CUF kwa nini tumefanya vibaya sana katika uchaguzi mdogo wa Igunga

Tatizo hamkupambana na CCM bali mlipambana na CDM
Hiyo na faida ya uasi
Mjifunze siku nyingine akili ziwarudi


Mtatiro mlikwenda Igunga mkijua kwa hakika kuwa mtapata matokeo mliyopata.

Ndio sababu mlipofika Igunga vita yenu ikawa ni Chadema na sio CCM. Kwa hiyo usije unalia lia hapa ili kudhani tapata huruma zetu.

Labda nikuhakikishie jambo moja tu kwamba hivi ndivyo itakavyokuwa hata chaguzi zijazo. Wewe baki tu ukijiridhisha kwa maneno mengi yasiyo na maana. Ile dominance ya kafu kwa siasa za upinzani bara na visiwani imekwisha. Nakuahakikishia hata kule Pemba mmekwisha.

Nashangaa kwa nini hukuzungumzia kwa nini wale wapiga kura wenu wengi wa october 2010 wamewapa kisogo!!!! Najua utabaki na story za ndoa yenu na ccm. Sawa kama ndio sababu huoni kwamba mmekwisha? Mmebaki nyie na ccm kuhubiri udini tu.

Hivi ndivyo NCCR walivyokwisha pia, now your the next. Na wewe utakwisha kisiasa na kafu yako.
 
Huwezi kupata ushindi kwa kuiponda CHADEMA. Kama vyama vikubwa vingeungana CCM ingeanguka mara moja
 
........Poleni kaka!! Nadhani CUF kuna tatizo la msingi,CHADEMA inazidi kuimarika sana wakati CUF mnazidi kuanguka sana...
 
Mimi nilikuiwÀ mfuasi mzuri sana wa cuf miaka ya nyuma lakini nilipoona cuf hawako serious na kumkomboa mtz ilibidi niwahame tu,
Kwa sbb cuf hakuna demokrasia ya kweli mimi toka nasoma primary mpaka leo mwenyekiti ni lipumba na katibu ni maalim seif,
Na kuna ukweli kuwa viongozi wa cuf mnatumiwa na ccm kwa njaa zenu!
Angalia tu hyo ndoa yenu na ccm ndio imewamaliza kabisa nategemea 2015 hata mbunge mmoja bara hamtapata kwa sbb hampo serious na maisha ya mtz mnaleta siasa za ccm za kupakana matope! Hata hivyo hongereni mmerudi nyuma hatua 8,,ccm b oyeeeee
 
usitafute mchawi,cdm kiliunga mkono upinzani kwa lkipindi kirefu now wako juu na waneleweka kwa wananchi hamtaki kuwassuport coz nyie ni wabinafsi,mnapaswa kujiuliza sana,mwanzo wa mafanikio ni kujua chanzo cha tatizo
 
cha msingi CUF vunjeni hiyo ndoa na CCM ndo kitu pekee kitakacho waokoa. vinginevyo hapo mtakuwa mnajaza maji kwenye gunia.
 
Mtatiro

Pole sana, ila mmetutia aibu kubwa sana, CUF mnapata KURA kama UPDP ya Dovutwa na wahuni wezake, kaka angalia sana.

Mimi nakushauri uhame chama hilo halina mjadala kama nia yako ni kufanikiwa kwenye politics nenda chama kingine makini hata kama kitakuwa NCCR Mageuzi ni bora kuliko CUF kwa sasa, CUF ndiyo ishakufa huku bara, haina mvuto na wala haitakaa ifufuke tena ndiyo bye bye...fungasha na jiunge na watu makini wenye nia na moyo dhabiti kwa nchi hii, bila hivyo utaendelea kulia kila siku.
 
Pole, hata hivyo hapo ulipo hapakufao. Una uwezo mkubwa wa kupambana na kufanya mambo ya maana, lakini jukwaa ulosimama bovu hata kama utajidai kukomaa ;kazi bure. Sana sana utazeeka siku si zako.
 
