chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,968
Wanachama wa Chama cha wananchi CUF wamepanga kufanya maandamano makubwa Dar ili kushinikiza aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Ibrahim Lipumba kupewa uenyekiti wa chama,
Wamesema wanamuunga mkono Lipumba kurudi kwenye nafasi ya uenyekiti na wapo tayari kwa gharama yoyote ile hata kama ni maisha yao lakini Profesa Lipumba awe mwenyekiti mpaka mwaka 2019 na wamechoka kuburuzwa na watawala wa Zanzibar.
Wameshangaa naibu katibu mkuu wa CUF Mazrui kutoa msimamo wake wakati chama bado hakijakaa na kutoa taswira kuwa huo ndio msimamo wa viongozi wengine kama Maalim Seif na Jussa