Elections 2015 CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake

Mkuu pasco..
Shkamoo bro... Mapinduziiiii....
Ama baada ya salam kaka... umenikumbusha article moja aliwahi kuandika Joseph Mihangwa about Jumbe... kuna sehem anasema kosa la jumbe lilikua ni "kutaka kukanyaga sehem ambayo hata malaika haruhusiwi kukanyaga"...
Back to the point mkuu... kuhusu experience and oool na mwenye haki ya kushika reigns za uongozi wa nchi yetu hii adhim... should we just get back to a one party state and get away with ool the theatrics of multypartism?
Yes turudi kwenye chama kimoja kwenya urais tuu, ila kwenye ubunge tuendelee kuwa na vyama vingi. Hili la urais tuliweke kabisa kwenye katiba kuwa chama chenye hati miliki ya urais wa JMT na Zanzibar ni CCM!. Hii ni kutokana na long eksipirience ya uzoefu wa muda mrefu!.

Pascal
 
Hii kauli alianza nayo Ali Karume
Pasco umeunga mkono hoja.
Ushauri: Anzisha petition, anzisha kukusanya sahihi za wadau wanaounga mkono hoja hii ili hoja hii akabidhiwe Zitto , Chenge au Mwakyembe aipeleke kama hoja ya dharura bungeni wiki hii ili ijadiliwe na usumbufu wa DOMOkrasi uishe.

Pasco , umenikumbusha "the devil's soldiers"
 
na kama hapa ni kazi tu itakuwa kazi tu pindipo jeshi la Tanganyika likaja kuuwa wazanzibari basi safari hii itakuwa ni TOTAL WARS vita vitahamishiwa tanganyika miundo mbinu yoyote ya tanganyika hiyo itachukuliwa kama ni silaha za kivita TIper pipe gas, airport, majumba ya serikali, badari, petrol station vyote hivyo vitachukuliwa kama ni silaha zakivita kwahivyo mukija kutuuwa safari hii ni kuuwana tu tanganyika haita baki salama ni TOTAL wars
 
Macho yote ya dunia yatakuwa kwenye uchaguzi wa Zanzibar, hivyo CUF ikishinda tena this time itatangazwa!.

Kuna hoja kuwa siku zote CUF huwa inashinda uchaguzi wa Zanzibar lakini haitangazwi!, kama hili ni kweli, then lazima kuna sababu kwa nini CUF washinde na wasitangazwe!. Sasa bila kuzijua hizo sababu, watu humu watabaki wanapga tuu kelele!. Watu wangezijua hizo sababu, kisha wajiulize kama siku zote CUF anashinda lakini hatangazwi kwa sababu abc, sasa ili this time shinde na kutangazwa, then hizo sababu nazo ziwe zimebadilika!.

Niliwauliza wenyewe CUF mara kibao, kama ni kweli siku zote huwa wanashinda lakini hawatangazwi, kitu kipi kimewafanya waamini this time wakishinda watatangazwa?!, hakuna mwenye jibu!.

Kiukweli siku zote uchaguzi wa Zanzibar ni twists and tuns, sometimes margin ya mshindi na mshindwa ni just 2% hivyo whoever knows the best game akifanikiwa ku twist, yeye ndio mshindi, ndio maana nimewauliza CUF, kama walishinda kihalali kwa kua nyingi, nini kinachowafanya waogope kurudiwa kwa uchaguzi, si ni watashinda tena?!, hawana jibu!.

Pasco

Pasco hope this time tumejua ukweli,na ukweli siku zote unakuweka huru.

UKWELI wa CUF kutokutangazwa sababu kuu ni UCHOTARA wa MAALIM SEIF,tumeona kwenye mabango ya CCM siku ya kusheherekea MAPINDUZI,tumeona mabango kwenye vijiwe vya CCM Zanzibar,tumeona kwenye mitandao wanaCCM wakiendeleza ubaguzi huu wa RANGI na hakuna TCRA inayokemea wala kufanya kazi yake hapo.

