Cuf kweli wameonyesha ni kiboko kwa kutetea umma na katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Cuf kweli wameonyesha ni kiboko kwa kutetea umma na katiba

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by oyoyoo, Dec 29, 2010.

 1. o

  oyoyoo Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawapongeza CUF na kuwalaani CDM kwa ukimya wao katika suala hili la Katiba. CUF wamethubutu jambo ambalo ni gumu kufanywa na CDM maana wao wako kimaslahi zaidi. Kama sivyo jitokezeni mniambie kwa nini hamkushiriki maandamano ya jana
   
 2. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,686
  Likes Received: 21,948
  Trophy Points: 280
  Mke anaandaa mgomo dhidi ya mumewe mchana kisha anakuambia tushirikiane mgomo huu,kisha usiku anaingia chumbani na mumewe na huba linaendelea. Utakuwa mjinga kumuunga mkono huyo mke.
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  inasikitisha sana mambo makubwa na muhimu kwa taif letu yanajadikiwa kirahisi kama poyoyoo hapo juu anavyojaribu kuyajadili. kwa upeo mfupi alio nao ingekua chadema wangesema chadema wanamwaga damu, as if Tanzania imejaa wale wanaopanda coaster na kuzunguka kila sehemu which confirm kwamba hawana kazi zaidi ya kuzurura

  Innisikitisha zaidi kuona kwamba poyoyoo na wenzake wameweza hata kupata courage ya kuja JF na kubandika kwani wanajua kuna shallow minded muppets wanaoweza kuwasikiliza

  kibaya zaidi ni kwamba poyoyoo na wanaofanan nae wanaangalia mustakabali wa taifa in such myopic way kiasi cha kujiuliza "hivi tumefanywa wajinga? au ni wajinga genetically?"

  najua poyoyoo anaandika kushusha hadhi ya JF na anaandika akijiandaa kupata matusi ili aathibitishe JF ni uwanja wa matusi... given a chance na hili ni ombi rasmi, dawa ni kudelete kila post au thread za namna hii bila kujali itikadi, dini au malalamiko

  Now to answer Poyoyo post: CUF wamefanya jema kuandamana, ila sina hakika kama that was choreographed or not because wao wamo kwenye serikali ya mseto na hivyo wao ni watawala pia, kingine vilevile cha kuogopa ni kwamba hatujasikia kaumia mtu wala yuko kizuizini.. zaidi ya drama for TV

  Pamoja na yote hayo, tupongeze wote wenye kudai katiba mpya, but we should always ask ourselves, kwenye katiba hiyo tunaomba nini?? anything can look or seem brand new depending on teh manufacturer, seller and customer
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Nawapongeza CUF,CHADEMA na wana harakati wote kwa kuanzisha vugu vugu la kudai kuandikwa kwa katiba mpya Tanzania.Mchakato wa kudai katiba mpya si jambo dogo la kuachiwa chama kimoja au wanaharakati pekee bali ni mchakato utakaofanikiwa kwa kuwashirikisha waTanzania wote bila kujali tofauti za dini au kabila.

  Historia inaonyesha wazi watawala wa kiafrka hawapendi kubadili katika bila kusukumwa na nguvu kubwa ya umma.Vyama vyote vya upinzani vinatakiwa kuunganisha nguvu zao ili kuwa na sauti mmoja kudai katiba mpya Tanzania.Si vyema wala haki kusifia chama fulani kiko mbele kudai katiba kuliko vyama vingine.
   
 5. H

  HADJ DROGBA Member

  #5
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 16, 2009
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poyoyo naona amedandia treni kwa mbele,CUF sasa hivi bandugu siku hizi sio ile ngangari tuliyoizoea siku za nyuma,hivyo basi kila jambo linalofanywa na CUF sasa hivi tuwe tunalitazama mara mbili mbili na sio kukurupuka tu,kila mtu anafahamu sasa hivi kuna suala la mgao wa umeme sambamba na TANESCO ama serikali kutakiwa kuilipa DOWANS mamilioni ya pesa,sasa wasiwasi wangu isije ikawa CUF inatumika kuondoa mawazo ya watanzania kuhusu mgao na malipo ya DOWANS na Kuyapeleka kwenye maandamano ya CUF kudai katiba ambayo wameapa kuilinda na kuitetea! Hili ni angalizo tu bandugu.
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280

  Oyoyoo
  Junior member
  Joining date wed dec 2010
  Posts: 7
  Thanks: 0
  Thanked 0 times in 0 posts
  Rep Power: 0  Maalim seif alikuwepo kwenye hayo maandamano? na je Lipumba alikuwepo kwenye hayo maandamano? kama huna huna jibu la maswali haya chukuwa kopo nenda chooni ukachambe maana inaonekana bado unanuka kinyesi.
   
