Cuf msidandie lift ya bure | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Cuf msidandie lift ya bure

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NgomaNzito, Aug 4, 2009.

 1. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  'CUF MSIDANDIE LIFT YA BURE'

  Mkuu wa nanihiiNinaomba nitoe maoni yangu kwa Umma wa Watanzania kuhusu hili sakata la Bunge na Utawala(serikali).

  Nimesoma kwenye vyombo vya habari vya Kibongo kuwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni amemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano kujiuzulu wadhifa wake, kutokana na mwelekeo wa kisiasa Dodoma.

  Mimi nafikiri ameenda mbali kidogo, Watanzania walipopiga kura 2005 hawakumpigia Malaika kura, walimpigia binadamu kama wao, kama kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi, serikali imekubali kushindwa bungeni na kuomba muda wa kutekeleza maazimio ya Bunge, mimi kama Kijana wa Kitanzania ninafikiri tumeanza kuwa na Democrasia ya kweli. Ninapenda kuwakumbusha Watanzania kwamba Rais Kikwete ndio Rais ambaye amekubali democrasia ndani ya bunge kuliko marais wengine wote waliopita.

  Alikuwa na uwezo wa kuwanyamazisha Wabunge wote kupitia vikao vya CCM na hakuna ambaye angefurukuta hata wapinzani. Wabunge wote hawa tunaowasifu kwa ujasiri walikuwepo hata wakati wa Mkapa, mbona hatukujua majina yao.

  Wako wapi akina Masumbuko Lamwai, Mabere Marando, Abbas Mtemvu, Lyatonga Mrema na wengine wengi, wote hawa walikuwa moto wa kuotea karibu bungeni.

  Ila kwa sababu JK amebadilisha mwelekeo wa Dodoma na kuuweka wa Democrasia zaidi wapinzani wanafikiri kuna ugomvi kati ya Wabunge wa CCM na Serikali yao. Hii ndio Democrasia ambayo majirani zetu wamekuwa wakinufaika nayo miaka nenda miaka rudiHii ndio Democrasia tuliyokuwa tukiililia Watanzania, uwezo wa kumpinga mkubwa wako bila kumkosea heshima, Wabunge wa CCM sasa wanaipinga serikali yao bila kuitwa watovu wa nidhamu.

  Hakuna vikwao vya akina Kolimba, wala Iddi Simba. Hakuna Kikao cha dharura cha Kamati Kuu wala cha Kamati ya Secretarieti ya Maelekezo Makao Makuu kama ambavyo tuliyasikia huko nyuma.

  Ninaomba Wapinzani wasitake kuichonganisha Serikali na Wabunge wake halafu wakaja poteza uhuru wa kuikatalia serikali.

  Hii ndio mara ya kwanza katika historia ya nchi kwa kumbukumbu zangu, ambapo serikali imekubali kushindwa katika mijada ya Bunge.

  Kwanza ninaomba kuipongeza Serikali ya Kikwete, kudumisha Democrasia ya kweli, na kukubali makosa pale panapooneka kuna makosa.

  Nafikiri tuangalie kwa macho manne haya mabadiliko hayakuja kwasababu tuna wabunge machachari bungeni, ishitoshe hawa wabunge wote walikuwepo kipindi kilichopita isipokuwa Zito na Shibuda. Ingekuwa Kipindi cha ndugu waliotangulia sidhani hata kama kuna mtu angejiuzulu, wala uchunguzi ungeruhusiwa toka Bungeni, sasa tusijisaidie kambini kabla mazoezi hayajaisha.

  Sisemi kwamba serikali haina makosa, ila ninachotaka kuwakumbusha Watanzania wenzangu tusidhani tumefika hapa tulipofika kwenye Democrasia ya kweli kwa sababu haya matatizo yanayotokea leo serikalini ni mapya, la hasha, fisadi kama hizi za Richmond na pacha wake Rada ni marudio tu kwenye nchi yetu, tofauti kubwa ni kuwa, this time, Serikali imekubali isifanywe siri bali wananchi waweze kujua jinsi Serikali yao inavyofanya kazi.

  Nachukua fursa hii kumpongeza Spika, kwa kuongoza ujasiri na Democrasia ndani ya Bunge, na kuruhusu mijadala bila kupendelea upande mmoja.

  Nampongeza Waziri Mkuu kukubali kuwa panapokuwepo na makosa mkubwa hukubali makosa yake na kuomba muda kurekebisha. Kama hali hii itaendelea kwenye nchi yetu basi tunapiga hatua kubwa sana katika Democrasia. Kama suala ni Hosea na Mwanyika! Mbona hata waliojiuzulu hawakujiuzulu kikamilifu, waliachia Uwaziri, wakaendelea kuwa Wabunge.

  Kwa mantiko hiyo ni kosa kuwa Fisadi Waziri lakini ni sawa kuwa Fisadi Mbunge! Mimi ninamwomba Rais Kikwete awateue akina Hosea na Wenzake kuwa Wabunge, halafu wajiuzulu nyadhifa zao ili wote wawe sawa! Akimaliza hilo, CUF nao waanze tution ya Democrasia kwa kufanya Uchaguzi mwingine wa viongozi wao wa Kitaifa, kama walivyo Chadema na CCM.

  Huwezi kuwa Kiongozi miaka ishirini, ofisi ileile, chama kilekile, nashindwa kuelewa kwanini Professor Lipumba asitumie utaalamu wake wa Uchumi kuapply "Theory of Diminishing Return" kwenye uongozi wake.

  Wadau msinimeze; nimetumia uhuru wangu wa Kikatiba, kutoa maoni yangu bila kuvunja sheria yoyote

  Source: MICHu

  WPwpkuja@cba.ua.edu

  Je ni kweli aliyoyasema mdau tujadili
   
Loading...