CUF kuunguruma Zanzibar kesho.

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Inasemwa asie mwana abebe japo jiwe,kesho katika uwanja wa Kibanda uhai au kibanda maiti kama kilivyokuwa kikijulikana hapo zamani kutafanyika mkutano mkubwa wa aina yake ,waandalizi wa mkutano huo wametabiri kuwa utakuwa ni mkutano mkubwa ambao haujawahi kufanyika hapa Zanzibar au Tanganyika.
Ni mkutano ambao utawakusanya raia wa visiwa viwili vinavyoijenga Zanzibar na kuto joto lao lupitia Chama hicho cha CUF.
Mada kubwa itakayozungumzwa ni kufundishwa siasa kwa Kikwete na kuelimishwa kwa ufasaha kuhusu Zanzibar.maelfu ya wananchi wameapa kujitokeza katika mkutano huo na kusema ni mkutano ambao umekuja kwa wakati muafaka na wanaenda kusikiliza kilichomtoa kanga manyoya,kitu ambacho kimekuwa kikitolewa na kusemwa na watu kama msemo lakini kesho viongozi wa CUF watakifafanua na kujulikana hicho kilichomtoa kanga manyoya ni kipi ? Tega sikio na ili upate kisa kamili kutoka mkutanoni. Nyote mwaalikwa japo kiroho.
 
Ni mkutano ambao utawakusanya raia wa visiwa viwili vinavyoijenga Zanzibar na kuto joto lao lupitia Chama hicho cha CUF.Mada kubwa itakayozungumzwa ni kufundishwa siasa kwa Kikwete na kuelimishwa kwa ufasaha kuhusu Zanzibar.maelfu ya wananchi wameapa kujitokeza katika mkutano huo na kusema ni mkutano ambao umekuja kwa wakati muafaka na wanaenda kusikiliza kilichomtoa kanga manyoya,kitu ambacho kimekuwa kikitolewa na kusemwa na watu kama msemo lakini kesho viongozi wa CUF watakifafanua na kujulikana hicho kilichomtoa kanga manyoya ni kipi ? Tega sikio na ili upate kisa kamili kutoka mkutanoni. Nyote mwaalikwa japo kiroho.
Bwana Mwiba kama huo Mkutano kweli unaweza kukusanya wananchi wa Visiwa Viwili-hongera. Lakini unayoeleza katika mkutano huo yawe na maslahi kwa wananchiwa visiwa vyote viwili. Unayaweza hayo?
 
Inasemwa asie mwana abebe japo jiwe,kesho katika uwanja wa Kibanda uhai au kibanda maiti kama kilivyokuwa kikijulikana hapo zamani kutafanyika mkutano mkubwa wa aina yake ,waandalizi wa mkutano huo wametabiri kuwa utakuwa ni mkutano mkubwa ambao haujawahi kufanyika hapa Zanzibar au Tanganyika.
Ni mkutano ambao utawakusanya raia wa visiwa viwili vinavyoijenga Zanzibar na kuto joto lao lupitia Chama hicho cha CUF.
Mada kubwa itakayozungumzwa ni kufundishwa siasa kwa Kikwete na kuelimishwa kwa ufasaha kuhusu Zanzibar.maelfu ya wananchi wameapa kujitokeza katika mkutano huo na kusema ni mkutano ambao umekuja kwa wakati muafaka na wanaenda kusikiliza kilichomtoa kanga manyoya,kitu ambacho kimekuwa kikitolewa na kusemwa na watu kama msemo lakini kesho viongozi wa CUF watakifafanua na kujulikana hicho kilichomtoa kanga manyoya ni kipi ? Tega sikio na ili upate kisa kamili kutoka mkutanoni. Nyote mwaalikwa japo kiroho.
Safi sana kwa walevi wa Tende... Kama huwajui walevi wa tende aka gongo wacheki hapa wamejaa tele...
 
Bwana Mwiba kama huo Mkutano kweli unaweza kukusanya wananchi wa Visiwa Viwili-hongera. Lakini unayoeleza katika mkutano huo yawe na maslahi kwa wananchiwa visiwa vyote viwili. Unayaweza hayo?

Pakacha ni dhahir jina limekusibu !! kwani siku zote unapoambiwa ni lazima na wewe mwenyewe ujiambie (kiswahili fasaha hicho)
 
Mwiba mkutano umekwisha? Lete saa habari za mkutano wa hicho chama chenu cha Zanzibar
 
Mwiba mkutano umekwisha? Lete saa habari za mkutano wa hicho chama chenu cha Zanzibar
Kikwete kaambiwa akome tena imerudiwa mara tatu na ikaongezewa kuwa mambo yake hukohuko bara au T/Bara,fitna zake na uchonganishi wake hauna nafasi tena jamaa wameshasitukia habari za wagawe uwatawale tena kama haitoshi amepewa jibu la papo kwa papo kuwa na kama ataenda kutesa na aende na wao wanamsubiri.

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuacha kutamka maneno ya kuwagawa Wazanzibari kwa vile hawagawanyiki.

Vile vile amesema kutokana na kauli hizo za Kikwete wanachama wa chama chake wataingia katika uchaguzi mkuu wa mwaka kesho, wakiwa wamejitayarisha kupambana na mazingira yoyote yatakayojitokeza.

Kiongozi huyo aliyewania urais wa Zanzibar mara tatu bila mafanikio, alikuwa anazungumzia kauli ya Kikwete akiwa ziarani kisiwani Pemba kuwa, wapinzani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) itawachukua muda mrefu kupata nafasi ya kuongoza nchi hiyo au wanaweza wasiipate kabisa.

Rais Kikwete alisema, "Tutamwendeleza kila mtu kwa sababu dhamana ya maendeleo ni yetu katika serikali. Hawa wengine hawana serikali. Kazi ya wabunge wao na wawakilishi wao ni kufoka tu. Sisi ndio wenye dhamana ya serikali na wala hatubagui."

Jana akihutubia mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Kibandamaiti Mkoa wa Mjini Magharibi, Maalim Seif alisema kauli hiyo ni ya kuwagawa Wazanzibari wote hata wa Chama Cha Mapinduzi visiwani humo, ambao mwaka 2000 walimchagua Dk Gharib Bilali, lakini chama hicho kilipoketi Dodoma kikawaletea Amani Karume ambaye alikuwa ameshika nafasi ya tisa.

Alisema kwamba viongozi wa CCM Tanzania Bara wamekuwa na utamaduni wa kuwagawa Wazanzibari kwa malengo ya kurudisha nyuma maendeleo ya Zanzibar na kuididimiza kisiasa na kiuchumi.

"Viongozi wa Tanzania Bara wapo katika mkakati wa Mwalimu Julius Nyerere wa kuitokomeza Zanzibar, tunamwambia Kikwete kachelewa Wazanzibari hatugawiki tena ng'o tena namwambia akome akome akome kutuletea fitna katika nchi yetu, afanye chokochoko huko huko bara," alisema Maalim Seif huku akishangiliwa na umati wa watu waliohudhuria mkutano huo.

Alisema kwamba, Wazanzibari hawapo tayari kuona umoja wa kitaifa ukivurugwa kwa kisingizio cha mapinduzi, kwa vile mapinduzi ya Zanzibar yalifanikishwa na Wazanzibari wenyewe na ndio wanaopaswa kuyalinda na sio yeye Kikwete.

Hamad alisema kauli zilizotolewa na Rais Kikwete wakati wa ziara yake Zanzibar haziashirii kuwepo uchaguzi huru na wa haki Zanzibar, kwa vile wapinzani wasitarajie kukamata madaraka ya dola na wengine wataishia kutafuta nafasi hiyo hadi mwisho wa maisha yao.
Alisema CUF imejifunza mambo mengi tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, baada ya kuvurugwa kwa uchaguzi mwaka 1995, 2000 na 2005 na sasa umekuwa ni utamaduni wa kudumu wa CCM.