 7. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  This administration is full of film maker, directors, producers etc!!! Big up great thinker kwenye bold!!!
  Dawa yetu inajulikana, tengeneza drama mbadala kuondoa attention ya machafu yao!!! Nala pop corn tu nikisubiri mwaka....
   
 8. N

  Nancy Tweed Senior Member

  #8
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Angalia historia ya mapinduzi katika Tanzania kisha utapata jawabu la swali lako. Kuna kundi la watu wao ni watu wa "action" na hawa ndiyo watu waliowezesha nchi hii kuwa huru. Na kuna kundi lingine ambalo unaweza kuwaita "educated fools" wao ni watu wa blah blah tuu. Hilo kundi la kwanza la watu wa "action" liko makini sana na ili uweze uwaongoza inabidi wewe iongozi uwe na "substence". Kundi la "educated fools" wao wanataka uwe na cheti tuu, kwa lugha nyingine ni "cerfiticket". Katika maoni yangu haya hili kundi la educated fools kuna kitu watakikosoa kwa sababu ndicho kitu pekee watakachoweza kukiona katika maoni yangu.
   
 9. kagumyamuheto

  kagumyamuheto JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  thread ni nzuri ila mwanzilishi anatakiwa asiwe biased. tunajaribu kuelekeza na kutoa mawazo mbadala wakati mwingine ku-attack upande wa pil ili kurudisha akili zilizopetuka katika mstari.

  Nadhani bado mtoa mada ni mchanga katika JF lakini Big up nathani huko mbeleni utakuwa mpiganaji mzuri.

  KIMSINGI TUMEFANIKIWA NA TUNAENDELEA KUFANIKIWA KURUDISHA FIKRA ZA KIZALENDO AMBAZO KWA BAHATI MBAYA ZIMEINGILIWA NA "SUMU" KUTOKA KWA BAADHI YA VIONGOZI AMA WA SERIKALI NA WA-DINI.

  1.0 ILE DHANA YA KUONA CHADEMA NDIO WAPAMBANAJI PEKEE WA NCHI INAANZA KUPOTEA
  2.0 SUALA LA DHARAU KUTOKA KWA NDUGU ZETU WAKRISTO DHIDI YA UISLAM NA WAISLAM TARATIBU INAPUNGUA
  3.0 SUALA LA KUONA KUWA KILA MMOJA ANA HAKI YA KUCHAGULIWA NA KUFAIDI RASILIMALI ZA NCHI NALO LINAANZA KUZOELEKA
  40. SUALA LA KUFUATA SIASA ZA KIISTAARABU ITACHUKUA MUDA LAKINI WADAU WAMESHAGUNDUA MAKOSA
  5.0 SUALA LA CHADEMA KUPAMBANA NA CUF BADALA YA CCM NDIO TUNAENDELEA KUPAMBANA NALO. VITA NI KUBWA LAKINI USHINDI UPO KARIBU.
  NASHUKURU MODS WAMEKUWA WASTAARABU SIKU HIZI. MWANZONI WALIKUWA WANAFUTA MICHANGO YANGU LAKINI BAADA YA KUGUNDUA ILIVYO NA MANUFAA KWA UMMA WAMEKUWA HAWAZIFUTI. PIA HATA WANA JF WENGI WANAELEWA SANA MICHANGO YANGU NDIO MAANA WENGI WANA-SAPOTI. NI WACHACHE WALIOLISHWA "SUMU HII" MUDA MREFU AMBAO HUJIFANYA KAMA HAWAELEWI NA KUITA UPUPU LAKINI MIOYONI WANAELEWA NA KUKUBALI.

  KWA MFANO VITA YA KIDINI IKITOKEA, YAANI ITABIDI KWANZA "NIWAUE NUSU YA WANAFAMILIA NINAOISHI NAO NA KUWASOMESHA NYUMBANI KWANGU KABLA YA KUTOKA NJE NA KUWAPIGA WAKRISTO WENGINE.

  TUENDELEE KUIJENGA NCHI YETU PAMOJA.
   
