‘CUF Lipumba’ wakaidi agizo la Polisi, waendelea na mkutano

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,781
5,205
cuf1pic.jpg

Kwa ufupi
Licha ya Polisi wilaya ya Ilala Kanda Maalum ya Dar es Salaam kutoa zuio la kufanyika kwa mkutano mkuu wa CUF upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, mkutano huo unaendelea huku ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ukiubariki mkutano huo


----
Dar es Salaam. Licha ya Jeshi la Polisi kuzuia mkutano wa Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Mwenyekiti anayetambulika na ofisi ya msajili wa vyama vya Profesa Ibrahim Lipumba, mkutano huo umeendelea muda mfupi baada ya mwenyekiti hiyo kuwasili ukumbini.

Naibu Katibu mkuu wa chama hicho-Bara, Magdalena Sakaya akizungumza katika mkutano huo leo Jumanne Machi 12, 2019 amesema jumla ya wajumbe waliofika wamefikia 598 hivyo akidi imetimia.

Mkutano huo ambao waandishi wa habari hawaruhusiwi kuingia ukumbini unaendelea ukipata baraka za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa, ambapo Naibu Msajili, Sisty Nyahoza ndiye aliyeufungua kwa kutoa hotuba.

Katika hotuba hiyo, Nyahoza amesema mkutano huo unafanyika kwa mujibu wa Katiba ya CUF ndio maana umetambuliwa na Ofisi yake.

Amewapongeza kwa kile alichosema wamehimili mapito ya mahakama na wameendelea kukilinda chama.

Vilevile amewapongeza kwa kuteua bodi mpya ya wadhamini na kuwakumbusha wajibu wao wa kutunza Mali na fedha.

Amewataka pia kuzingatia mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa.

Nyahoza pia amesema sheria ya sasa ya vyama vya siasa hairuhusu vyama kuwa na vikundi vya ulinzi.

Baada ya hotuba ya Nyahoza, Sakaya ametangaza mchakato wa marekebisho ya CUF.

Licha ya RPC wa Ilala, Zubery Chembera aliyeleta taarifa ya zuio, askari wa jeshi hilo wameendelea kubaki eneo hilo wakiendelea na ulinzi.

Chanzo: Mwananchi
 
Huyu ndio profesa bwana CUF yetu imerudi. Hapa ngangari, nginja nginja mpaka baharini.... Nilimiss sana upinzani wa hoja na vitendo tumechoka upinzani wa propaganda na mitandao aka nyuma ya keyboard. Sasa ni songa front...mbele kwa mbele...Hongera prof
 
"Hata serikali inakesi mahakani na shughuli sa kiserikali zinaendelea" by magdalena sakaya.
Kwa uwendawazimu wa lipumba na genge lake ,polisi wamebariki mkutuno huo kwa maana ya kupuuza amri ya kimahakama.
Serikali ya magufuli ni kama mbwa anayebweka hana meno .



Sent using Jamii Forums mobile app
Kama serikali inabweka haina meno mbona hamuandamani ,andamana basi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom