CUF: Kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa na kukosekana kwa uchaguzi huru na wa haki ni sababu ya wananchi kudorora katika kujiandikisha kupiga kura

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Mkurugenzi Mipango na Uchaguzi wa Chama cha


Dar es Salaam. Chama cha Wananchi (CUF) nchini Tanzania kimesema baada ya kufanya utafiti katika mikoa nane kwenye shughuli ya uandikishaji wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa tangu lilipoanza Oktoba 8, 2019 wamebaini sababu nne za shughuli hiyo kudorora.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Oktoba 14, 2019, Mkurugenzi Mipango na Uchaguzi wa CUF, Mneke Jaffar amesema sababu ya kwanza ni kutofanyika kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa tofauti na chaguzi za mwaka 2004, 2009 na 2014 ambayo ilihamasisha wananchi kujiandikisha na kujua umuhimu wa kufanya hivyo katika uchaguzi.

"Kwa muda mrefu sasa ni Chama cha Mapinduzi peke yake kimekuwa kikifanya mikutano huku vyama vya upinzani vikizuiwa kwa sababu mbalimbali," amesema Jaffar.

Jaffar amedai sababu ya pili ni kufanyika kwa uchaguzi usio huru na haki ambapo wamedai matokeo yanakuwa tofauti na yale waliyotarajia katika chaguzi za marudio.

Jaffar ametaja sababu nyingine ni kupatikana kwa washindi wanaopita bila kupingwa katika chaguzi za marudio na nne ni viongozi waliochaguliwa kuhama vyama vya upinzani na kwenda CCM na kutokuwepo vitambulisho ambavyo vitawasaidia wananchi kwa matumizi ya baadaye.

Chama hicho kwa sasa viongozi wake wakuu wapo katika ziara ya kichama kanda ya ziwa kimetaja mambo manne ambayo yatafanya idadi ya waandikishaji kuongezeka katika siku tatu zilioongezwa na Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo.

Jaffari ameiomba Serikali kutamka vyama vya siasa kuwa huru kisheria kufanya mikutano ya hadhara leo Oktoba 14, 2019 ili wananchi wahamasike kujiandikisha.

"Ni muhimu Serikali itoe tamko mapema ikiwezekana hata leo ili hawa waandikishaji wapate watu wa kuwaandikisha," amesema Jaffar.

CUF imetaka pia Serikali kuwahakikishia wananchi kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki kwa kudhibiti vitendo vya uvunjifu wa demokrasia.

Jaffar ameiomba Serikali kupitia Tamisemi kuzuia kile CUF ilichodai waandikishaji kutoka vituoni kwenda majumbani kuandikisha watu.

CUF pia imelitaka jeshi la polisi kufanya haki kwa kusimamia pande zote kwa usawa kwenye uchaguzi utakaofanyika Novemba 24,2019 nchi nzima.

"Katika kumbukizi ya miaka 20 ya Mwalimu Julius Nyerere, tunaitaka Serikali kuyaenzi na kuyatenda yale mazuri ambayo aliyafanya enzi za uhai wake," amesema Jaffar
 
CUF ya Lipumba ni tawi la chama tawala.

It’s so obvious now watu hawataki au hawaoni sababu ya kujiandikisha kwa kuwa wanajua matokeo yashapangwa.

Rais kishawalaumu na kuwatisha Wananchi wa maeneo yaliyochagua upinzani.

Serikali imewashughukikia na kuwa Unga jela Wapinzani.

Viongozi wa Serikali na chama tawala wanesikika wazi wazi wakipiga mkwala kwa wale Watakaowatngaza Wapinzani kushinda. Mkulu mwenyewe alitoa huu mkwala hadharani.

Kwa hayo Macha he kweli kuna haja ya kwenda kupiga jua au mvua kwa ajili ya uchaguzi!? Watanzania siyo wote wajinga. Wapinzani wawasikilize na kuwaunga mkono Wananchi.
 
Duh! Noma sana huu uchaguzi ujue,wajiangalie sana hao viongozi wanaopenda kupiga mikwara,ukiona mtu anapiga mikwara ujue ni mwoga.
Nalog off
 
KUNA SABABU MOJA KUBWA NA YA MSINGI INAKWEPA KUTAJWA" NIKUTEUWE MM,NKUPE GARI,MAFUTA,NYUMA,NIKULIPE MSHAHARA ALAFU UMTANGAZE MPINZANI HAKUNA NEUTRAL HAPO"
 
Back
Top Bottom