Na sababu ya pili kubwa ni kwamba CCM imesema haitatoa Zanzibar kwa VIKARATASI sasa unauhakika gani CUF wakishinda tena watapewa?Uhakika ni huu hata wakishinda hawatapewa tutarudia tena UCHAGUZI maana UCHAGUZI ni HURU NA HAKI pale CCM tu ikishinda.
 
na kama hapa ni kazi tu itakuwa kazi tu pindipo jeshi la Tanganyika likaja kuuwa wazanzibari basi safari hii itakuwa ni TOTAL WARS vita vitahamishiwa tanganyika miundo mbinu yoyote ya tanganyika hiyo itachukuliwa kama ni silaha za kivita TIper pipe gas, airport, majumba ya serikali, badari, petrol station vyote hivyo vitachukuliwa kama ni silaha zakivita kwahivyo mukija kutuuwa safari hii ni kuuwana tu tanganyika haita baki salama ni TOTAL wars
Mkuu Kifoi, nimekuripoti kwa mode, ili awape kabisa jina lako 'wale jamaa' zetu ili kutumia kinga kuliko kuja kutibu!. Nakuomba waage kabisa ndugu zako kwa kuwaambia ulisema nini humu jf!. Uhuru wa jf kutumia majina sio kinga ya ugaidi kwa kisingizio cha sababu yoyote ile!, na mode kama Mtanzania, anawajibika kuwa disclose magaidi wote tulionao humu jf, au hata wale wenye elements za ugaidi!.

Pasco
 
UKISUSA WENGINE TWALA - NINA MASHAKA NA MAALIM SEIF

Mzee Jecha ametangazia umma wa wazanzibar kuwa uchaguzi wa marudio ni machi 20 kufuatia kufutwa kwa uchaguzi wa oct 25 2015 kwa sababu ambazo kisayansi haziendani kabisa ila zinaendana saaana na siasa, lakini maji yamemwagika tukachote mengine!

Baadhi ya vyama vya siasa vinafurahia sana kurudiwa kwa uchaguzi huu na vingine vinagoma kurudiwa kwa uchaguzi huu, lakini mstakbari wa wazanzibar wanahitaji kuwa na amani, je amani ya lazima itafaulu kuweka nchi katika utulivu?

Kuna baadhi ya wapenda mageuzi au mabadiliko nchini wanakosa imani na Maalim Seif hii inakuja baada ya kusema CUF haitarudia uchaguzi Zanzibar, sasa kama hamtarudia uchaguzi Zanzibar si ushindi utakwenda kwa CCM dhahiri? Eti kurudia uchaguzi Zanzibar ni haramu! sasa ukisusa na CCM washinde viti vyote ndiyo itakuwa halali?

TUACHE KUWA DOUBLE STANDARD, TWENDE TUKAPIGE KURA, TENA TUJITOKEZE KWA WINGI TUWAONESHE CCM TULISHINDA KWA UKWELI
Nimeikuta hii mahali,

Pasco
 
Pia nimeikuta hii mahali
Chama kikuu cha upinzani Zanzibar CUF, kimeitaka Tume ya Uchaguzi visiwani humo ZEC kuondoa na kutotumia karatasi za kupigia kura zenye kuonesha jina la mgombea wake wa urais pamoja na baraza la wawakilishi kwa lengo la kugomea uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20 visiwani humo.

Chanzo: DW Swahili
Marudio haya ni kwenye Kupiga kura tu!
Hakuna kujiuzulu wala kujitoa Mjumbe yeyote wa Tume ya Uchaguzi.
Hakuna kujaza form ya kugombea wala kutogombea.
Hakuna Kampeni za kuomba kuchaguliwa au kutochaguliwa.
Hakuna kubadilisha Mawakala wala Vituo vya kupiga kura.
Hata uamuzi wa ADC kumvua uanachama Hamad Rashid( Mgombea Urais) hautambuliki.
CUF wasilete Chokochoko na kuleta Uvunjuifu wa Amani
Kama wamejitoa wanachama wao si hawatoenda kupiga kura hivyo Pressure ya nini?
Gharama za kuchapisha upya makaratasi ya kupigia kura ili kuondoa Jina na sura ya Mtu ni bora zipelekwe kwenye Huduma za kijamii
Baeleze baelewe!.

Cuf wanataka kujifurahisha tuu, hakuna cha kujitoa, na kushiriki uchaguzi huu wa marudia sio hiyari bali ni lazima!.
Nisome hapa nilisema nini
CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima

Pasco
 
Wanabodi, baada ya kutangazwa tarehe ya uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar, kuna watu wanadhani Chama cha Wananchi CUF, kina hiyari ya kushiriki uchaguzi huo au kutoshiriki, as if kushiriki uchaguzi wa marudio ni jambo la hiyari!, no way!, watakuwa wanajidanya!. CUF hakina option yoyote ya kuamua ama ishiriki ama isishiriki uchaguzi huo, kwa sababu ushiriki wa uchaguzi wa marudio sio suala la option bali ni jambo la lazima, watake wasitake ni lazima washiriki, kwa sababu kila kitu kiko vile vile kama mwanzo!, nikimaanisha hata wakisusa, picha na majina ya wagombea wao yatakuwepo kwenye karatasi za kura!.

Wenye option ya kuamua kushiriki au kutoshiriki uchaguzi huo ni wapiga kura, ndio wanaweza kuamua ama kujitokeza kushiriki kupiga kura, au kususa kupiga kura kwa kutokujitokeza, na mgombea hata kama atapata kura moja ya ndio, ndio atatangazwa mshindi!, hivyo kupiga kura au kutopiga kura ndio bado ni option!, lakini kushiriki uchaguzi huo sio option ni jambo la lazima!.

Iwapo CUF itatangaza kususia uchaguzi huo, tangazo hilo ndilo litakuwa tangazo rasmi la kifo rasmi cha kilichokuwa kinaitwa Chama cha Wananchi CUF, kwa sababu, ngome kuu ya CUF ni Pemba, kususia uchaguzi ni kuipoteza Pemba ambapo na ngome kuu ikiishakuangua, it is just a matter of time, chama chenyewe chote kielekee kaburini!.

Hata kama CUF watatangaza kususa, majina ya wagombea wa CUF tayari yako kwenye karatasi za kura katika uchaguzi huo, hivyo wakitangaza kususa, maana ni wagombea wa CUF hawatachaguliwa, hivyo kuipatia CCM ushindi wa mezani, ikiwemo kuitwaa ngome ya CUF kule Pemba na kuivunja uti wake wa mgongo, kwa CCM kuvitwaa viti vyote vya Uwakilishi Zanzibar na Pemba, ambapo pia huo ndio utakuwa mwisho wa SUK na CCM kutawala peke yake na kuhitimishwa kwa kifo rasmi cha chama cha wananachi, CUF!.

Nakiri kupandisha uzi huu kufuatia bandiko la mwana jf huyu

Hoja katika badhiko hilo mi kitisho cha CUF kuwa kisiposhiriki, hali ya amani na utulivu wa visiwa vya Zanzibar, utakuwa mashakani!. Maadam Zanzibarr sio nchi bali ni sehemu ya JMT, dhima ya muungano, ni undungu wa asili kati ya watu wa Tanganyika na watu wa Zanzibar, lakini sababu halisi ya muungano ni kuipatia Zanzibar ulinzi na usalama, Zanzibar haina polisi wala jeshi, hivyo jukumu la ulinzi na usalama wa Zanzibar, sio jukumu la Zanzibar tuu, bali ni jukumu la JMT, haiwezekani sehemu moja ya JMT iwe katika hali tete, wakati JMT ni nchi moja, ulinzi na usalama wa JMT utakuwa mikononi mwa JMT!.

Hivyo CUF washiriki uchaguzi huu wa marudio, au wasishiriki kwa kuususia, it will not make any difference kwenye amani na utulivu wa Zanzibar kwa sababu jukumu la ulinzi na usalama wa Zanzibar, sio jukumu la Wanzanzibari wenyewe pekee, bali pia ni jukumu la serikali ya JMT, chini ya Amiri Jeshi Mkuu, Dr. Joh Pombe Magufuli!.

Zanzibar kama sehemu ya JMT, inayo assuarance ya Amri Jeshi Mkuu wa JMT, kuhakikisha kuwa Uchaguzi wa marudio wa Zanzibar, uliotangazwa, utafanyika kwa uhuru, amani, usalama na utulivu, mshindi atapatikana kwa haki, atatangazwa, ataapishwa na kuunda serikali nyingine ya Zanzibar yenye jina la SUK lakini wawakilishi wa CUF kuendelea kuitawala Zanzibar kwa uhuru na amani kabisa bila`wasiwasi wowote kwa ile falsafa ya kule ya Mapinduzi Daima!.

Demokasia ya kweli ni serikali ya watu, inayoongozwa na watu kwa manufaa ya watu hao!, (of the people, by the people, and for the people), ila demokasia hiyo haikuwe kiwango cha asilimia ya watu hao!, hivyo hata kama nchi ina watu milioni moja, serikali ikachaguliwa na watu 10 tuu, bado serikali hiyo itakuwa ni serikali halali kisheria, japo itakosa peoples legitimacy, kwa watu hao ndio watakuwa wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kutokupiga kura!.

Kushiriki uchaguzi wowote, kwa kugombea nafasi yoyote ni hiyari, pia kuamua kutokushiriki katika uchaguzi pia ni hiyari, sambamba na kujiandikisha kupiga kura ni hiyari, kutokujiandikisha pia ni hiyari, na kujiandikisha kupiga kura na kisha kuamua kutokupiga kura pia ni hiyari, zote hizo ni demokrasia.Kama CUF itawashawishi wafuasi wake kususia uchaguzi huo, hiyo itakuwa ndio demokrasia yao!.

Kitendo cha CUF kushiriki uchaguzi wa mwanzo kunaifanya CUF ni lazima ishiriki uchaguzi wa marudio sio kwa hiyari ua kwa kupenda, bali ipende, isipende, ni lazima ishiriki uchaguzi huo!.

Hapa hakuna suala la choice. Na iwapo CUF watasusa kushiriki uchaguzi huo wa marudio, kususa huko kutakuwa ni kususa batili kwa sabu picha na majina ya wagombea wa CUF yataendelea kuwepo kwenye karatasi za kura!, hivyo kususa huko ndiko kutakao ipatia CCM ushindi wa mezani, tena this time CCM itashinda viti vyote vya uwakilishi Unguja na Pemba, na huu ndio utakuwa mwisho rasmi wa CUF. Kamwe CUF isikubali kuingia katika mtego wa kususia uchaguzi wa marudio!.

Turufu ya CUF kutishia kususa ni kwa kisingizio cha itabembelezwa ili kusitokea machafuko Zanzibar!. Kiukweli JK alikuwa ni mpole sana, hivyo Zanzibar imemchezea sana hadi kumtia vidole machoni katika yale mabadiliko batili ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010.

Kwa sasa Amiri Jeshi Mkuu ni Dr. John Pombe Magufuli, hii ni namba nyingine, huyu sio mtu wa mchezo mchezo au kuchezewa kama JK, hivyo CUF kama wanadhani watasusa na kubembelezwa, ili kuepusha machafuko Zanzibar, nawahakikishia this time watakuwa wame bugi step, hata wakisusa, hakutakuwa na vujo wala ,achafuko yoyote Zanzibar kwa sababu sasa ni zamu ya hapa hapa ni kazi tuu!.

Wanzanzibar, na Watanzania wote, chini ya Amiri Jeshi Mkuu, wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya JMT, tuna jukumu kubwa la kuilinda amani na utulivu wa eneo lote la JMT, ikiwemo Zanzibar, kwa gharama yoyote!, hii ikiwa ni pamoja na kuulinda muungano kwa gharama yoyote!.
Wasalaam
Pasco
Mkuu Pasco hapo umenena,
Pamoja na ukweli kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa katika Baraza la Wawakilishi CUF haitakuwemo, na vile vile Maalim Seif Hamad ndo atatoweka kwenye misafara ya urais.
 
Pia nimeikuta hii mahali

Baeleze baelewe!.

Cuf wanataka kujifurahisha tuu, hakuna cha kujitoa, na kushiriki uchaguzi huu wa marudia sio hiyari bali ni lazima!.
Nisome hapa nilisema nini
CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima

Pasco
Baada ya Jecha kutangaza tarehe ya maigizo ya uchaguzi wa marudio na kuifurahisha CCM. Mkwamo unataka kuchukua hatua mpya. Sinema ya Jecha na CCM inahamia Mahakamani.

Nineikuta sehemu:
Katika hatua nyingine mawakilishi na madiwani wateule wa CUF kupanga kwenda mahakamani kutetea nafasi zao.

Wameeleza kwamba, kwa kuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imewapa hati za ushindi baada ya kufanya uchaguzi mkuu tarehe 25 Oktoba 2015, mpaka sasa hakuna aliyejitokeza kupinga ushindi wao.

Hata hivyo, Maalim Seif amesema, viongozi hao waliochaguliwa na wananchi katika uchaguzi huo na kisha kupewa shahada zao, watakwenda mahakamani kutetea nafasi zao na kutoruhusu viongozi wengine wa ngazi hizo kuchaguliwa tena kwa vile wao wanavyo vielelezo vyote vya kuchaguliwa kwao.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi yaliyobandikwa katika vituo vya kupigia kura na kuthibitishwa na wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo, majimbo yote 18 ya uchaguzi Kisiwani Pemba yalichukuliwa na CUF, sambamba na wadi zote 32 za uchaguzi.

Chanzo : Maalim Seif: Ondoeni shaka, nitatangazwa

Je mahakama itafanya kazi yake kwa uhuru? Au mahakama itageuka Jecha namba 2?

Angalizo: Kisheria ,Tume ikishatangaza matokeo haiwezi kuyafuta. Kinaachoweza kufanywa na mlalamikiaji wa matokeo ni kwenda Mahakamani. Mahakama ikiridhika na ushahidi wa kupinga matokeo. mahakama inatengua matokeo hayo(inafuta matokeo) na kuamuru uchaguzi wa marudio.
Jecha aliingilia kazi ya Mahakama.
 
Wanabodi, baada ya kutangazwa tarehe ya uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar, kuna watu wanadhani Chama cha Wananchi CUF, kina hiyari ya kushiriki uchaguzi huo au kutoshiriki, as if kushiriki uchaguzi wa marudio ni jambo la hiyari!, no way!, watakuwa wanajidanya!. CUF hakina option yoyote ya kuamua ama ishiriki ama isishiriki uchaguzi huo, kwa sababu ushiriki wa uchaguzi wa marudio sio suala la option bali ni jambo la lazima, watake wasitake ni lazima washiriki, kwa sababu kila kitu kiko vile vile kama mwanzo!, nikimaanisha hata wakisusa, picha na majina ya wagombea wao yatakuwepo kwenye karatasi za kura!.

Wenye option ya kuamua kushiriki au kutoshiriki uchaguzi huo ni wapiga kura, ndio wanaweza kuamua ama kujitokeza kushiriki kupiga kura, au kususa kupiga kura kwa kutokujitokeza, na mgombea hata kama atapata kura moja ya ndio, ndio atatangazwa mshindi!, hivyo kupiga kura au kutopiga kura ndio bado ni option!, lakini kushiriki uchaguzi huo sio option ni jambo la lazima!.

Iwapo CUF itatangaza kususia uchaguzi huo, tangazo hilo ndilo litakuwa tangazo rasmi la kifo rasmi cha kilichokuwa kinaitwa Chama cha Wananchi CUF, kwa sababu, ngome kuu ya CUF ni Pemba, kususia uchaguzi ni kuipoteza Pemba ambapo na ngome kuu ikiishakuangua, it is just a matter of time, chama chenyewe chote kielekee kaburini!.

Hata kama CUF watatangaza kususa, majina ya wagombea wa CUF tayari yako kwenye karatasi za kura katika uchaguzi huo, hivyo wakitangaza kususa, maana ni wagombea wa CUF hawatachaguliwa, hivyo kuipatia CCM ushindi wa mezani, ikiwemo kuitwaa ngome ya CUF kule Pemba na kuivunja uti wake wa mgongo, kwa CCM kuvitwaa viti vyote vya Uwakilishi Zanzibar na Pemba, ambapo pia huo ndio utakuwa mwisho wa SUK na CCM kutawala peke yake na kuhitimishwa kwa kifo rasmi cha chama cha wananachi, CUF!.

Nakiri kupandisha uzi huu kufuatia bandiko la mwana jf huyu

Hoja katika badhiko hilo mi kitisho cha CUF kuwa kisiposhiriki, hali ya amani na utulivu wa visiwa vya Zanzibar, utakuwa mashakani!. Maadam Zanzibarr sio nchi bali ni sehemu ya JMT, dhima ya muungano, ni undungu wa asili kati ya watu wa Tanganyika na watu wa Zanzibar, lakini sababu halisi ya muungano ni kuipatia Zanzibar ulinzi na usalama, Zanzibar haina polisi wala jeshi, hivyo jukumu la ulinzi na usalama wa Zanzibar, sio jukumu la Zanzibar tuu, bali ni jukumu la JMT, haiwezekani sehemu moja ya JMT iwe katika hali tete, wakati JMT ni nchi moja, ulinzi na usalama wa JMT utakuwa mikononi mwa JMT!.

Hivyo CUF washiriki uchaguzi huu wa marudio, au wasishiriki kwa kuususia, it will not make any difference kwenye amani na utulivu wa Zanzibar kwa sababu jukumu la ulinzi na usalama wa Zanzibar, sio jukumu la Wanzanzibari wenyewe pekee, bali pia ni jukumu la serikali ya JMT, chini ya Amiri Jeshi Mkuu, Dr. Joh Pombe Magufuli!.

Zanzibar kama sehemu ya JMT, inayo assuarance ya Amri Jeshi Mkuu wa JMT, kuhakikisha kuwa Uchaguzi wa marudio wa Zanzibar, uliotangazwa, utafanyika kwa uhuru, amani, usalama na utulivu, mshindi atapatikana kwa haki, atatangazwa, ataapishwa na kuunda serikali nyingine ya Zanzibar yenye jina la SUK lakini wawakilishi wa CUF kuendelea kuitawala Zanzibar kwa uhuru na amani kabisa bila`wasiwasi wowote kwa ile falsafa ya kule ya Mapinduzi Daima!.

Demokasia ya kweli ni serikali ya watu, inayoongozwa na watu kwa manufaa ya watu hao!, (of the people, by the people, and for the people), ila demokasia hiyo haikuwe kiwango cha asilimia ya watu hao!, hivyo hata kama nchi ina watu milioni moja, serikali ikachaguliwa na watu 10 tuu, bado serikali hiyo itakuwa ni serikali halali kisheria, japo itakosa peoples legitimacy, kwa watu hao ndio watakuwa wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kutokupiga kura!.

Kushiriki uchaguzi wowote, kwa kugombea nafasi yoyote ni hiyari, pia kuamua kutokushiriki katika uchaguzi pia ni hiyari, sambamba na kujiandikisha kupiga kura ni hiyari, kutokujiandikisha pia ni hiyari, na kujiandikisha kupiga kura na kisha kuamua kutokupiga kura pia ni hiyari, zote hizo ni demokrasia.Kama CUF itawashawishi wafuasi wake kususia uchaguzi huo, hiyo itakuwa ndio demokrasia yao!.

Kitendo cha CUF kushiriki uchaguzi wa mwanzo kunaifanya CUF ni lazima ishiriki uchaguzi wa marudio sio kwa hiyari ua kwa kupenda, bali ipende, isipende, ni lazima ishiriki uchaguzi huo!.

Hapa hakuna suala la choice. Na iwapo CUF watasusa kushiriki uchaguzi huo wa marudio, kususa huko kutakuwa ni kususa batili kwa sabu picha na majina ya wagombea wa CUF yataendelea kuwepo kwenye karatasi za kura!, hivyo kususa huko ndiko kutakao ipatia CCM ushindi wa mezani, tena this time CCM itashinda viti vyote vya uwakilishi Unguja na Pemba, na huu ndio utakuwa mwisho rasmi wa CUF. Kamwe CUF isikubali kuingia katika mtego wa kususia uchaguzi wa marudio!.

