Elections 2015 CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake

HAKUNA KAFIRI HATA MMOJA ANAYEITAKIA MEMA ZNZ AU UISLAMU, huo ndio ukweli hata wakipinga watu wa dunia nzima. PASCO yumonkatika kundi hilo hata kama atakuwa mchambuzi mzuri , hatoki katika kapu hilo, chuki, fitna na dharau kuona kwamba haiwezekani kuwaachia watu wengine waongoze, ndipo tutakapo waua na kulinda maslahi yetu kwa hali yoyote ile (Tutaulinda muungano kwa gharama yoyote).
.
Mkuu Dangadunguri, tunapojadili siasa, tujadili siasa na sio kuchanganya hoja za siasa na udini, kwa nini tuuchukie Uislamu?!, pamoja na tofauti zetu za kidini, sisi ni wamoja!, lazima tujifunze kukubaliana, kuvumiliana, kustahiliana na tukishindwa kabisa kukubaliana, then tunakubaliana kutokukubaliana!,haya mambo ya kuitana makafiri ni kama kututukana!. Tanzania ni nchi ambayo haina dini, lakini watu wake wana dini zao, dini kuu zikiwa mbili, Waislamu iliyoletwa na Waarabu, na Ukristo ulioletwa na wakoloni wazungu, wote hao walipokuja walitukuta tuna dini zetu za asili wakatufunza dini zao, na kuziona ndio bora, zile dini zetu za asili wakatuita wapagani na dini zetu wakaziona ni za kishenzi, dini zao ndio bora. Kitendo chaa kumuita mtu kafiri ni cha kibaguzi, na kujionyesha dini ndio bora huku unaelewa wazi kila mtu ana dini yake kama sio Mkristo ni Muislamu au anayefuata dini yake ya asili, hivyo hili suala la ukafiri linatokea wapi?!.

Mimi ni Mkristo lakini ninawaunga mkono Waislamu katika hoja ya Mahakama ya Kadhi-
Mwarobaini wa Kweli wa Mahakama ya Kadhi ni Huu,
Pia kwenye hoja ya OIC, mimi ni Mkristu lakini niliunga mkono hoja ya Tanzania kujiunga OAC
Magobe T,
  1. ni kweli, unapoahidiwa kitu, kipindi chote cha kusubiria, lazima uwe mpole. Kabla ya ahadi hizo, hao ndio waliokuwa mstari wa mbele kuichachafya serikali.
  2. Kilichofanyika katika Ilani ya CCM, kilikuwa danganya toto kwa jina ya 'engenging the Muslim community'. Lakini kwa vile walipewa legitimate expectation, hata kama lengo halikuwa kweli, lakini sasa litabidi liwe kweli vinginevyo hako mbeleni hakutakalika.
  3. Mimi ni Mkatoliki Die Hard, lakini nawaunga mkono ndugu zetu Waislamu kweli hili la Mahakama ya Kadhi hata kwenye la IOC kwa upande wa Zanzibar.
  4. Uganga ni member wa IOC na pia anayo mahakama ya Kadhi.
  5. Kabla ya uhuru mpaka tunapata uhuru, tulikuwa na Mahakama ya Kadhi, haina problem kwa isiyowahusu.
  6. Jamii ya Hindu, wanayozo mahakama zao, Sunni wana mahakama zao, Ismailia wana mahakama zao na Singasinga pia wana mahakama zao. Kamwe huwezi kusikia kesi mahakama za kawaida wahindi wanadaiana, ukuina tuu imetinga mahakamama zetu, ujue one part sio mwenzao.
  7. Nadhani hata sisi tuna mahakama zetu za mambo ya ndoa, ambazo hukutana kila Alhamisi pale St. Joseph, uzuri wetu sisi, ni upatanisho tuu, hatuvunji ndoa kamwe!.
  8. Na kama zikianza, zitawahusu Waislamu tuu ambao wataridhia kutumia sharia law kwa ridhaa zao wenyewe bila kulazimishwa.
  9. Ikitokea ndoa ya Muislamu na asiye Muislamu, sheria za nchi ndizo zitatumika.
  10. Nasisitiza, waacheni wapate wanacholilia as long as serikali haitazigharimia wala kuwaingilia. Sio vizuri kuwadanganya wenzenu kama danganya toto, watafika mahali wakate tamaa na kuamua kufanya lolote, tusije tukajiundia katawi ketu cha Al-Shabab na Al-Qaeda!.

Tukija kwenye suala la Muungano na kuulinda kwa gharama yoyote, hapa ndipo ninapotofautiana na wengi. Nikiwarudisha nyuma katika maumbile ya nchi, Visiwa vyote vya bahari jirani na nchi kavu vilikuwa ni sehemu ya hiyo nchi kavu kabla ya kumeguka miaka milioni nyingi nyuma, hivyo visiwa vya Zanzibar ni sehemu halali ya Tanganyika, ni mali ya Tanganyika, hivyo Tanganyika kuhakikisha unaulinda muungano kwa gharama yoyote ni fulfillment of its duty.