Alisema Wazanzibari hivi sasa wanaishi katika lindi la umasikini na viongozi waliopo madarakani kazi yao kubwa ni kukusanya mapato ya serikali na kutumia kwa maslahi yao binafsi, huku wakiacha wananchi wakiteseka.

Alisema hivi sasa Zanzibar wananchi wanakabiliwa na tatizo kubwa la ufisadi wa ardhi, lakini Rais Kikwete ameshindwa kukemea vitendo hivyo licha ya kuwa ni tatizo kubwa hivi sasa kwa Unguja na Pemba.

"Wazanzibari wamepokea ujumbe wake, lakini tunaamini anataka mikono yake iwe na damu kama Rais Mkapa alivyoondoka na damu mikononi, lakini Wazanzibari tunakusubiri njoo, tulikuamini kwa kauli yako ya kushughulikia mpasuko wa kisiasa, lakini sasa tumekufahamu tunakwambia njoo," alirudia kusema Maalim Seif huku akishangiliwa.

Akihutubia katika mkutano huo mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba alisema CUF imesikitishwa na kauli ya Rais Kikwete kwa vile inakwenda kinyume na ahadi yake ya kumaliza mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar.

Alisema kwamba, tangu mapema alijenga wasiwasi na uwezo wa utendaji wa Rais Kikwete na kumbatiza jina la msanii na alipata matumaini mapya baada ya hotuba yake ya kwanza kuahidi kushughulikia matatizo ya Zanzibar.

Lipumba alisema katika mikutano mitatu ya Rais Kikwete na mabalozi aliyoifanya kuanzia 2006 hadi 2008, alikuwa akiwaeleza kuwa ameshafikia hatua nzuri katika kushughulikia mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar kitendo ambacho ni kinyume na kauli zake.
"Tunamshukuru Kikwete kwa kuweka mambo wazi kwa vile sasa katudanganya basi tena, kwa vile wanasema wao ndio wanaoamua na rais atateuliwa na yeye nashukuru ametupa muda wa kuweza kujipanga, tena kujipanga kweli kweli, tumechoka na bakora za CCM," alisema mwenyekiti huyo huku akishangiliwa.

Aliwataka vijana, wanawake na wazee kujipanga kukabiliana na vitendo vyovyote vinavyozorotesha demokrasia kwa kuanzia na uchaguzi mdogo wa uwakilishi unaotarajiwa kufanyika Mei 23 katika Jimbo la Magogoni .

Mkutano huo ulitawaliwa na vilio vya wanawake kwa vile ulibeba ujumbe wa kuwakumbuka wanachama wa CUF waliouawa Januari 26 na 27 mwaka 2001, hali iliyofanya baadhi ya wanawake kumwaga machozi baada ya kusomewa utenzi kukumbusha majina ya watu waliokufa katika vurugu hizo.
 
Wazanzibari bwana we! si huyu huyu mnamtegemea kuwaletea mwafaka? sasa mwamwambia akome X3? Sasa mlitegemea nini?
My final word hakuna mwana Sisi M atakayewaletea mwafaka. Ila ni nyinyi wazanzibari wenyewe. Amkeni chukueni hatua jikomboeni katika sanduku la kura basi! Tena lindeni sanduku kwa kila namna. Narudia kwa kila namna. Domokrasia ina gharama wandugu wangu. Ila haya yote yafanyeni kwa upendo na ushirikiano maana adui yenu mwamjua.
 
Ni kweli ina gharama ndio ukaona Pemba wameondoka na viti vyote ,hivyo Kikwete kawaita walevi wa tende,sasa na huko Tanganyika nanyi wacheni kutumia mapuya tafuteni ile yenyewe sijui inaitwa Chang'aa ili mpate kupambana na hao mamluki wa kipolisi wanaotumwa na CCM.Pemba wamewachinja polisi kama kuku wa kideri yote ni kwa ulevi wa tende.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom