sijui kama vyama hivi wamejipanga vipi kuziba ombwe la uongozi au nchi itaishia mikononi mwa 'ma-mbwa'?
 
,tatiro anajidangamya na kujaribu kuwadanganya watu.tatizo si wapinzani kuungana ila tatizo ni aina ya wapinzani wenyewe.cuf walishajipambanua kuwa sehemu ya serikali hivyo si rahisi kwa cdm na cuf kuungana.
 
Kweli mfa maji haachi kutapatapa. Vipi ule mgogoro wao wa kuchapana makonde kule Arusha umekwisha na sasa wanataka kuungana? Huyu Mtatiro kweli sasa nimeona anataka kuhamia CDM. Nataka kuwa kama mtabiri, miezi miwili haitapita tutamsikia kule kwa vidole viwili kwani kauli hii ni mpya kabisa kutoka kwa huyu mkiristo.

Mkuu Issue ya Dini inaingia vp hapo?
 
cuf tayari wapo ikulu hivyo hawawezi kukomaa tena.chadema ndio wanaoweza kupambana kwenda iulu.
 
Bwana Mtatiro ametoa wazo zuri sana. Na wote tunaelewa hii ndiyo njia rahisi ya kuiondoa CCM madarakani.

Sasa tumuulize bwana Mtatiro maswali ya msingi yafuatayo, akiweza kuyapatia UFUMBUZI basi tutakuwa tayari kuishauri CHADEMA ishirikiane na CUF: I'm very serious about this, na nadhani hata wanajamvi wengi watanisapoti;

1. Je itawezekanaje CUF kuwa chama tawala na wakati huo huo kuwa upande wa vyama vya upinzani?
Maana CUF ni chama tawala-inatawala sehemu ya JMT kwa kushirikiana na CCM

2. CUF Ina MUAFAKA na CCM, ambao umezaa ndoa yao. Sasa itakuwaje huku ndoa na CCM na wakati huo huo urafiki na CHADEMA?

3. Kama CUF iko serious kukuza urafiki na CHADEMA, je CUF iko tayari kuvunja MUAFAKA na CCM na KUJITOA katika GNU?

4. Moja ya sera za CUF ni kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kama itashinda uchaguzi. CHADEMA, in black and white, haiko tayari kuunda serikali na mafisadi-CCM, Je CUF iko tayari kurekebisha hili?

Haya mambo manne ndiyo masuala muhimu yanayozuia urafiki wa kweli kati ya CUF na CHADEMA. Mengine ni madogo na yanajadilika na ni rahisi kuafikiana.

Sasa ninamwomba bwana Mtatiro kwa manufaa ya nchi hii na wananchi atupe UFUMBUZI wa haya masuala ya msingi.
Mimi Nina uhakika haya yakitatuliwa, CHADEMA iko tayari kushirikiana na CUF
 
Kwani lengo ni nini kuiondoa CCM madarakani, Kwenda Ikulu au kuwaletea wananchi maendeleo? Saidieni maendeleo bila hata kuiondoa CCM madarakani na hapo wananchi wenyewe wataona umuhimu wenu. CCM haiwezi kuondoka madarakani kwa kupnga kuungana bila kujua mnataka kuwafanyia nini wananchi.

Mkuu, utawezaje kuwaletea maendeleo wananchi bila kuwa na serikali? Lazima CCM iondolewe madarakani kwanza ndio maendeleo yaje. CCM ndiyo kikwazo cha maendeleo ya nchi hii. Au we hujui unahitaji kuelimishwa?
 
mtatiro hapa kaja na hoja ya msingi,badala ya kutoa hoja mnaishia kuchambana kama mabibi harusi hapa,kweli jf sasa ni jamvi la wambea

Hiyo ni hesabu tu ndugu yangu, hakuna hoja yoyote ya maana aliyoleta Mtatiro hapo. Ukumbuke hoja hiyo walishatoa wenzie mwaka 2010 kabla ya Uchaguzi mkuu na haikuwezekana ( Kama unakumbuka CDM walichelewa sana kuweka mgombea Urais). kila mtu ana style yake ya kutoa hoja, mwingine ataweka picha, mwingine maelezo marefu, mwingine atachora table, mwingine graph, unaweza kuita watu maBIBI harusi or what ever, but the end of the day you might be calling youself those good names !

