msem
JF-Expert Member
- Nov 7, 2015
- 1,832
- 1,627
Mkuu uko sawia,wasiposhiriki watakuwa wamejiweka mlalo wa mende,ni vyema wakaliangalia hili kwa makini.Wanabodi, baada ya kutangazwa tarehe ya uchaguzi wa visiwani Zanzibar,
Kuna watu wanadhani Chama cha Wananchi CUF, kina hiyari kushiriki uchaguzi huo au kutoshiri, as if kushiriki uchaguzi wa marudio ni jambo la hiyari!, watakuwa wanajidanya!. CUF hakina option yoyote ya kuamua ama ishiiki ama isishiriki, kwa sababu ushiriki wa uchaguzi wa marrudio sio option bali ni lazima kwa sababu kila kitu kiko vile vile kam,a mwanzo!.
Wenye option ya kuamua kushiriki au kutoshiriki ni wapiga kura, ndio wanaweza kuamua ama kujitokeza kushiriki kupiga kua, au kususa kupiga kura, na mgombea hata kama atapata kura moja ya ndio, ndio atatangazwa mshindi!, hivyo kupiga kura au kutopiga kura ndio bado ni option!, iwapo CUF itatangaza kususia uchaguzi huo, tangazo hilo ndilo litakuwa tangazo rasmi la kifo rasmi cha kilichokuwa Chama cha Wananchi CUF, kwa sababu majina ya wagombea wa CUF tatakuwepo kwenye karatasi za uchaguzi na hawatachaguliwa, hivyo kuipatia CCM ushindi wa mezani, ikiwemo kuivunja ngome ya CUF kule Pemba, kwa CCM kuvitwaa viti vyote vya Uwakilishi Zanzibarr na Pemba, ambapo pia huo ndio utakuwa mwisho wa SUK na CCM kutawala peke yake na kuhitimishwa kwa kifo rasmi cha chama cha wananachi, CUF!.
Nakiri kupandisha uzi huu kufuatia bandiko la mwana jf huyu
Zanzibarr sio nchi bali ni sehemu ya JMT, dhima ya muungano, ni undungu wa asili kati ya watu wa Tanganyika na Zanzibar, lakini sababu halisi ya muungano ni kuipatia Zanzibar ulinzi na usalama, Zanzibar haina polisi wala jeshi, hivyo jukumu la ulinzi na usalama wa Zanzibar, sio jukumu la Zanzibar, ni jukumu la JMT!. Hivyo CUF washirriki au wasuse, it will make no diference kwa sabau jukumu la ulinzi na usalama wa Zanzibar, ni jukumu la serikali ya JMT, chini ya Amiri Jeshi Mkuu, Drr. Jojm Pombe Magufuli.
Uchaguzi umetangazwa, utafanyika kwa amani na utulivu, mshindi atapatikana kwa haki, atatangazwa, ataapishwa na kuunda SUK nyingine, kwa uhuru kabisa bila`wasiwasi wowote!.
Hata hivyo kushiriki uchaguzi kugombea nafasi yoyote ni hiyari, pia kuamua kutokushiriki katika uchaguzi pia ni hiyari, sambamba na kujiandikisha kupiga kura ni hiyari, kutokujiandikisha pia ni hiyari, na kujiandikisha kupiga kura na kutokupiga kura pia ni hiyari, zote hizo ni demokrasia.
Kitendo cha CUF kushiriki uchaguzi wa mwanzo kunaifanya CUF ni lazima ishiriki uchaguzi wa maudio sio kwa hiyai bali kwa lazima. Hapa hakuna choice. Na iwapo CUF watasusana uchaguzi wa marudio, kususa huko kutakuwa ni kususa batili. kutakao ipatia CCM ushindi wa mezani, tena this time CCM itashinda viti vyote vya uwakilishi Unguja na Pemba, na huu ndio utakuwa mwisho rasmi wa CUF. Kamwe CUF isikubali kuingia katika mtego wa kususia uchaguzi wa marudio!.
Kikweli JK alikuwa ni mpole sana, hivyo Zanzibar imemchezea sana hadi kumtia vidole machoni katika yale mabadiliko batili ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010. John Pombe Magufuli, hii ni namba nyingine, huyu sio mtu wa mchezo mchezo au kuchezewa kama JK, hivyo CUF kama wanadhani watasusa na kubembelezwa, this time watakuwa wame bugi step, sasa hapa ni kazi tuu!.
Tutaulinda muungano kwa gharama yoyote!.
Pasco