Cuf kutoa tamko kesho kuhusu kukamatwa kwa shekh ponda!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Cuf kutoa tamko kesho kuhusu kukamatwa kwa shekh ponda!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kigu, Oct 20, 2012.

 1. k

  kigu Senior Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuna tetesi kesho CUF watatoa tamko kuhusu kukamatwa kwa shekh ponda, ktk mkutano wa Buguruni,.........na kutoa njia ya ufumbuzi wa tatizo.
   
 2. T

  Top Cat Member

  #2
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 97
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ufumbuzi ni CUF kuacha siasa za misikitini la sivyo chama kitaendelea kubakia Buguruni na Lindi wakati vingine vinaenea Tz nzima
   
 3. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  watakemea vitu vichache bila kushambulia motive behind, then watasuggests mazungumzo.Hii dalili kuwa wanataka wa elevate hawa magaidi kwenda ktk level ya wanamapinduzi safi.Halafu wakirudi watakwenda pongezana kuwa wameweka vizuri ili mkafir wasishtukie issue.Ila Mungu mkubwa hawana skills za kufanya vitu sawasawa kama walivyofanya Jangwani kwa kumuweka muislam awe mchungaji.What a disgust?
   
 4. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Ahaaaa! Wameona chadema wametoa tamko na wameamua kukopi na paste kila kitu utaona ilo tangazo kama litakuwa tofauti na lile la chadema.........majamaa yanajua kukopi na kupesti yatabadilisha heading tu content ile ile ya chadema
   
 5. k

  kigu Senior Member

  #5
  Oct 20, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mbona chadema Lindi, buguruni haipo au na wao wana siasa za makanisani?
   
 6. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,764
  Trophy Points: 280
  hawa ni wazee wa kucopy na na kupaste wanasubiri wengine waanze.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 7. A

  Albimany JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Nyote munaumwa muliotchangia mada hii,

  Mbona tokea juzi CUF walishatoa tamkio au hamusomi habari hadi ziwe na neno CDM?
   
 8. A

  Albimany JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  NA hili lilikua nini?

  Chama cha Wananchi CUF kinasikitishwa na matukio ambayo hayakutarajiwa kutokea hapa Zanzibar yaliyoanza kujitokeza jana tarehe 17/10/2012 ambayo yamesababisha vurugu kubwa katika Manispaa ya Zanzibar na vitongoji vyake.

  Matukio hayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa mali za Umma, wananchi mmoja mmoja na hata vyama vya siasa. Miongoni mwa vitendo hivyo ni kuvunjwa Maduka, vyombo vya usafiri, kukatwa miti ovyo na nguzo za umeme, pamoja na kuchomwa moto maskani za CCM. Matukio mengine ya kusikitisha na kuhuzunisha kufuatia vurugu hizo ni kuwepo taarifa za kuuwawa kwa Askari Polisi.

  Kutokana na vitendo hivyo, Chama Cha wananchi CUF kinaalaani kwa nguvu zote matukio hayo ambayo yamepelekea uvunjifu wa mkubwa wa amani ya nchi, na kusababisha hofu kubwa kwa raia pamoja na wageni wanaotembelea Zanzibar.

  Sambamba na vurugu hizo, Chama Cha Wananchi CUF kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyotolewa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed iliyoeleza juu ya kutoweka kwa Sheikh Farid Hadi Ahmed katika mazingira ya kutatanisha.

  Katika Taarifa hiyo, Serikali imethibitisha kuwa vyombo vyake vyote vya ulinzi havijamkamata Sheikh Farid, jambo ambalo limezidisha hofu na wasi wasi kwa wananchi juu ya mahali alipo na hali yake kiongozi huyo wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar.

  Chama cha Wananchi CUF kinaiomba Serikali kuendeleza juhudi zote za kuhakikisha taarifa za ukweli na za uhakika zinapatikana juu ya kadhia ya kutoweka kwa Sheikh huyo kwani Sheikh Farid ni raia wa nchi hii, na Serikali hii ni kwajili ya wananchi wote, ili kuondoa hofu na wasi wasi ambao umesababisha baadhi ya wananchi kujengwa na dhana mbaya.

  Aidha, Chama cha wananchi CUF kinawataka wanachama wake, wapenzi na wananchi wote kwa ujumla kutojiingiza na kutofanya vitendo vyovyote vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani ya nchi yetu.

  Sote kwa pamoja tukatae kabisa kujihusisha na vitendo vya kuleta vurugu kwa vitendo na kauli zitakazopelekea kuiondolea sifa njema nchi hii ya Zanzibar ambayo imejijengea duniani kote.

  Haki sawa kwa Wote

  ………………………..
  Salim Biman
  Kaimu Naibu katibu Mkuu Zanzibar
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Naona hili tamko linawalenga wazanzibar, labda mniwekee kwa rangi ni wapi limewataja akina ponda na waathirika wa vurugu za dar es salaam, najituma kuamini kuwa kafu bara bado kutoa tamuko.
   
 10. k

  kigu Senior Member

  #10
  Oct 20, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [

  Chama cha Wananchi CUF kinasikitishwa na matukio ambayo hayakutarajiwa kutokea hapa Zanzibar yaliyoanza kujitokeza jana tarehe 17/10/2012 ambayo yamesababisha vurugu kubwa katika Manispaa ya Zanzibar na vitongoji vyake.

  Matukio hayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa mali za Umma, wananchi mmoja mmoja na hata vyama vya siasa. Miongoni mwa vitendo hivyo ni kuvunjwa Maduka, vyombo vya usafiri, kukatwa miti ovyo na nguzo za umeme, pamoja na kuchomwa moto maskani za CCM. Matukio mengine ya kusikitisha na kuhuzunisha kufuatia vurugu hizo ni kuwepo taarifa za kuuwawa kwa Askari Polisi.

  Kutokana na vitendo hivyo, Chama Cha wananchi CUF kinaalaani kwa nguvu zote matukio hayo ambayo yamepelekea uvunjifu wa mkubwa wa amani ya nchi, na kusababisha hofu kubwa kwa raia pamoja na wageni wanaotembelea Zanzibar.

  Sambamba na vurugu hizo, Chama Cha Wananchi CUF kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyotolewa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed iliyoeleza juu ya kutoweka kwa Sheikh Farid Hadi Ahmed katika mazingira ya kutatanisha.

  Katika Taarifa hiyo, Serikali imethibitisha kuwa vyombo vyake vyote vya ulinzi havijamkamata Sheikh Farid, jambo ambalo limezidisha hofu na wasi wasi kwa wananchi juu ya mahali alipo na hali yake kiongozi huyo wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar.

  Chama cha Wananchi CUF kinaiomba Serikali kuendeleza juhudi zote za kuhakikisha taarifa za ukweli na za uhakika zinapatikana juu ya kadhia ya kutoweka kwa Sheikh huyo kwani Sheikh Farid ni raia wa nchi hii, na Serikali hii ni kwajili ya wananchi wote, ili kuondoa hofu na wasi wasi ambao umesababisha baadhi ya wananchi kujengwa na dhana mbaya.

  Aidha, Chama cha wananchi CUF kinawataka wanachama wake, wapenzi na wananchi wote kwa ujumla kutojiingiza na kutofanya vitendo vyovyote vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani ya nchi yetu.

  Sote kwa pamoja tukatae kabisa kujihusisha na vitendo vya kuleta vurugu kwa vitendo na kauli zitakazopelekea kuiondolea sifa njema nchi hii ya Zanzibar ambayo imejijengea duniani kote.

  Haki sawa kwa Wote

  ………………………..
  Salim Biman
  Kaimu Naibu katibu Mkuu Zanzibar ]


  hilo ni tamko kuhusu kutekwa shekh farid Zanziba na wala sio kuhusu shekh Ponda Dar, hata ukisoma huilewi we wawapi?
   