 10. o

  oyoyoo Member

  #10
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acid naona itakuwa uminywa kama jina lako lakini kuniita poyoyoo ni kunikosea na nilifahamu utajitokeza kwa aina hii. Ni wazi CUF wameonyesha they have taken the thing on street na sio kusema na kukabidhi bungeni bunge lenyewe limejaa wasanii tu. Sasa kama hujui CUF wanamkuza Mtatiro ndio maana walimuachia shughuli, ninyi CDM mnakuzana humu JF kwa kumchafua Zitto. Angalieni safari hii tunakwenda wote lakini wengine tutaachana njiani. Ukweli unauma kuusikia na hasa ukiwalenga cdm
   
 11. n

  nyantella JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Katiba gani inaandikwa na chama kimoja CUF peke yake halafu watu wanaenda kuandamana si wangesambaza tuone contents kwanza au watoe tuone walichompa mama CK pale wizara ya katiba? wanakataa hii iliyopo kwa sababu iliandikwa na chama kimoja halafu wanaandika ya kwao wanaiita rasimu ya katiba ya URT, nani kaiandika? tusitaniane katiba si document rahisi kuandika hivyo inahitaji sober minds sii za akina Mtatiro!

  By the way wana JF did you hear what Mtatiro said to the journalists? aliwaambia eti "katiba ina ruhusu raia kuandamana wakati wowote!" meaning the current katiba is not that bad afterall!! strange so what exactly were they demonstrating for?

  Ila tusubiri tutaona na kusikia vituko vingi around the katiba mwaka huu, it is the current song for parrots! tusubiri NCCR, TLP, UDP, CCM, CDM, Maaskofu, Masheikh, wahinduu and any tomm and harry who feel like bringing his hodge podge calling it katiba to bring it, tukae tusome zote then we come out with one! Tuache vurugu, we need cool heads to work on this important document.
   
 12. t

  tufikiri Senior Member

  #12
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Umeeleza vizuri, isipokuwa kuna mambo madogo lazima tuwekane sawa. Kwanza kwa kusema Kama Katiba iliyopo inaruhusu maandamano basi haina tatizo. No, hizo ni fikra finyu. Katiba iliyopo sio kwamba vifungu vyote havifai, isipokuwa watu wanataka waifanyie marekebisho makubwa kwa kuiandika upya na sio kuiammend. Pili, Kwa mtazamo wangu, Katiba inatakiwa iwe zao/tunda la wananchi. CUF ni chama cha wananchi, kwa hiyo wananchi kupitia chama chochote au mtu binafsi anayo haki ya kupeleka MAPENDEKEZO YA KATIBA atakayo ona yanafaa. Mchakato wa kutunga Katiba mpya utakapoanza Lazima Tume au kikundi kazi kiundwe kupitia haya maoni ya wananchi ili kuja na Mapendekezo ya Katiba ambayo yanatokana na Wananchi wenyewe kabla ya kupelekwa mbele ya Bunge. Tatizo hapa unachanganya mambo, kuna tofauti kati ya Katiba ile iliyoandikwa na Chama kimoja wakati wa kipindi cha Chama kushika Hatamu, ambapo chama kilikuwa na maamuzi kuliko Bunge. CUF wanachopeleka ni Mapendekezo kama ambavyo mtu yeyoye anaweza kupendekeza. Katika suala la Madai ya Katiba mpya,tunapaswa tusidharau mawazo ya mtu yeyote.
   
 13. N

  Nonda JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Umeleta mada nzuri, lakini ulinganisho wa CUF na CHADEMA haukuwa wa lazima.Umeulazimisha!
  Je lengo ni kuibua malumbano? Kupandisha watu mizuka? Kwa faida gani ? na faida ya nani ?

  Kwa wale wanaosema CUF imo kwenye mseto. Hilo liko Zanzibar na siyo kwenye serikali ya Muungano.
  Kilio hapa, tunadai katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano. Kwa hiyo mimi sioni kwa nini watu wajenge mantiki hii ya Chakaza :-

  « Mke anaandaa mgomo dhidi ya mumewe mchana kisha anakuambia tushirikiane mgomo huu,kisha usiku anaingia chumbani na mumewe na huba linaendelea. Utakuwa mjinga kumuunga mkono huyo mke. »


  Au Chakaza unataka tuamini kuwa CUF ni mshiriki katika Serikali ya Muungano ? Unapindisha ukweli, mkuu.

  Mimi nafikiri kuna haja ya vyama vya upizani kufanya kazi kwa karibu kwa maslahi ya taifa.
   
 14. semmy samson

  semmy samson Member

  #14
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nami naunga mkono sana swala walilolifanya cuf ila nawalaumu kitu kimoja kwanini wafanye wenyewe bila kuwashirikisha vyama vingine vya upinzani? Au wanataka tuwaone wao kama cuf wanauwezo huo pekee yao...

  Nadhani ili hili swala la katiba liwe na nguvu vyama vyote vya upinzani viliwekee mkazo na sio liwe la maslahi ya chama kimoja.,, msije mkawa mnaanza kujipigia kampeni za 2015....
   
Loading...