CUF na CHADEMA waungane kuiondoa CCM madarakani - Mtatiro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF na CHADEMA waungane kuiondoa CCM madarakani - Mtatiro

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Oct 31, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ifuatayo ni taarifa rasmi iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Julias Mtatiro kuhusu uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika Jumapili iliyopita:.............Fuatilia......


  Yalikuwa mapambano ya pesa. Wanaogawa pesa wataendelea kushinda chaguzi hizi, hapa hakikomeshwi chama fulani, wanakomeshwa watanzania ambao hadi leo wanaishi kwenye lindi la umasikini, maradhi na ujinga.

  Kwa vyovyote vile CCM wameshinda kwa mgongo wa mgawanyiko wa upinzani. Kuna watu ati wanasifia vyama vyao vya upinzani hapa, tunajidanganya wenyewe bado.

  Ukweli ni kuwa... , mgawanyiko wetu unatuponza sana, na kwa vyovyote vile kwa kadri tutakavyozidi kugawanyika huku tuKijidanganya ati PEKE YETU TUTAWEZA - mwisho wa siku hatutaweza.

  Huu ungekuwa uchaguzi wa jimbo moja peke yake, au kata moja peke yake au kijiji kimoja peke yake, ingekuwa rahisi kwa chama chochote chenye pesa za kumwaga kuzimwaga na kupambana na pesa za CCM na labda upinzani ungeweza kushinda.

  Lakini katika chaguzi zilizosambaa nchi nzima ni vigumu sana upinzani kupambana na CCM ukiwa katika mgawanyiko mkubwa sana. Hii ni kwa sababu CCM wana muscles pana za kiutawala na ki-ujanja zilizozagaa kila pembe ya nchi.

  Tutajisifu hapa kwa TAMBO na MBWEMBWE, tutasifia kila mmoja chama chake lakini ukweli ni kuwa CCM wanafurahia sana mgawanyiko wetu, angalia baadhi ya matokeo hapa chini;
  KATA YA MNELO MIEMBENI- WILAYA YA NACHINGWEA;
  CCM 818,
  CUF 611,
  CDM 138.

  KATA YA KITANGIRI - WILAYA YA NEWALA,
  CCM 1416,
  CUF 1195,
  CDM 157,

  KATA YA LWEZERA - WILAYA YA GEITA,
  CCM 1309,
  CDM 933,
  CUF 317.

  KATA YA LIKOKONA - WILAYA YA NANYUMBU,
  CCM 1142,
  CUF 927,
  CDM 346,
  NCCR 31.

  KATA YA MAKATA - WILAYA YA LIWALE,
  CCM 808,
  CUF 850,
  CDM 24,
  NCCR 03,

  KATA YA MAGOMENI - WILAYA YA BAGAMOYO,
  CCM 1240,
  CUF 780,
  CDM 420
  Huu ni mfano wa kata chache tu ambazo upinzani wenyewe tumezigawa CCM, hata kata ya MAKATA wilaya ya liwale ambayo CUF tumeshinda utaona tumeipata kwa tofauti ya kura kidogo na CCM na kama CDM wangepata kura kidogo tu zaidi hata hiyo ingekwenda CCM.

  Ikiwa pana chama kimoja cha upinzani kitajidanganya ati kwenye hizi chaguzi pana kitaishinda CCM peke yake, chama hicho kinajidanganya.

  Vyama vya upinzani lazima tukae chini na tujitafakari mara mbilimbili mwelekeo wa siasa zetu ikiwa kweli tunahitaji kuiondoa CCM.

  Wachangiaji waweke mawazo yao hapa, wasije kutetea vyama vyao.
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kwani lengo ni nini kuiondoa CCM madarakani, Kwenda Ikulu au kuwaletea wananchi maendeleo? Saidieni maendeleo bila hata kuiondoa CCM madarakani na hapo wananchi wenyewe wataona umuhimu wenu. CCM haiwezi kuondoka madarakani kwa kupnga kuungana bila kujua mnataka kuwafanyia nini wananchi.
   
 3. GODLOVEME

  GODLOVEME JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  ni sawa but kwanini tukamilishe mzunguko wa kuwa kwenye duara moja
  CUF join CCM
  CUF join CDM
  Therefore
  CDM and CCM are joine together indirect as a result no upinzani tanzania
   
 4. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  CHezea CCM wewe, mmeanza kulalama tayari. Kwa nini siyo CUF na TLP?
   
 5. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kweli mfa maji haachi kutapatapa. Vipi ule mgogoro wao wa kuchapana makonde kule Arusha umekwisha na sasa wanataka kuungana? Huyu Mtatiro kweli sasa nimeona anataka kuhamia CDM. Nataka kuwa kama mtabiri, miezi miwili haitapita tutamsikia kule kwa vidole viwili kwani kauli hii ni mpya kabisa kutoka kwa huyu mkiristo.
   
 6. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mkuu nakuja baadaye kidogo au vipi.
   
 7. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mtatiro bana.
  Huyu si ndo kila siku yeye na mahafidhina wengine hawaachi kuitukana chadema. Sasa kama kuungana wanaruhusiwa waungane na dovutwa na mziray. Kwani kuna mtu amewakataza.
   
 8. K

  Kishalu JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 850
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Hapa tatizo linakuja kuwa CUF tayari imeungana na CCM sasa ukisema waungane na CHADEMA itakuwa unataka kuuwa Chadema kiujanjaujanja.

  Swala hapa sio chama ila kumsimamisha mtu makini ktk nafasi husika maana wengi wa watanzania wanaangalia mtu makini sio tu mnasimamisha mtu yeyote then mnasema kwa kuwa chama kinakubadilika.

  Atachaguliwa hapo sio sahihi pili itafutwe mbinu ya kuwa na tume huru ya uchaguzi maana hata huu uchaguzi mdogo watu wengi wameshindwa kupiga kura kwa visababu vidogodogo tu
  .
   
 9. M

  Molemo JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mtatiro alivyo mnafiki amechukua zile kata ambazo CUF imepata kura nyingi ili ahalalishe hoja yake.Kwanini asiweke matokeo ya kata zote 29?
   
 10. K

  Kimweli JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 865
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Nyie ndo wakutukana ukristo umetoka wapi hapa, umeongea mambo ya maana ila tatizo ni hilo neno.
   
 11. h

  hacena JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kiufanya hila ni dhambi kubwa sana kwa nini watu huwa hapendi kuwa wakweli, kuna kata kanda ya ziwa ukijumlisha kura za CDM na CUF, CCM wameshindwa na CUF walipata kura 116 tu, mbona hawazungumzii uchaguzi wa Tarime ambapo CUF walimchukuwa Mwera na kugawa wapiga kura na CCM kushinda.
   
 12. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tatizo mmoja wapo ni CCM-B
   
 13. Mkuu rombo

  Mkuu rombo JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ni bora cdm waungane na nsisiara mageuzi,tlp,chausta,kuliko caf ambao wameshaungana na ccm
   
 14. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mtatiro si "unadoa" na CCM, sasa unataka bwana mwingine?
  sijawahi kuona "Mwanamake" ana mabwana wawili...
   
 15. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,936
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  operation mchakamchaka ni kwa ajili ya kuipinga cdm ..... kafu bana
   
 16. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #16
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hii ni ndoto ya mchana juani, litawezekana vipi hili wakati CCM na CUF wapo kwenye utamu wa ndoa yao ili kuvuruga upinzani? Mtatiro acha danganya toto hizi.
   
 17. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  cuf hawajiamini, hawana fikra na mikakati ya kuwakomboa watanzania, inapenda kuolewa na famous figue, wamegundua mume ccm kwisha habari yake, wanataka kulazimisha talaka moja wakajipime kwa mume mpya cdm, sasa wanajitongozesha, ngoja tuone jinsi chadema watakavyowavalia miwani ya mbao.
   
 18. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Matatiro, lakini nyinyi CUF si mlishaungana na CCM huko Zanzibar?

  Frankly speaking vyama vya upinzani hai kama CUF-Bara nacho ni Upinzani basi ni CDM na CUF ONLY.

  No disrespect to other political parties, lakini kuungana na vyama kama TLP, UDP, TPP Maendeleo, JAHAZI, DP, UPDP na hata NCCR-MAGEUZI ni kurudisha nyuma harakati za ukombozi wa nchi hii kutoka CCM.

  Chama ambacho CDM ingeweza kuunganisha nacho nguvu ni CUF lakini bahati mbaya wenzetu mmeshaunganisha nguvu na Chama Tawala CCM.
   
 19. K

  Kigano JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 349
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  If the idea is multipartism: Then
  CUF + CCM = CCM in ful control
  CUF + CDM = CCM in full control + CDM
  CCM in full control + CDM = CCM in full control

  Therefore: CUF + CDM + CCM = CCM in full control
  Unaweza kujua nani yuko nyuma ya huu ushauri.
   
 20. M

  MARUKENI Member

  #20
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtatiro kabla hujaongelea habari zozote za kuungana cdm na cuf rejea hotuba zako zote ulizozitoa za kuishutumu cdm ndo utuletee huo unafiki wako .hao waliokutuma uishie hapo hapo.
   
Loading...