 11. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  watoe tamko kama chama au kama serikali...wananichanganya na hawa watu
   
 12. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  Cuf MNAWEZA KUSOMA HII NAYO KUWEKA MSIMAMO JUU YA BAKWATA NA KUMTAKA KIKWETE ALIVUNJE
   
 13. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  Bakwata ni chombo kinachotambuliwa rasmi na serikali kama wasemaji wakuu wa waislam Tanzania. Unaelewa waislam wapo madhehebu mengi lakini hawana uwakilishi katika Bakwata, Uongozi wake mara nyingi unakuwa watu wachache na wasio kuwa na sifa hili linalifanya Bakwata likose sifa ya kuwa msemaji wa waislam pia Utendaji wake umekuwa ukipigiwa kelele na waislam miaka nenda miaka rudi lakini mara nyingi wameshindwa kwa vile serikali imekuwa ina wa kingia kifua.
  Hali hio imepelekea Bakwata kutokuwa na support yoyote kutoka kwa waislam Tanzania.Na athari zake ndio hizi inapotekea matatizo kama haya serikali inamleta shehe wa Bakwata kutuliza watu lakini ukweli hakuna anaemsikiliza.hivyo kuna ombwe kubwa baina ya serikali na waislam wa nchii Jambo ambalo sio jema likaachwa kuendelea

  NINI CHA KUFANYA ?
  Napenda kutoa ushauri kwa Rais Kikwete kutumia busara na kulivunja BAKWATA mara moja.Naelewa hili si suala la serikali lakini ushahidi upo kwamba nyerere aliivunja jumuiya iliyokuwepo kabla ya Bakwata"kwa lengo la kuwapa waafrika uongozi wao wenyewe wa kiislam na kuleta maendeleo" lakini lengo hilo halikufikiwa.
  Pia ni vyema kwa serikali kuwa na uhusiano na jumuiya ambayo inasikilizwa na wanajumuiya,ukweli sasa hivi Bakwata haina ushawishi wowote kwa waislam.Inapotokea matatizo kama haya Serikali ili kutuliza jazba na fujo inahitaji kuwa na ushirikiano na chombo kinacho kubalika ambapo akisimama kiongozi wao atasikilizwa.
  Tumeona kamanda Kova na MKuu wa mkoa mara 2 ndani ya TV wakiwa na mkuu wa Bakwata wa Dar es salaam, sheikh Hadi lakini waislam hawa kumsikiliza kwani kwa wasilam sasa hivi Bakwata ni kama majizi tu na hawana faida yoyote kwa maendeleo yao.
  Utaona bakwata wali rithishwa mali zote ya iliyokuwa jumuia ya waislam enzi hizo kazi yao kubwa ni kuziuza hizo mali na viwanja.
  Bakwata tangia wakati huo hawakuweza kuleta maendeleo yoyote kwa waislam si katika elimu , afya na maendelo ya uchumi, hawana dira ni kichaka cha wachache kinacho hujumu mali za waislam

  Ana chotaka kufanya Nchimbi ni muhimu sana,serikali inatakiwa lazima iwe na uhusuano mzuri na makundi ya jamii ikiwa ni dini ama makundi mengine,hivyo wakati wa kukumbatia Bakwata umeisha kwani serikali inajiweka mbali na waislam kwani bakwata haina mvuto tena.

  Bakwata inafanya inavotaka na kufisadi mali za waislam na kwa sasa bakwata baada ya kuona hawana waislam ambao wapo nyuma yao wanauza mali hizi kwa kasi ya ajab.

  Waislam wana haki na mali hizi, hivi wiwanja na nyumba sio za Issa bin SImba au Al had hawana haki ya kufanya ufisadi na serikali ikawa upande wao.
  Na pia nina neno kwake Mheshimiwa rais kama kiongozi wa nchi una wajibu kuona amani haitoweki kutokana na hili na kwa vile na wewe ni muislam unalo jukumu kubwa kuhakikisha suala la Bakwata unalimaliza kabla ya muda wako wa urais haujaisha
  Livunje hili baraza na badala yake haraka uunde kamati ya muda ambayo itatoka kutoka madhebu yote ya waislam tanzania.Kumbuka Bakwata ndio baraza linalo tambuliwa na serikali kuhusu mambo yote ya waislamu.
  hivyo ni vyema kamati hio ikatoka kutoka madhehebu yote ya waisalm mfano sunni,shia,ibaadhi,bohora,ansari na wengineo.
  kazi ya kamati hii ya muda itakuwa ni kuhakiki mali zote za waislamzilizopo na zilizouzwa kwa njia ya udanganyifu na kama kuna wizi sheria ichukue mkondo wake.