Turufu ya CUF kutishia kususa ni kwa kisingizio cha itabembelezwa ili kusitokea machafuko Zanzibar!. Kiukweli JK alikuwa ni mpole sana, hivyo Zanzibar imemchezea sana hadi kumtia vidole machoni katika yale mabadiliko batili ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010.

Kwa sasa Amiri Jeshi Mkuu ni Dr. John Pombe Magufuli, hii ni namba nyingine, huyu sio mtu wa mchezo mchezo au kuchezewa kama JK, hivyo CUF kama wanadhani watasusa na kubembelezwa, ili kuepusha machafuko Zanzibar, nawahakikishia this time watakuwa wame bugi step, hata wakisusa, hakutakuwa na vujo wala ,achafuko yoyote Zanzibar kwa sababu sasa ni zamu ya hapa hapa ni kazi tuu!.

Wanzanzibar, na Watanzania wote, chini ya Amiri Jeshi Mkuu, wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya JMT, tuna jukumu kubwa la kuilinda amani na utulivu wa eneo lote la JMT, ikiwemo Zanzibar, kwa gharama yoyote!, hii ikiwa ni pamoja na kuulinda muungano kwa gharama yoyote!.
Wasalaam
Pasco

Mkuu safi sana kwa ufafanuzi. Ila nauliza ivi tunafuata upole wa mtu au umakini wa mtu au tunafuata democracy? maana unasema ooh mara Magu achezewi kama kktwe. kwa iyo ni ruksa serikali kuwa juu ya sheria?
 
Tatizo wanasheria wa UKAWA na UKAWA kwa ujumla ni mbumbumbu wa sheria.Wasome kifungu namba 28 cha sheria ya uchaguzi ya Zanzibar.Mtu akitaka kujitoa Yeye mwenyewe anatakiwa aandike atie sahihi mbele ya jaji au hakimu kuhusu kujitoa kwake.Angalia upuuzi aliofanya CUF eti wametoa tamko la kujitoa!!!! Sheria haitambui tamko la chama kujitoa inatambua mtu kujitoa .Wakuu naweka sheria hiyo hapa muone umbumbumbu walionao CUF NA WAPIGA FILIMBI WAO AKINA LOWASA.Soma pale kifungu cha 28 cha hii sheria ya uchaguzi zanzibar kuhusu kujitoa muone.Hili ni kosa moja tu la kisheria walilokosea CUF yako matano mengine zaidi siandiki hapa sababu silipwi kwa kazi hiyo.Jecha yuko vizuri mno kichwani kuliko hao mbumbumbu wa CUF

http://zec.go.tz/en/wp-content/uploads/2015/08/Kanuni.pdf
Hii hoja yangu kuwa CUF ni lazima washiriki uchaguzi wa marudio bado iko valid, CUF wapende wasipende, ni lazima washiriki na hakuna cha kujitoa!.

Mapinduzi Daima

Pasco
 
Mawakala wa cuf kutokuwepo siku ya kupiga kura 20 march inatosha kuitangazia dunia kuwa Cuf haijashiriki uchaguzi.
 
Hivi unamjua Pasco ama unajifanya taahira? Kati ya Pasco na wewe Mmawia nani hadhi yake ni kubwa humu jf? Au kwa vile kaandika kitu ambacho kimekuchukiza? Pasco yupo upande wenu isipokuwa anaandika kutokana na hali halisi. Binafsi namkubali sana Pasco ijapokuwa tumekuwa tukikwaruzana katika mambo mengi hususan mapenzi yake kwa Lowasa
Hakuna member mwenye hadhi kubwa kuliko mwenzake hapa jukwaani msijitukuze kabla ya kutukuzwa
 
Nakumbushia tuu kuna neno nilisema humu kuhusu CUF kushiiki kwa lazima itake isitake, nilipuuzwa, lakini jana Jecha kayasema haya haya, sijui na yeye atapuuzwa?!. Najua CUF kama kawaida yao, watakuja na matamko. Matamko hayasaidii kitu, ama wachukue hatua au wakae kimya na kushiiki uchaguzi huu!.

Bila wasiwasi naamini wanachama wa vyama vyote vya siasa Zanzibar watashiriki uchaguzi wa marudio pamoja na shinikizo la viongozi wao waliotaka ushindi wa mezani.
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom