Elections 2015 CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,441
113,449
Wanabodi, baada ya kutangazwa tarehe ya uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar, kuna watu wanadhani Chama cha Wananchi CUF, kina hiyari ya kushiriki uchaguzi huo au kutoshiriki, as if kushiriki uchaguzi wa marudio ni jambo la hiyari!, no way!, watakuwa wanajidanya!. CUF hakina option yoyote ya kuamua ama ishiriki ama isishiriki uchaguzi huo, kwa sababu ushiriki wa uchaguzi wa marudio sio suala la option bali ni jambo la lazima, watake wasitake ni lazima washiriki, kwa sababu kila kitu kiko vile vile kama mwanzo!, nikimaanisha hata wakisusa, picha na majina ya wagombea wao yatakuwepo kwenye karatasi za kura!.

Wenye option ya kuamua kushiriki au kutoshiriki uchaguzi huo ni wapiga kura, ndio wanaweza kuamua ama kujitokeza kushiriki kupiga kura, au kususa kupiga kura kwa kutokujitokeza, na mgombea hata kama atapata kura moja ya ndio, ndio atatangazwa mshindi!, hivyo kupiga kura au kutopiga kura ndio bado ni option!, lakini kushiriki uchaguzi huo sio option ni jambo la lazima!.

Iwapo CUF itatangaza kususia uchaguzi huo, tangazo hilo ndilo litakuwa tangazo rasmi la kifo rasmi cha kilichokuwa kinaitwa Chama cha Wananchi CUF, kwa sababu, ngome kuu ya CUF ni Pemba, kususia uchaguzi ni kuipoteza Pemba ambapo na ngome kuu ikiishakuangua, it is just a matter of time, chama chenyewe chote kielekee kaburini!. Tena CUF kisijidanganye kwa kudhani kwa vile kinakubalika sana Pemba, kinaweza kususa na kuiacha Pemba chini ya CCM, halafu uchaguzi wa 2020, kitarudi tena Pemba na kuitwaa tena ngome yake!, that would be a grave mistake!, ni kosa la kifo, CUF iliachia ngome yake itekwe na CCM, itakuwa imetekwa jumla, 2020, CUF itaishia kwenye kilio na kusaga meno, maana they will never regain what they lost!.

Hata kama CUF watatangaza kususa, majina ya wagombea wa CUF tayari yako kwenye karatasi za kura katika uchaguzi huo, hivyo wakitangaza kususa, maana ni wagombea wa CUF hawatachaguliwa, hivyo kuipatia CCM ushindi wa mezani, ikiwemo kuitwaa ngome ya CUF kule Pemba na kuivunja uti wake wa mgongo, kwa CCM kuvitwaa viti vyote vya Uwakilishi Zanzibar na Pemba, ambapo pia huo ndio utakuwa mwisho wa SUK na CCM kutawala peke yake na kuhitimishwa kwa kifo rasmi cha chama cha wananachi, CUF!.

Nakiri kupandisha uzi huu kufuatia bandiko la mwana jf huyu

Haiwi haiwi uvumivu sasa umefikia mwisho ,Polisi wa Muungano wapo njiani wakisaidia juhudi za mwizi kuendeleza wizi kwa maana sasa wananchi kila mmoja kwa upande wake anatoka njiani kifua mbele kupinga hatua za CCM kutaka uchaguzi urudiwe kwa kuwa ilipigwa na chini ,wanachi wakati wa kulazimishwa kuekewa utawala wasio uchagua umepitwa na wakati.

Polisi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wapo njiani kupambana na wananchi wenye hasira kali ,muda huu ni mabomu kila kona na pia inasemekana zimesikika risasi za moto.
Kama huamini mpigie simu aliepo Zanzibar.

Hoja katika badhiko hilo mi kitisho cha CUF kuwa kisiposhiriki, hali ya amani na utulivu wa visiwa vya Zanzibar, utakuwa mashakani!. Maadam Zanzibarr sio nchi bali ni sehemu ya JMT, dhima ya muungano, ni undungu wa asili kati ya watu wa Tanganyika na watu wa Zanzibar, lakini sababu halisi ya muungano ni kuipatia Zanzibar ulinzi na usalama, Zanzibar haina polisi wala jeshi, hivyo jukumu la ulinzi na usalama wa Zanzibar, sio jukumu la Zanzibar tuu, bali ni jukumu la JMT, haiwezekani sehemu moja ya JMT iwe katika hali tete, wakati JMT ni nchi moja, ulinzi na usalama wa JMT utakuwa mikononi mwa JMT!.

Hivyo CUF washiriki uchaguzi huu wa marudio, au wasishiriki kwa kuususia, it will not make any difference kwenye amani na utulivu wa Zanzibar kwa sababu jukumu la ulinzi na usalama wa Zanzibar, sio jukumu la Wanzanzibari wenyewe pekee, bali pia ni jukumu la serikali ya JMT, chini ya Amiri Jeshi Mkuu, Dr. Joh Pombe Magufuli!.

Zanzibar kama sehemu ya JMT, inayo assuarance ya Amri Jeshi Mkuu wa JMT, kuhakikisha kuwa Uchaguzi wa marudio wa Zanzibar, uliotangazwa, utafanyika kwa uhuru, amani, usalama na utulivu, mshindi atapatikana kwa haki, atatangazwa, ataapishwa na kuunda serikali nyingine ya Zanzibar yenye jina la SUK lakini wawakilishi wa CUF kuendelea kuitawala Zanzibar kwa uhuru na amani kabisa bila`wasiwasi wowote kwa ile falsafa ya kule ya Mapinduzi Daima!.

Demokasia ya kweli ni serikali ya watu, inayoongozwa na watu kwa manufaa ya watu hao!, (of the people, by the people, and for the people), ila demokasia hiyo haikuwe kiwango cha asilimia ya watu hao!, hivyo hata kama nchi ina watu milioni moja, serikali ikachaguliwa na watu 10 tuu, bado serikali hiyo itakuwa ni serikali halali kisheria, japo itakosa peoples legitimacy, kwa watu hao ndio watakuwa wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kutokupiga kura!.

Kushiriki uchaguzi wowote, kwa kugombea nafasi yoyote ni hiyari, pia kuamua kutokushiriki katika uchaguzi pia ni hiyari, sambamba na kujiandikisha kupiga kura ni hiyari, kutokujiandikisha pia ni hiyari, na kujiandikisha kupiga kura na kisha kuamua kutokupiga kura pia ni hiyari, zote hizo ni demokrasia.Kama CUF itawashawishi wafuasi wake kususia uchaguzi huo, hiyo itakuwa ndio demokrasia yao!.

Kitendo cha CUF kushiriki uchaguzi wa mwanzo kunaifanya CUF ni lazima ishiriki uchaguzi wa marudio sio kwa hiyari ua kwa kupenda, bali ipende, isipende, ni lazima ishiriki uchaguzi huo!.

Hapa hakuna suala la choice. Na iwapo CUF watasusa kushiriki uchaguzi huo wa marudio, kususa huko kutakuwa ni kususa batili kwa sabu picha na majina ya wagombea wa CUF yataendelea kuwepo kwenye karatasi za kura!, hivyo kususa huko ndiko kutakao ipatia CCM ushindi wa mezani, tena this time CCM itashinda viti vyote vya uwakilishi Unguja na Pemba, na huu ndio utakuwa mwisho rasmi wa CUF. Kamwe CUF isikubali kuingia katika mtego wa kususia uchaguzi wa marudio!.

Turufu ya CUF kutishia kususa ni kwa kisingizio cha itabembelezwa ili kusitokea machafuko Zanzibar!. Kiukweli JK alikuwa ni mpole sana, hivyo Zanzibar imemchezea sana hadi kumtia vidole machoni katika yale mabadiliko batili ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010.

Kwa sasa Amiri Jeshi Mkuu ni Dr. John Pombe Magufuli, hii ni namba nyingine, huyu sio mtu wa mchezo mchezo au kuchezewa kama JK, hivyo CUF kama wanadhani watasusa na kubembelezwa, ili kuepusha machafuko Zanzibar, nawahakikishia this time watakuwa wame bugi step, hata wakisusa, hakutakuwa na vujo wala ,achafuko yoyote Zanzibar kwa sababu sasa ni zamu ya hapa hapa ni kazi tuu!.

Wanzanzibar, na Watanzania wote, chini ya Amiri Jeshi Mkuu, wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya JMT, tuna jukumu kubwa la kuilinda amani na utulivu wa eneo lote la JMT, ikiwemo Zanzibar, kwa gharama yoyote!, hii ikiwa ni pamoja na kuulinda muungano kwa gharama yoyote!.
Wasalaam
Pasco
 
Wanabodi, baada ya kutangazwa tarehe ya uchaguzi wa visiwani Zanzibar,

Kuna watu wanadhani Chama cha Wananchi CUF, kina hiyari kushiriki uchaguzi huo au kutoshiri, as if kushiriki uchaguzi wa marudio ni jambo la hiyari!, watakuwa wanajidanya!. CUF hakina option yoyote ya kuamua ama ishiiki ama isishiriki, kwa sababu ushiriki wa uchaguzi wa marrudio sio option bali ni lazima kwa sababu kila kitu kiko vile vile kam,a mwanzo!.

Wenye option ya kuamua kushiriki au kutoshiriki ni wapiga kura, ndio wanaweza kuamua ama kujitokeza kushiriki kupiga kua, au kususa kupiga kura, na mgombea hata kama atapata kura moja ya ndio, ndio atatangazwa mshindi!, hivyo kupiga kura au kutopiga kura ndio bado ni option!, iwapo CUF itatangaza kususia uchaguzi huo, tangazo hilo ndilo litakuwa tangazo rasmi la kifo rasmi cha kilichokuwa Chama cha Wananchi CUF, kwa sababu majina ya wagombea wa CUF tatakuwepo kwenye karatasi za uchaguzi na hawatachaguliwa, hivyo kuipatia CCM ushindi wa mezani, ikiwemo kuivunja ngome ya CUF kule Pemba, kwa CCM kuvitwaa viti vyote vya Uwakilishi Zanzibarr na Pemba, ambapo pia huo ndio utakuwa mwisho wa SUK na CCM kutawala peke yake na kuhitimishwa kwa kifo rasmi cha chama cha wananachi, CUF!.

Nakiri kupandisha uzi huu kufuatia bandiko la mwana jf huyu
Zanzibarr sio nchi bali ni sehemu ya JMT, dhima ya muungano, ni undungu wa asili kati ya watu wa Tanganyika na Zanzibar, lakini sababu halisi ya muungano ni kuipatia Zanzibar ulinzi na usalama, Zanzibar haina polisi wala jeshi, hivyo jukumu la ulinzi na usalama wa Zanzibar, sio jukumu la Zanzibar, ni jukumu la JMT!. Hivyo CUF washirriki au wasuse, it will make no diference kwa sabau jukumu la ulinzi na usalama wa Zanzibar, ni jukumu la serikali ya JMT, chini ya Amiri Jeshi Mkuu, Drr. Jojm Pombe Magufuli.

Uchaguzi umetangazwa, utafanyika kwa amani na utulivu, mshindi atapatikana kwa haki, atatangazwa, ataapishwa na kuunda SUK nyingine, kwa uhuru kabisa bila`wasiwasi wowote!.

Hata hivyo kushiriki uchaguzi kugombea nafasi yoyote ni hiyari, pia kuamua kutokushiriki katika uchaguzi pia ni hiyari, sambamba na kujiandikisha kupiga kura ni hiyari, kutokujiandikisha pia ni hiyari, na kujiandikisha kupiga kura na kutokupiga kura pia ni hiyari, zote hizo ni demokrasia.

Kitendo cha CUF kushiriki uchaguzi wa mwanzo kunaifanya CUF ni lazima ishiriki uchaguzi wa maudio sio kwa hiyai bali kwa lazima. Hapa hakuna choice. Na iwapo CUF watasusana uchaguzi wa marudio, kususa huko kutakuwa ni kususa batili. kutakao ipatia CCM ushindi wa mezani, tena this time CCM itashinda viti vyote vya uwakilishi Unguja na Pemba, na huu ndio utakuwa mwisho rasmi wa CUF. Kamwe CUF isikubali kuingia katika mtego wa kususia uchaguzi wa marudio!.

Kikweli JK alikuwa ni mpole sana, hivyo Zanzibar imemchezea sana hadi kumtia vidole machoni katika yale mabadiliko batili ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010. John Pombe Magufuli, hii ni namba nyingine, huyu sio mtu wa mchezo mchezo au kuchezewa kama JK, hivyo CUF kama wanadhani watasusa na kubembelezwa, this time watakuwa wame bugi step, sasa hapa ni kazi tuu!.

Tutaulinda muungano kwa gharama yoyote!.

Pasco
Umetumwa au?kwanza umeandika kama ni mtoto wa chekechea hata hujui kupitia maandishi na kufanyia editing kama ni posho utapata tu,nenda taratibu watu tusome tukuelewe
 
Umetumwa au?kwanza umeandika kama ni mtoto wa chekechea hata hujui kupitia maandishi na kufanyia editing kama ni posho utapata tu,nenda taratibu watu tusome tukuelewe
Hivi unamjua Pasco ama unajifanya taahira? Kati ya Pasco na wewe Mmawia nani hadhi yake ni kubwa humu jf? Au kwa vile kaandika kitu ambacho kimekuchukiza? Pasco yupo upande wenu isipokuwa anaandika kutokana na hali halisi. Binafsi namkubali sana Pasco ijapokuwa tumekuwa tukikwaruzana katika mambo mengi hususan mapenzi yake kwa Lowasa
 
Pasco Maskiniii
Kutoshiri uchaguzi kwa CUF kinadharia inaweza onekana ni mwisho wa CUF. Lakini kwa siasa za Zanzibar zilipofika wana haja ya kutathmin nini wana kitaka. Je waridhie kushiriki chaguzi huku wakijua kuwa kamwe hawawezi shinda?
Yaani wao objective yao iwe ni ving'ora tu na kuishia kupewa nafasi za wizara nyepesi kwenye SUK huku washindani wao wakinawwir kwenye hatamu za uongozi?
Kwa wapenda demokrasia wote siasa zinazoendelea Zanzibar zikitiliwa mkazo na maneno ya kihafidhina ya kina marehemu bi Asha Bakari ya CCM hawawezi kuachia nchi kwa karatasi ni msiba mkubwa.
Mimi nadhhani CUF wana option muhimu katika kubadilisha hali hii..waridhie hali iliyopo na kisha waendeleze Ubwege wa kulalamika kama walivyoitwa hapo awwal...au wajipange upya kwa kuendelea kususia uchaguzi ili warudishe misingi imara ya demokrasia kuwa mshindi ndio atawale?
Kwa maoni yangu hii ndio option bora zaidi. Lazima status quo iliyokuwepo ambayo ni hatari zaidi ikomeshwe..na hapa hakuna haja ya kuangalia vyeo kwenye SUK ambayo kumbe formula yake iko pre-defined.
Maalim una kazi kubwa..lakini hili si la CUF peke yao..ni la wote wenye kuamini kwenye misingi ya demokrasia.
 
Wanabodi, baada ya kutangazwa tarehe ya uchaguzi wa visiwani Zanzibar,

Kuna watu wanadhani Chama cha Wananchi CUF, kina hiyari kushiriki uchaguzi huo au kutoshiri, as if kushiriki uchaguzi wa marudio ni jambo la hiyari!, watakuwa wanajidanya!. CUF hakina option yoyote ya kuamua ama ishiiki ama isishiriki, kwa sababu ushiriki wa uchaguzi wa marrudio sio option bali ni lazima kwa sababu kila kitu kiko vile vile kam,a mwanzo!.

Wenye option ya kuamua kushiriki au kutoshiriki ni wapiga kura, ndio wanaweza kuamua ama kujitokeza kushiriki kupiga kua, au kususa kupiga kura, na mgombea hata kama atapata kura moja ya ndio, ndio atatangazwa mshindi!, hivyo kupiga kura au kutopiga kura ndio bado ni option!, iwapo CUF itatangaza kususia uchaguzi huo, tangazo hilo ndilo litakuwa tangazo rasmi la kifo rasmi cha kilichokuwa Chama cha Wananchi CUF, kwa sababu majina ya wagombea wa CUF tatakuwepo kwenye karatasi za uchaguzi na hawatachaguliwa, hivyo kuipatia CCM ushindi wa mezani, ikiwemo kuivunja ngome ya CUF kule Pemba, kwa CCM kuvitwaa viti vyote vya Uwakilishi Zanzibarr na Pemba, ambapo pia huo ndio utakuwa mwisho wa SUK na CCM kutawala peke yake na kuhitimishwa kwa kifo rasmi cha chama cha wananachi, CUF!.

Nakiri kupandisha uzi huu kufuatia bandiko la mwana jf huyu
Zanzibarr sio nchi bali ni sehemu ya JMT, dhima ya muungano, ni undungu wa asili kati ya watu wa Tanganyika na Zanzibar, lakini sababu halisi ya muungano ni kuipatia Zanzibar ulinzi na usalama, Zanzibar haina polisi wala jeshi, hivyo jukumu la ulinzi na usalama wa Zanzibar, sio jukumu la Zanzibar, ni jukumu la JMT!. Hivyo CUF washirriki au wasuse, it will make no diference kwa sabau jukumu la ulinzi na usalama wa Zanzibar, ni jukumu la serikali ya JMT, chini ya Amiri Jeshi Mkuu, Drr. Jojm Pombe Magufuli.

Uchaguzi umetangazwa, utafanyika kwa amani na utulivu, mshindi atapatikana kwa haki, atatangazwa, ataapishwa na kuunda SUK nyingine, kwa uhuru kabisa bila`wasiwasi wowote!.

Hata hivyo kushiriki uchaguzi kugombea nafasi yoyote ni hiyari, pia kuamua kutokushiriki katika uchaguzi pia ni hiyari, sambamba na kujiandikisha kupiga kura ni hiyari, kutokujiandikisha pia ni hiyari, na kujiandikisha kupiga kura na kutokupiga kura pia ni hiyari, zote hizo ni demokrasia.

Kitendo cha CUF kushiriki uchaguzi wa mwanzo kunaifanya CUF ni lazima ishiriki uchaguzi wa maudio sio kwa hiyai bali kwa lazima. Hapa hakuna choice. Na iwapo CUF watasusana uchaguzi wa marudio, kususa huko kutakuwa ni kususa batili. kutakao ipatia CCM ushindi wa mezani, tena this time CCM itashinda viti vyote vya uwakilishi Unguja na Pemba, na huu ndio utakuwa mwisho rasmi wa CUF. Kamwe CUF isikubali kuingia katika mtego wa kususia uchaguzi wa marudio!.

Kikweli JK alikuwa ni mpole sana, hivyo Zanzibar imemchezea sana hadi kumtia vidole machoni katika yale mabadiliko batili ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010. John Pombe Magufuli, hii ni namba nyingine, huyu sio mtu wa mchezo mchezo au kuchezewa kama JK, hivyo CUF kama wanadhani watasusa na kubembelezwa, this time watakuwa wame bugi step, sasa hapa ni kazi tuu!.