Waarabu wakiongozwa na Sultan Seyyid Said, ile mwaka 1832, walivivamia visiwa vile na kuvitwaa kana kwamba wameviokota na havina mwenyewe, ambapo Sultan Said akaifanya Zanzibar kuwa makao makuu yake, bila kuwashirikisha wenyeji aliowakuta pale aliwaona ni sawa tuu na manyani na ngedere.

Mwaka 1884 wakati wakoloni wanagawana bara la Afrika kama mali mali yao, walimtambua Sultan wa Zanzibar na kungawia visiwa hivyo na ukanda pwani wa maili 10, chini ya ulinzi wa Muingereza, hivyo Mwarabu kujihalalishia visiwa vya Zanzibar kama halal yake.

Mwaka 1963 Muingereza akatoa uhuru wa bandia kwa Sultan na vibaraka wake, na ndipo Januari 12, mwaka 1964, wenye nchi yao, wakafanya Mapinduzi Matukufu, wakavitwaa visiwa vyao toka kwa Sultan mvamizi, ila kwenye mapinduzi yale. hawakuwatimua Waarabu, ila waarabu walikimbia wenyewe!.
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa!.
Shujaa Mkuu wa Mapinduzi Sheikh Abedi Amani Karume, akaomba ulinzi kutoka kwa Tanganyika, ili kuhalalisha nchi huru moja kuilinda nchi huru nyingine, bila ya kuonekana ni uvamizi, ikabidi Tanganyika na Zanzibar ziungane fasta fasta hapo Aprili 26, 1964.
Hivyo kwa sehemu moja, muungano unaipatia ulinzi Zanzibar, lakini kwa sehemu ya pili, muungano umeirudisha sehemu halali ya Tanganyika chini ya milki yake, hivyo lazima ulindwe kwa gharama yoyote maani ni mali yetu halali!.

Pasco
 
Jecha alipofuta uchaguzi ni nani alikuwa amejaza fomu ya malalamiko?
Paschal jiongeze, kama kusoma hujui basi hata picha huoni?.
Paskali jibu hili swali

Unapigwa na pacha mmoja unaenda kumshtakia kwa pacha mwenzie?
Mkuu Gamba la Nyoka, msimamo wangu kuhusu kilichotokea Zanzibar uko wazi kabisa, Jecha hakuwa na mamlaka yale ya kujiugeuza ZEC, alichofanya Jecha ni kitendo haramu, lakini ili haramu iwe ni haramu kweli, lazima iharimishwe, haramu isipoharimishwa hugeuka halal!. Kwa vile ile haramu ya Jecha haikuharimishwa, hivyo ikahalalishwa na uchaguzi wa marudio.

Pia nikatolea mfano wa kubakwa. Kubaka ni kosa la jinai, lakini ili liwe kosa, lazima anayebakwa alalamike, mwanamke akibakwa asipolalamika, na akabakwa tena na tena, atahesabika ameridhia, hivyo Wazanzibari katika umoja wao, wameridhia unakaji huu wa demokrasia Zanzibar, kwa sababu hakuna yoyote aliyelalamika rasmi, kulalamikia kwenye media sio utaratibu rasmi wa kuwasilisha , malalamiko.

Kuhusu hili la Zanzibar, mimi mwenyewe tuu nimepandisha nyuzi Zaidi ya 10 na hizi ni baadhi tuu.
  1. Zanzibar: Kama Maalim Kajitangazia Ushindi, kwa nini hajashitakiwa? Jecha Kapata Wapi Mamlaka ile?
  2. Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda
  3. Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua hatua zozote
  4. Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar?
  5. Zanzibar: Japo SMZ ya SUK sio de jure tena bali ni de facto, lakini ipo!, na hakuna aliyejiuzulu!
  6. CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake
  7. Hatimaye CUF 'Wameridhia' Rasmi, Kushiriki Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar!.
  8. Uchaguzi wa Marejeo Zanzibar ni Huru na Haki! Tuyasubiri Matokeo, Tuyakubali!
  9. Jee Kuna Uwezekano Siku Zote Huwa Hazitoshi, Bali Zinatosheshwa?!. Utosheshaji Ulipogoma, Ukafutwa?!
  10. Uhalali wa Rais Dr. Shein Wa Zanzibar ni Kutokana na Uchaguzi Halali, Huru na Wa Haki! .
  11. Ukweli Mchungu Zanzibar: Hakuna Mgogoro Wowote wa Kisiasa, Shein ni Rais Halali, Uchaguzi ni 2020!
  12. Pemba Chini ya CCM kuneemeka au Kujutia Kuichagua CUF Chaguzi Zilizopita?!
  13. Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!
Paskali
 
Back
Top Bottom