Hongera sana Bw Julius Kwa kuwa mwana demokrasia wa kweli. Mimi nina kufamu tangu UCLAS ulikuwa mpambanaji. Usikate tamaa.
 
Mdogo wangu Mtatiro,Kwanza hongera sana,nadhani ninachokiamini kwako tangu ulipokuwa mlimani bado kipo ingawa kimebaki kidogo kitakwaisha na unakimaliza mwenyewe.

Mimi nimekuwa nikikufuatilia sana tangu ulipokuwa UDSM, misukosuko ya migomo ulivyokuwa unakabiliana nayo na nakumbuka ulikuwa kiongozi ktk serikali ya wanafunzi, mm nilikuwa nasaga lami tu lakini niliamini iko siku utapigania nchi yako, kosa ulilolifanya ni ku-join chama mapema, sidhani kam ulikuwa umeshafanya tafiti nzuri ku-identify the right political party to join,anyway you still have the chance,and put in your mind that you can not change the past but the future.

Huko Igunga ki ukweli hata mimi nimeshangaa,kuambulia kura 1,2,4 na hata 0 ni kitu kisichoingia akilini,na to be honest it is bad impression,jaribu kutumia elimu yako vizuri,kwa hali ya nchi yetu ilipo leo na kwa siasa za kuponda vyama vya upinzani mbele ya watanzania walio jaa makovu ya hali mbaya ya maisha kwa kila kitu,ni hatari kwenu kukiponda chama cha upinzani live,wananchi hawatakueleweni hata kidogo,na mbaya zaidi mnaponda chama ambacho kwa uelewa wa kawaida tu usiohitaji hata diploma kinaonyesha wazi kiko kwa maslahi ya wanyonge,na kitendo cha kuwa kitu kimoja na CCM-Magamba ambayo leo yametufikisha hapa tulipo ndipo umaaruf wenu unapotea siku hadi siku.

Kaeni chini mkubali mabadiliko ya kweli, ila kwako wewe nilivyokuwa nakufuatilia tangu chuo,bado nina imani kwamba you have the spirit of uzalendo,ila ku-uishi huo uzalendo ndani ya chama chenye ndoa na CCM na viongozi wako wa juu walilridhia na sehemu ya chama chako ambako kina nguvu ni ZN,itakuwia vigumu sana kutoka,maana ukijaribu kufurukuta utazimwa tu,kama kweli unajutia matokeo yanayoendelea kutangazwa,you have to think twice Mtatiro.

For sure CUF imepoteza mwelekeo na sidhani kama mtaki-reform,sijui mta-deploy strategy ipi,kwani kila mtakapotaka kuwa seriousl against na Magamba/mme wa CUF mtaishia kugombana,na mwisho wa siku wanatembea kwa ving'ola ili tuwapishe njia wapite hawatakubali,angalia juzi juzi bungeni mlivyinisononesha mlivyoinga mkono hoja iliyoletwa na CCM kuhusu kambi rasmi ya upinzani,hilo nalo liliwatoa maksi.

Kingine ukitaka kupata approach ya CUF kwa wananchi usisubiri kuletewa mezani assesment report kaa vijiweni na uswazi ambako mabomu ya nchi hii yaliko,na yanatengenezwa na ccm-magamba/mafisadi,hivyo siku walala hoi wakisema enough is enough hapo ndo utakuja jutia kile mnachokifanya kwa mgongo wa kujifanya nayi ni wapinzani,ni kweli hata huko vijiini watu wanajua ninyi ni B ya CCM.

Mmeshindana lakini hamtashinda.

Nimalize tu kwa kukuomba utupe hali halisi ya mchuano kati ya magamba na Chadema,ki ukweli wengineo hatutalala kama hatutasikia matokeo,kwani tunajua makamanda wetu huko wanapiganisha lakini tuashaka na uchakachuaji.

Ushauri:
H
amasisha wana CUF wasaidie kulinda kura zisichakachuliwe huko Igunga utapata abruplty positive respond kwa wananchi, tena simama imara usaidie kusiwepo na hujuma,jikaze kiume,najua uko dissapointed lakini nimekupa siri ya kurudisha ghafla imani ya wanachi kwa CUF.