  Pia hio kamati itatakiwa kutengeneza katiba ambayo itapitishwa na misikiti yote
  uwekwe utaratibu wa kuchagua viongozi wapya ambao uwe wa wazi na wanaokubalika.

  nakuhakukishia mheshimiwa rais utakuwa umewafanyia hisani kubwa wasilam wa nchii na kwa taifa lako.matatizo mengi haya yataisha kwani kwa hali ilivo sasa inaonekana kama serikali wao na Bakwata lao moja.
  hili inawezekana na pia naamini kama ulivokuwa na ujasiri wa kuwapatia watanzania katiba mpya basi na hili utaweza.
  Allah akupe nguvu ufanye wema kuepusha shari ya kukumbatia baraza lisilo takiwana utaondoka kama shujaa wa kweli kutafuta suluh
  u katikatatizo kubwa lililo kosa ufumbuzi kwa muda mrefu.
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Macos, Uongozi wa BAKWATA ulipatikanaje? Nani aliwachagua, na kama wanafanya kinyume na maslahi mapana ya waislam wengi hakuna namna yoyote ya kuwaondoa bila ya chombo cha nje kuingilia kati i.e rais kama ulivyoshauri?

  I am curious to know, kama kuna katiba inayoongoza taasisi hii ya waislam na kama ipo inasemaje kuhusu uongozi/miiko? Na pia viongozi wa BAKWATA wakishachaguliwa wanakaa kwa muda gani?
   
 15. A

  Amani kwa wote Member

  #15
  Oct 20, 2012
  Joined: Sep 22, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  aliyeweka hii nyuzi kuna kitu anakitafuta halafu me nashangaa hawa watu wana elimu kweli au wanafikiri sisi ndo kama hao wanaopost picha za matusi FB
   
 16. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  kwa ufupi katiba ya bakwata ilifanyiwa mabadiliko chini ya mrema wakati ule akiwa ccm na kuondoa kabisa uwezekano wa kuondolewa kwa kiongozi ama mufti wa bakwata hata kama atafanya ufisadi aina gani.
  Ku kawaida katiba hizi za asasi za kiraia lazima zipetishwe na wizara ya mamb yandani.. Na mrema aliris=dhia hili
  pili uongozi wa bakwata hauchaguliwi na waislam ama maimam ama taasisi nyengine bali huchaguliwa na wajumbe wa bakwata kutoka kila mkoa amabo nao huwa wanateuliwa na mufti !!
  Sasa utaona hili baraza halina sura ya kitaifa ya waislam...ni kikundi cha wachache lakini kinatambuliwa kama wasemaji wa wasilam wote
  sio haki lazima hali hii irekebishwe...na kwa vile serikali ndio ilio pitisha katiba yao yenye ukiritimba ni wao peke yao wanao weza kulivunja
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hii ndiyo classic example ya 'zidumu fikra za ...". Kama ni nimekuelewa vizuri, ni sawa na wakuu wa mikoa -ambao huteuliwa na rais wawe ndio wanachagua serikali kuu including rais! Mental!

  Na kuhusu katiba, are you saying tangu wakati wa Mwinyi (Mrema alikuwa CCM wakati wa Mwinyi) BAKWATA hawajafanyia marekebisho ya katiba yao licha ya kelele za waumini wanaowaongoza? Is that possible?
   
 18. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  hakuna mabadiliko yaliyofanywa..alipo fariki mufti hemed bin jumaa kuna waislam wasomi walijitokeza kutaka kugombea
  wasomi wa dini na kisekula alikuwepo professa mikidadi na pia proffessa njozi lakini uchaguzi ukaingiliwa na hao wakaaambiwa hawana sifa "ati si wanachama wa bakwata" wakati bakwata inawakilisha waisam wote.ALILETWA HUYU ISSA BIN SIMBA NA SYSTEM HISTORIA YAKE HAIJULIKANI ...ELIMU YAKE YA SCHOOL SIJUI LABDA DARASA LA PILI NA HANA ELIMU YA DINI YA KIISLAM PIA LAKINI NDIO TUMEWEKEWA.
  Nyuma kidogo marehemu omar juma makamo wa rais wakati wa mkapa inasemekana aliliona hili na akataka kurekebisha hali na alijaribu kumshawishi ramadhan dau akubali kuongoza baraza hili lakini inasemekana alipigwa stop.
  Hii ndio kadhia yenyewe
   
 19. Rapha

  Rapha Tanzanite Member

  #19
  Oct 21, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 631
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Kweli wanachanganya!!
   
Loading...