Membensamba
Senior Member
- Nov 4, 2010
- 157
- 10
Chadema kikifanya makosa ya kujiunga na cuf nitakuwa kimeua kambi ya upinzani bungeni. Mwenendo wa madai ya cuf na kauli za Hamadi pamoja na hali halisi ya muafaka baina ya ccm na cuf unanipa kuona yafuatayo.
1. Cuf kama wabia na ccm huko Zanzibar wamepoteza ile status ya kuwa wapinzani wa kweli wa ccm, kwani sasa ni watawala pamoja. Kuindoa ccm madarakani Zanzibar ni kuiondoa pia cuf, kwa kuwa chama kingine hakina muafaka wa kutawala pamoja na cuf. Kwa hiyo ni lazima cuf walinde maslahi ya ccm kwa kujua kuwa kwa kufanya hivyo wanalinda pia maslahi yao. Mtakumbuka jinsi Maalim Seif ilivyogeuka ghafla baada ya muafaka kumpigia debe Karume atawale tena? Kama aliweza kumpigia debe kiongozi wa ccm kubaki madarakani hata kinyume na katiba, hiyo inaashiria nini? Angalia jinsi ccm walivyompigia kura mbunge wa cuf kushika nafasi huko sadek, nayo inaashiria nini?
2. Kauli za Hamadi juu ya yale waliyoongea sirini na Mbowe ni mashambulio ya makusudi kwa chadema, na ni udhihirisho kuwa wahatatunza siri za kambi ya upinzani wakiwa meza moja. Kama anaweza kubwata namna hiyo hadharani, ni neno dogo kwake kuropoka kwa wabia wake ccm mambo ya ndani ya kambi?
3. Cuf wanadai kuungana na chadema kama vile ni haki yao, wakati chadema hakilazimiki kuunda alliance na chama chochote kwa kuwa kimetimiza masharti ya kanuni za bunge za kuunda upinzani. Ni nia gani waliyo nayo cuf kulazimisha ushirikiano?
Kutokana na hayo, ni dhahiri kuwa kama chadema wakifanya makosa ya kuungana na hawa jamaa hakutakuwa na kambi imara. Kambi ni kambi tu ikiwa wahusika wote mnaimba wimbo mmoja. Lakini kama huyu anasema hivi na mwenzake anampinga au anatoa siri kwa "adui" hiyo siyo kambi. Nani atakubali ndugu wa mshataki wake awe wakili wa kumtetea mahakamani? Chadema kutokuungana na cuf sio vyema tu, ila ni MUHIMU. Ikumbukwe kuwa Zanzibar sasa hakuna tena chama kikuu cha upinzani.