Lastly hongera kwa ujasiri wa kutuhabarisha na kutamka wazi yaliyowakuta Igunga.
 
Anguko lenu limeanzia mlipokubali kuingia mseto na CCM, hata baada ya kuambiwa kuwa itawagharimu lakn hamkusikia. Pia wanamseto wenu wanatumia mseto kuwadhohofisha.

Fuatilia hotuba za Nape juu ya Seif. Hata nyinyi mmepiga propaganda nyingi sana dhidi ya chadema na hivyo kukiacha chadema kuwa chama pekee chenye hoja za kipinzani. Kaeni na mtafute ushauri wa kuendesha chama chenu, la sivyo endeleeni kula posho hadi hapo mtakapokosa hata mbuge mmoja.
 
Daah! IGUNGa kiboko, yaan jamaa kunavituo hata kura 1 hawana, nying sana ni 4, 7, mpaka 11, hiyo ni fedheha! Inasikitisha, kwa nguvu alizotumia, Hamad na mtata, na nikiangalia attendance ya watu kwenye mikutano yao. Kumbe cuf hawana tofauti na vile vya vingine Updp, sau, n.k kwi kwi! Naingia zangu mwitu!
 
Umesema maneno mazuri ya kishujaa ingawa hayaja kamilika. Kama mwanasiasa tena kijana wa kizazi hiki huwezi kupewa jukumu kubwa hivi la kiongozi na kuongoza chama chako katika kushindwa huku kuliko tukuka halafu usijiuzulu. Nasema haiwezekani, ungetakiwa useme pamajo na maneno yako mazuri kuwa unajiuzulu na kuawapa nafasi wezako wenye uwezo zaidi kukiongoza chama na wewe ukabakia mwanchama muaminifu tu.
 
oh KAFU tafuteni jina lingine huku bara. Joto ya Jiwe mnaanza kuionja. mwisho mtabaki kuhamia CCM kwa mume wenu!
 
Pamoja na kukiri kushindwa nakushauri hama hicho chama before its too late. CUF waachie kina Jussa na Hamad wewe sio type yao.
 
Mtatiro huo ndio ukomavu ambao unatakiwa wa kisiasa, ila mafanikio ya cuf hayatatokea kamwe kwa muafaka huo mlioufanya,roho za watu zilizolia juu ya cuf mwaka 2001 itaendelea kuwalilia. Na ccm inachukua jambo hilo mtaji wao mkubwa na kuendelea kutimiza malengo yao kwa kuwafunika macho na pazia la muafaka.

Hamad Rashid naye akajitokeza kuipinga chadema kwa nguvu zake zote, wananchi wa tz wanaona wana macho, wanaufahamu. Badala ya ninyi (cuf) kuungana na chadema na vyama vingine, mmekuwa wapinzania wakuu wa chadema kuliko ccm. Hapo mnavua mlichopanda.

Hata kama wewe huenda na nia njema ya kutaka kuisaidia cuf kwa mwelekeo huo si muda mrefu ujana unakimbia sana, na utapoteza nguvu ya kutaka kuwatumikia wananchi. Fanya maamuzi sahihi!!!!!!!!!!!!!!!
 
Naomba uwe wa kwanza kuandaa mchakato wa kuungana kwa vyama vya upinzani Tanzania ili mwaka 2015 muingoe magamba, na pia itakuwa anjia nzuri ya kugawana wabunge kimajimbo na kuwanadi kwa kushirikiana ili bunge lijalo liwe na spika mpinzani hoja zitakuwa na nguvu na
mkakubaliana kuunda serikali ya pamoja, ndo mwanzo wa maendeleo.

Lakini hili la kung'ang'ana kila mtu kivyake mnatoa fursa kwa CCM kuzidi kuwaibia kura. Kazi kwako sasa, nakutuma uwe mtume wa hili.

Mmeona alivofanya rais mpya wa Zambia, Kenya nk. Karne hii bila serikali ya mseto hatutafika, angalia USA, uk na nchi kadha wa kadha igeni kwao.
 
Back
Top Bottom