Hizo "Plus" na "Equal" signs tunazoweka hapo ni hoja tayari. Tunachotaka kusema ni kwamba, vyama vya upinzani vinaweza kuungana vyote, na baadae vitaweza hata kuungana na chama tawala, end of the day hakuna tutakachokuwa tumefanya. It was a move from Single party to Multipartism, na lengo kubwa lilikuwa ni kuwa na jicho la upande mwingine. baada ya kuungana-ungana kwa sababu yoyote ile, tutarudi pale pale tulipotoka. Badala ya kusajili vyama vyote hivyo ili viungane tena, si tufute tu usajili wa baadhi ya vyama tunavyoona haviwezi kucompete ili tubaki na viwili au vitatu vitakavyoweza kuhimili competition ?

ukiona hatuweki hoja hapa, tunaona mada hiyo ni nyepesi mno kiasi cha kuhitaji kujadiliwa kwa maelezo marefu. Kwakuwa vyama vingi bado vinahitaji kukuwa na kujiweka sawa, Labda mtu alete hoja ya kuachiana maeneo ambayo mwingine yuko strong, lakini tatizo litabaki pale pale (Tutasema ukanda), Vyama hivyo vitapaje kukua katika yale maeneo wanayoachiana ?

HAYA NDIYO NILIYOKUWA NAJARIBU KUYAWEKA PALE KWENYE ALAMA ZANGU ZA KUJUMLISHA ambazo ndugu yangu Kalunguine, kwa uwezo wako mkubwa wa kuelewa, ukaona ni kuchambana kama maBIBI harusi ! Hata hivyo nakushukuru sana kwa mchango wako huo !
 
Kweli mfa maji haachi kutapatapa. Vipi ule mgogoro wao wa kuchapana makonde kule Arusha umekwisha na sasa wanataka kuungana? Huyu Mtatiro kweli sasa nimeona anataka kuhamia CDM. Nataka kuwa kama mtabiri, miezi miwili haitapita tutamsikia kule kwa vidole viwili kwani kauli hii ni mpya kabisa kutoka kwa huyu mkiristo.

Wewe ni mdini kweli kweli kweli, ni matatizo ya kisaikolojia. Nenda katibiwe
 
Itakuwa ni kuruhusu mke mmoja aolewe na wawaume wawili. Kimsingi kura walizopata CUF, unganisha na za CCM ndo ujue kuwa ni familia moja. Wala CDM hawawezi kukubali kukamatwa ugoni!!!!
 
sijui Mtatiro anamaanisha CUF ipi cuf ya Zanzibar au CUF bara?.. maana wabunge wao toka ZNZ walishatamka kuwa CDM inaongozwa na DISCO JOCKER
 
Hulka ya ubinafsi na wivu ndivyo vinavyotuangamiza. Ukitaka kupata mafanikio kuna kila hali ya kutokea jasho na uvumilivu mwingi wa kuvumilia na kuvumiliana hadi kuzoeana kutakakojenga tabia ya kuwa na common goals.

Majeshi yana vikosi mbalimbali ambavyo kila kikosi kina mafunzo ya aina yake, vya anga, majini, nchi kavu, mizinga, nk. Kila kikosi kikiamu kufanya kazi kivyake bila mwunganiko wa vikosi vyote ni dhahiri ushindi utabaki mikononi mwa adui.

CUF licha ya kukubali kuunda serikali ya umoja Zanzibar ni jambo linalohusu dola ya Zanzibar, ingawa iko ndani ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania. Makubaliano hayo yalihuzu Zanzibar hivyo si kigezo cha kuzuia wave la kuunganisha nguvu na Chama kingine katika kutekeleza Azima yao. Vinginevyo tutakuwa watu wenye mtazamo finyu katika hili.

Vyama vikubwa vinne Chadema, CUF, NCCR Mageuzi, na TLP vyenye uwakilishi vyenye uwakilishi bungeni vikiamua kuwa kitu kimoja katika uchaguzi Mkuu ujao kwa kuwa na jopo la kusimamisha wagombea wenye sifa katika majimbo na Taifa, vyama kuna uwekezakano mkubwa sana wa kuinyanyasa CCM na kuipa kipigo cha mbwa mwizi na kuisambaratisha kabisa.

Kauli ya Julius Matatiro ni kilio cha wengi baada ya kuona mizengwe ya CCM inazidi kuwaliza vyama vya upinzani kwa sababu ya ufa uliojengeka kati ya chama na chama wakati kimoja kinapoonekana kuanza kuwika ni kuanza mikwara ya kukichafua badala ya kuunga mkono.

Chadema kama nilivyosema katika mada moja majuzi wanatakiwa watazame nyuma walikotoka, matokeo ya chaguzi, na kuziondoa kero wanazoona zinaleta taabu katika kuunganisha nguvu ya Vyama vya upinzani nchini.

