CUF kuiga sawa, lakini hata hili la kushika kichwa? Mmetisha!

Hivi huyu ITATIRO alikuwa TAHLISO? Mwenyekiti wa TAHLISO wa sasa anagombea uenyekiti wa taifa UVCCM!!? TAHLISO ni shina la MAGAMBA? Huko CUF ni "MSHENGA" wa MAGAMBA? Tafakari

Ndugu yangu kuhusu TAHLISO, ni ngumu sana kwa mtu asiye CCM kukiongoza.Huwa kunakuwa na kashkash sana na kuingiliwa na vijana wa Usalama. Wakati mwingine wajumbe wa uchaguzi (maraisi wa vyuo vyote as potential members), kama kuna mtu asiyeeleweka vizuri kichama (CCM) au anayeonekana kakaa kimapinduzimapinduzi huwa anapata wakati mgumu sana. Nakumbuka kuna jamaa yangu mmoja aliwahi kunieleza yeye na wenzake walishafuatwa na vijana wa Usalama kuwatahadhalisha yeye na marafiki zake ili wajiepushe kumpigia kura kiongozi fulani kuwa raisi wa TAHLISO kwa kuwa alikuwa hakubaliki katika jicho la serikali.
Kwa hiyo hapo kaka, vijana wengi ambao ni viongozi wa TAHLISO lazima wawe ni CCM na wakikua kidogo wanagombea uenyekiti wa Taifa UV-CCM, au wanapewa ukuu wa wilaya, n.k
Usidhani ni coincidence...mambo yote yanapangwa na kuhakikishwa yanatokea!
 
Wao hata ibada kwao ni act na mizaha.Hizi si sifa za Mungu Aliye hai,Mungu anayependa waabuduo ktk roho na kweli.Sasa sala zao Feki ni chukizo mbele ya Mwenyezi Mungu.CDM wanaingiza Mchungaji na Sheikh wa Kweli wanaojua wanamwomba nani naye aombwaye anajua wamwombao na wakiombacho.

Walio waaminifu kwa Mungu wanaomba sana ktk nchii hii ndio maana mipango ya CCM inatibuka bila wao kujua.CDM kusimamia kwao ktk kweli ndio salama yao.Siku wataiacha hii kweli mambo yatakwenda mrama sana.

CUF mungu wenu mfu bado anawavuta palipo kifo.
 
KWa vile viongozi walibaki AR hadi jana nadhani waliona Lema akiwa mjini panakuweje?Wakawafundishe wapemba na hiyo.Wao si masultani?
 
Mimi ninaitakia mema nchi yangu Tanzania lakini kwa aina hii ya upinzani dhidi ya upinzani nina wasiwasi na safari ya kuikomboa Tanzania. Wakati tu ndio ndio utakaotufanya tutafakari na kujua tulipojikwaa ingawaje inasemwa kuwa "binadamu ndie mnyama pekee anayejikwaa kwa jiwe hilo hilo mara kadhaa".
 
Cuf ilishakufa siku nyingi huku bara inafanya kazi kama idara ya ccm lao moja huwezi kuwatofautisha kwa sababu wote wanapambana na cdm.
 
Mkuu hebu nikumbushe siku ya mapokezi ya Lipumba pale airport Dar, Dr. Slaa alikuwepo kumpokea Prof. Lipumba kwa vishindo inawezekana Dr. Slaa huyohuyo ndiye aliyeratibu ujio wa CUF Arusha; siasa za bongo zimetawaliwa na viini macho. CUF na Chadema wote ni mabingwa wa maandamano sasa sijui mlaumiana kitu gani; CCM ni chama huru tutawakaribisha wapinzani wanaokubaliana na sera zetu za kumuendeleza mtanzania.

Chama
Gongo la mboto DSM
Ndugu nakupa ushauri wa bure,hebu achana na siasa za fitina,ubaguzi etc,tuongelee ukombozi wa taifa letu,tunahitaji siasa safi za kuwasaidia wananchi wanaotaabika kila uchao,fikiri na chukua hatua,
 
Hii ndoa na CCM itawatesa sana hawa jamaa.

Nikikumbuka mbunge wao Mh. Magdalena Sakaya alivyokamatwa wakashindwa kumtoa wala kukemea sababu tu waliomkamata ni wabia wao (serikali ya ccm) nakosa la kusema.

Kwa ajili ya ndoa fake wanamtosa mpaka mwenzao.
 
Naona CUF na Chadema wanapambana baada za kuchonganishwa na CCM.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom