CUF kuandamana nchi nzima

Hapo wanawadanganya wenzao wakiamini watawakomboa lakini wanaporudi kwenye mishahara mpaka ipite miezi mitatu maji umeme ni kwenye nyumba za wahafidhina tu,mahospitali ndio hivyo mende wamewashinda kunguni ,usije ukajaribu kufungua droo unaweza ukaona upo katika kideo kwa mende wanavyohangaika kutafuta nafasi ya kukaa.Maana wangejiuliza iweje raisi mkewe awe ni muarabu bibi wa raisi muhindi ,hapa ndipo walipo wahafidhina wakiwakusanya wafanyakazi wa serikali na wanafunzi ndipo mkutano unapotimia la si hivyo basi watabaki na meza matuta na minazi wakiihutubia.

Halafu wanasema wenzetu weusi
Huu uweusi upomidomoni mwaotu na ukienda majumbani utakuta weupemtupu?
Lakini kwa mtizamo wangu ni kuwa wanzibar hajayao ni maendeleo au maisha bora kama mkuu mwenzangu alivyo ahidi,si pemba wala unguja na huko pemba kama wccm wangali wafanyia mazuri hao na kuonyesha kuwajali pamoja na kwamba ndio hakuichagua ccm basi mimi ninafikiria wasinge pata taaabu saana ya kumfikiria seif jinsi gani ya kumporomosha kisiasa dunia ya leo ni watu kuwa na uhakika wa kuala yake tu na akiumwa na mbu wapi atapata kidonge hayo mengine baadae,
Lakini wanasema sefu anachuki au ni muarabu na wapemba wake mbona wakati walipo uliwa wapemba hawakukimbila oman au saudia?au hiyo serikali ya oman au iran ilisema nini kuhus hao ndugu zao wa kipemba?
UCHAGUZI ULIO HURU NA HAKI NDIO SUUHISHO LA MATATIZO YA ZANZIBAR.
 
Kada nashukuru kuwa unaleta argument nzuri na umeacha yale mambo ya ubishi wako na mwafrika wa kike na kuharibu mada bila sababu.

Katika hili, Huwezi kusema kuwa viongozi wa CUF wanaongozwa na Oman bila kuwa tayari kusema viongozi wa ccm wanaongozwa na nani. Huwezi kusema mambo ya CCM baadhi tu na kuyaacha mengine. Ningesema uongo kuwa ccm wameuza migodi na madini ya watanzania basi ungesema kuwa ninachanganya madawa.

CCM ni ile ile bara na visiwani, je unapinga hili?

oh no you didnt ! Ungenikuta kwenye prime hapa JF mwanzoni nafikiri ndio ungemjua the real kada ! Sometimes i do agree that i had to be that way, and situation caused it, sometimes i wanted to be even rougher than that but fate only prevented it !

Haya turudi kwenye topic !
 
CUF hawautaki mseto hata kuuona hiyo ndio imeshatoka wandugu ,na ndio mnaona kasi wanayoondokea CUF kama mnasema ni chama cha wapemba basi ndio hivyo hao hawasikii kitu tena ,mtabaki njooni tukae wameitega CCM na CCM imetegeka ,CUF ni wakali wa siasa,maana wameshaondoka na kila mtu na kuwawacha CCM mapepe ,sasa hivi kila kona ya dunia ina mawazo ya kuwa CCM ndio mbaya na huna pa kupita. Nasema hilo jambo ndio limeshatoka ,walala hoi wanasema imetoka hio !!!
Mheshimiwa naona sasa umeeleza ukweli. Hakika hii ndiyo dhamira ya CUF. Sasa nani asiyetaka huo muafaka. Sawa na tusubiri Wenzao wameshika mpini. Wao wameshika makali. Hivyo, hao wa nje, unafikiri ni mazuzu, kila siku watakuwa wanasikiliza hadhithi za alnacha za CUF tu?
 
Kasheshe,

Mzee wangu vipi leo, wengi hapa tumejua kilichotokea Butiama. Wengi hapa tumejua kuwa CUF na CCM walikubaliana kwenye kikao cha muafaka na kwenye meza ya marudiano na vyama vyote vikapeleka makubaliano kwenye vikao vya chama. Yaliyotokea ni kama ifuatavyo:

1. CUF wakapitisha rasimu ya makubaliano hence report ya BBC

Hawakutakiwa kwenda BBC. Nilishaelekeza kwamba walikua na MOU... ya kutofanya hivyo.

2. CCM wakakataa mambo Butiama na wakataka kuanza maigizo.

Hii spinning ya kuwageuzia CUF inaweza kufanikiwa kule kijiji cha matembele lakini sio jambo forums.
CCM hawakukataa wametoa mapendekezo zaidi ya kuboresha... vipi mheshimiwa?
 
Hawakutakiwa kwenda BBC. Nilishaelekeza kwamba walikua na MOU... ya kutofanya hivyo.

CCM hawakukataa wametoa mapendekezo zaidi ya kuboresha... vipi mheshimiwa?