Rais Mkapa alipotembelewa na Mwai Kibaki mara baada ya kuiangusha KANU alitoa mwanya kwa Mwai Kibaki kuongea na viongozi wa vyama vya upinzani nchini kwa lengo wajifunze wenzao walivyofanikiwa. Mwai Kibaki alisema wazi kilichosaidia ni kuunganisha nguvu za vyama vya upinzani vinginevyo KANU isingepata kipigo kile cha mbwa mwizi. Mkapa alifanya vema, lakini vyama vya upinzani badala ya kujifunza aliyowausia Mwai kibaki wakarudi na mambo yale yale yaliyozoeleka kila chama kivyake, vinginevyo leo tungekuwa tunazungumza CCM ilivyokula mwanguko wa Mende katika uchaguzi Mkuu uliopita kama nguvu zao zingeunanika.

Nguvu ya sasa katika kujenga upinzani wa kweli wenye nguvu ni kuunganisha nguvu za vyama vya upinzani kuwa kitu kimoja katika chaguzi ndogo zilizosalia na pia kujiandaa uchaguzi Mkuu ujao kuwa na nguvu moja kwa kusimamisha mgombe mmoja katika kila jimbo mwenye sifa za kuukubalika kwa wapiga kura.
 
Tatizo si kuungana bali Wananchi wengi hawana elimu ya Uraia na kujua umuhimu wa kura yake. CHADEMA isimame kama ilivyo hawa 'cuf' vigeugeu mno, hawachelewi kujiengua na kuanzisha chama kingine. N.b: ADC, FORD,
 
kuungana kwa sababu na wakati wa uchaguzi siyo suluhu! Kuungana kunakotarajiwa kunatakiwa kutokane na utashi wa ndani wa viongozi na wanachama wa vyama husika.

Hili linatakiwa lianzie na kuzipitia katiba za vyama husika kuona ni wapi wanawiana kiitikadi na wapi wanatofautiana na kwa ukubwa gani! Kinyume cha hapo utakuwa ni muungano bandia kwa ajili tu ya tamaa ya kuingia madarakani lakini muda si muda mtavurugana kwa kukosa kushughulikia misingi ya tofauti za vyama.

Yaani tofauti ninazozungumzia ni za kwa nini kuna CDM, CUF, TLP, n.k. Kwa nini hawa wote hawakujiunga katika kimojawapo kilichotangulia kuanzishwa?

Jibu la swali hili kwamba kama si tamaa binafsi tu za kutaka kupata ruzuku na/au madaraka, basi ni wazi kwamba kuna tofauti za kimsingi ambazo kabla ya kuungana kuiondoa CCM madarakani ni lazima zifanyiwe kazi si kwa lengo mahsusi ya kuiondoa CCM bali kuunganisha nguvu ya kuwatumikia wananchi.

Maana kuiondoa CCM ni jambo moja na kuwatumikia wananchi walio wengi ni jambo jingine.
 
Haiwezekani kwa vyama vyenye mitazamo tofauti kabisa karibu katika kila jambo kuungana. Hii italeta matatizo zaidi hata kwetu wananchi wa kawaida na tukaona heri CCM ingeendelea. Lengo si kuiondoa CCM kwa gharama yoyote hata kama ni kuingia kwenye taabu zaidi; bali lengo liwe kuiondoa CCM kuelekea na kuingia kwenye hali bora zaidi na kwa vyovyote vile muungano wa CUF na CHADEMA hautaleta hali bora kwa watanzania.
 
Nakemea roho ya usaliti, pepo mchafu toka katika jina la sultani lipumba. Yaani mtatiro anshawishi CUF aungane na CDM kumsaliti mumewe, that is not fair.
 
Kwani CUF si tayari mmeshaungana na CCM mnataka muungano mwingine tena? Nyie jitahidini mshinde kwenye maeneo ambayo tayari mnadhani mnayo nguvu, na chadema nao watapigana kushinda kwenye maeneo yao! Nyie CUF bara mmefanya kosa kubwa kuwekwe mfukoni na CCM! huku bara watu hawana imani nyie tena!
 
Tatizo siyo kuungana bali wananchi hawana mwamko wa Mabadiliko wapo tu wanakubali kupewa zawadi na CCM na kusahau kabisa kuwa ule ni unyonge wa kutojitambua. Kumbuka Hakuna umaskini mkubwa kama wakukosa kujitambua unachokifanya.
 
watz wanapaswa kuungana kiitikadi,waache tofauti,watakiweka chama chochote wanachokitaka madarakani.hii inahitaji elimu ya uraia ya kutosha.
 
Back
Top Bottom