Ni chama chenye historia ya pekee hapa Tanzania.
Kimejipambanua kufuata kwa vitendo misingi ya demokrasia na kutumia njia sahihi za diplomasia na ustaarabu wa siasa za vyama vingi katika kujijenga kwake.
Wengi wetu hatuelewi nini chama hiki kinafanya tunabaki kutazama matukio na kuhukumu tu.
Kilidhihirika nguvu zake (Zanzibar) uchaguzi wa mwanzo tu Tanzania miaka ya 1995, kiliibwaga CCM na kilichotokea ni historia. Jee kwa CCM kulazimisha madaraka ndio CUF ilikufa?
Cuf walitumia njia ya mazungumzo na wala sio kwenda msituni kujenga hoja zake na kuishawishi dunia hali halisi ya demokrasia Tanzania. Katika hali fulani licha ya mtawala kufanya hilba bado CUF ilipata fursa kujieneza zaidi na kufanya siasa za kistaarabu.
Uchaguzi wa 2000 Zanzibar-walijitutumuwa zaidi kuionesha dunia namna demokrasia ilivyosiginwa Tanzania. Yaliyotokea ni historia vile vile. Waliendelea kutumia njia za kidemokrasia na kikatiba kuonesha madai yao yaliyopuuzwa na watawala wa CCM. Walifanya maandamano kwa njia za kikatiba lakini mtawala alitumia mabavu kukandamiza. Pamoja na athari mbaya kwa wananchi kupata madhara lakini waliiamsha dunia kufuatilia kwa karibu kilichokuwa kinaendelea Zanzibar. Hata hivyo naamini kuna kitu CUF walijifunza kupitia maandamano yale na nadhani hawakutaka kufanya makosa mengine.
CUF walishiriki tena muafaka wa 2000- 2005kuondowa sintofahamu ya siasa na mara zote watawala walifanya hiana ndani yake ili kuipoteza CUF na kuuwa morali ya wanachama wake Lakini jee CUF ilikufa?
CUF haikuchoka na wala kamwe haikufikiria njia ya mapambano na uharakati kama wengine wanavyofikiri kwa hili la 2015.
Bado CUF ilitumia njia za kidemokrasia ndani ya Bunge na Baraza la wawakilishi kutaka kuwe na haki na usawa katika mfumo wa demokrasia.Nini kilitokea kwa maslahi mapana ya taifa na kwa wananchi kupitia jitihada za CUF na Maalim Seif?
Tumeshudia wote 2009 kwa mara ya kwanza jitihada zilizaa matunda kwa CUF kufanikisha kuundwa SUK kupitia uungwana wa MH KARUME (Amani). Tena kwa njia ya maridhiano ya kikatiba na wala sio MOU. Wazanzibari walipiga kura Kuidhinisha GNU na kuwekwa mfumo mzuri wa maamuzi .
Ni CUF hiyo hiyo iliyoamini mwanzo ule ungeendelezwa na kuheshimu ustaarabu na walishiriki katika SUK vizuri kwa mustkbali wa Taifa.
Ikumbukwe kuwa wakati wote huo walishatengeneza image kwa ulimwengu kwa unguli wa kisiasa za kistaarabu na kuheshimu misingi ya kidemokrasia na kamwe hawakutanguliza maslahi binafsi.(Case studies zao ni nzuri na zipo).
Hali ya uchaguzi 2015 na somo kuu kotoka CUF.
Uzalendo wa nchi na misingi ya demokrasia ilikuwa ndio kipaumbele chao. Hawakufikiria madaraka hata pale Katiba na haki zinaposiginwa. Aliyofanya jecha na Utawala wa CCM Dunia imeona na historia imeandikwa ya kuvunjwa katiba na misingi ya Demokrasia.
CUF iko vile vile kama awali. Haikuterereka na kutoka katika mstari wake eti wakimbilie kushiriki batili na kuvunja katiba ilimradi waingie Baraza la wawakilishi akapambane na CCM. Hio sio siasa na wala sio misingi ya CUF.
Kwa hili la uchaguzi wa 2015 na ule unaoitwa wa marudio umezidi kuipambanua CUf kuwa ni nani hapa Tanzania.
Dunia imeshuhudia kwa mara nyennine uimara wa CUf na uongozi uliotukuka na mfano wa kuigwa kwa Afrika.
Nchi nyengine huwezi kufika huko katikati unakutana na misururu ya damu.
Somo walilotowa CUF itakuwa ni aibu kwa dunia na kwa nchi za Magharibi ikiwa hakutachukuliwa hatuwa mahsusi. Uchafu uliofanyika Zanzibar kama utaachwa basi itakuwa ndio mwisho wa demokrasia ya dunia.
Somo kuu ni kuwa CUF imeendelea kuwa mwalimu wa demokrasia Tanzania.
Nawasilisha