Tutaulinda muungano kwa gharama yoyote!.

Pasco
Pasco, naomba kupingana nawe. Chama chochote kina option ya kujitoa kwenye ugombea wa nafasi fulani. CUF wanaweza kuiandikia tume na kujitoa kwenye uchaguzi. Pia,SUK inaundwa na mshindi wa kwanza na wa pili, CUF wasipokuwepo kuna chama kitakachofuatia kwa kura, hata kama kwa kura kumi. Kuvunjwa kwa ngome ya CUF pemba hiyo ni ndoto,kutokuwepo kwenye uchaguzi hakutaondoa harakati za kisiasa za CUF Zanzibar,wataendelea! 2005-2010,wawakilishi wa CUF walisusia Vikao vyote vya BW, haikuwafuta kwenye ramani ya siasa, and it was the same as if they had not participated in the election. Leo wamemtimua aliyekuwa mgombea kupitia ADC, Hamad Rashid, je! Ataebdelea kuwa mgombea?
 
Pasco Maskiniii
Kutoshiri uchaguzi kwa CUF kinadharia inaweza onekana ni mwisho wa CUF. Lakini kwa siasa za Zanzibar zilipofika wana haja ya kutathmin nini wana kitaka. Je waridhie kushiriki chaguzi huku wakijua kuwa kamwe hawawezi shinda?
Yaani wao objective yao iwe ni ving'ora tu na kuishia kupewa nafasi za wizara nyepesi kwenye SUK huku washindani wao wakinawwir kwenye hatamu za uongozi?
Kwa wapenda demokrasia wote siasa zinazoendelea Zanzibar zikitiliwa mkazo na maneno ya kihafidhina ya kina marehemu bi Asha Bakari ya CCM hawawezi kuachia nchi kwa karatasi ni msiba mkubwa.
Mimi nadhhani CUF wana option muhimu katika kubadilisha hali hii..waridhie hali iliyopo na kisha waendeleze Ubwege wa kulalamika kama walivyoitwa hapo awwal...au wajipange upya kwa kuendelea kususia uchaguzi ili warudishe misingi imara ya demokrasia kuwa mshindi ndio atawale?
Kwa maoni yangu hii ndio option bora zaidi. Lazima status quo iliyokuwepo ambayo ni hatari zaidi ikomeshwe..na hapa hakuna haja ya kuangalia vyeo kwenye SUK ambayo kumbe formula yake iko pre-defined.
Maalim una kazi kubwa..lakini hili si la CUF peke yao..ni la wote wenye kuamini kwenye misingi ya demokrasia.
Well. Umeandika vema. Ila kwa upande wangu nakubaliana na Pasco. CUF hawana option nyingine zaidi ya kushiriki uchaguzi. Kumbuka uhai wa chama cha siasa upo kwenye kushiriki uchaguzi. Kama chama hakishiriki uchaguzi maana yake ni kwamba kimejiondoa chenyewe kwenye siasa. CUF wakithubutu kufanya hivyo ndo tutakuwa tumewazika rasmi
 
Njaa ni kitu hatari sana ! yaani pasco unajidhalilisha kwa kiwango hiki ! kwa bei gani uliyolipwa ? huwezi kufuta cuf kwa kusimika wabunge wa uongo pemba , yalitokea haya siku za nyuma .
 
Hivi unamjua Pasco ama unajifanya taahira? Kati ya Pasco na wewe Mmawia nani hadhi yake ni kubwa humu jf? Au kwa vile kaandika kitu ambacho kimekuchukiza? Pasco yupo upande wenu isipokuwa anaandika kutokana na hali halisi. Binafsi namkubali sana Pasco ijapokuwa tumekuwa tukikwaruzana katika mambo mengi hususan mapenzi yake kwa Lowasa
pasco huyu mganga njaa ndio wa kumtisha naye humu ? Nimekudharau sana .
 
Back
Top Bottom