Kulingana na ile story ya BBC, CUF walifanya kikao cha kawaida kama kile cha CCM Butiama. Wana CUF wakaamua kukubaliana na muafaka na wakaviambia vyombo vya habari walichoamua, je kuna makosa katika hilo?

Tofauti na CUF, ccm wao wakakaa kikao Butiama, wakafukuza vyombo vya habari (talk about transparency) wakati wa mjadala wa suala la zanzibar, hata hivyo bado habari zikaleak kuwa wamekataa huo muafaka walioutumia miezi kumi na nne kuutafuta. Nani hapa wa kulaumiwa, CUF waliokubali muafaka au CCM walioukataa?
 
“Hatuwezi kuondoa hoja hiyo kwa sababu hilo ni wazo la NEC. Mimi naendesha mazungumzo kwa niaba ya chama chetu na NEC ndiyo yenye uamuzi wa mwisho,” alisema Makamba.

Makamba alisema kama alivyosema Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete Jumanne iliyopita, sahihi ya yeye Makamba na ya Katibu Mkuu wa CUF Seif Sharrif Hamad hazitoshi bila uamuzi wa ngazi za juu za vyama hivyo.

Alisisitiza kuwa,”Makubaliano hayawezi kufikiwa hadi wananchi wa Zanzibar watoe maoni yao kupitia kura ya maoni.” Makamba pia alikanusha maelezo ya CUF kuwa vyama hivyo vilikuwa vimefikia hatua ya mwisho ya kutia saini makubaliano ya Mwafaka kwa kusema bado vyama hivyo vipo katika ngazi ya mazungumzo.

“Mimi nashangaa watu wanasema tumefikia makubaliano, makubaliano gani hayo? Sisi (CCM na CUF) hatujatoa tamko rasmi la kufikia makubaliano kwa sababu mazungumzo bado yanaendelea,” alisema Makamba.

Katibu Mkuu huyo alisema yeye anachofanya ni kusubiri barua ya majibu kutoka CUF, ambayo aliwaandikia kuwaomba wakutane ili awaeleze nini NEC imeamua. Alisema hadi sasa yeye hajapokea barua kutoka CUF kumjulisha kama watarudi kwenye mazungumzo.

“Mimi niliwaandikia barua na wenyewe inabidi wanijibu nipeleke kwenye chama changu halafu tukutane tuzungumze. Kama hawataki au wanataka waniandikie mimi bado sijapata msimamo wao,” alisema Makamba.

Chama cha CUF kilishatoa msimamo wake kupitia Profesa Lipumba juzi akisema hawatakuwa tayari kuendelea na mazungumzo endapo CCM haitaondoa hoja ya kufanya kura ya maoni Zanzibar.

Habari zaidi ....
 
“......

“Mimi nashangaa watu wanasema tumefikia makubaliano, makubaliano gani hayo? Sisi (CCM na CUF) hatujatoa tamko rasmi la kufikia makubaliano kwa sababu mazungumzo bado yanaendelea,” alisema Makamba.

.......

Habari zaidi ....

Kulingana na haya maelezo ya Makamba, inaonekana kuwa kumbe hakuna chochote walichokubaliana. Hii story kuwa CUF wamekataa muafaka imetoka wapi?
 
Kulingana na ile story ya BBC, CUF walifanya kikao cha kawaida kama kile cha CCM Butiama. Wana CUF wakaamua kukubaliana na muafaka na wakaviambia vyombo vya habari walichoamua, je kuna makosa katika hilo?

Tofauti na CUF, ccm wao wakakaa kikao Butiama, wakafukuza vyombo vya habari (talk about transparency) wakati wa mjadala wa suala la zanzibar, hata hivyo bado habari zikaleak kuwa wamekataa huo muafaka walioutumia miezi kumi na nne kuutafuta. Nani hapa wa kulaumiwa, CUF waliokubali muafaka au CCM walioukataa?

Ndugu yangu rafiki yangu, mpenzi Mwafrika wa Kike... kwanza ni muhimu urudi nyuma kwanza kwenye mambo waliokubaliana kwenye uendeshaji wa hiyo mikutano yao... ukilijua hilo utajua kiwingu kililetwa na CUF. kumbuka haya yalikuwa yofanyika kabla ya hapa...
 
Unajua Kasheshe najaribu sana kukuamini na kuja upande wako. Mimi ni kati ya wale wasiopenda mauaji yanayofanywa na polisi na jeshi dhidi ya watu wa pemba. Nachukizwa na sipendi kabisa kuona siasa ikiingizwa kwenye sehemu ambayo kuna hatari ya kupoteza maisha ya watu.

Vile vile sipendi spinning za kuwaharibia wenzenu kama vile kina .... wanavyojaribu kukipaka chama cha CUF kuwa chama cha fujo. Sifurahishwi pia na spinning ya kusema kuwa CCM wanalinda maslahi ya weusi huko unguja na wakati CUF wanalinda maslahi ya Oman.

Pamoja nakusema haya, nimesubiria sana uweke hiyo MOU hapa au hayo makubaliano hapa kuonyesha nini unajua ambacho mimi sijui lakini holla.

Tafadhali onyesha makubaliano ambayo CUF wamekiuka tofauti na kile tunajua kilitokea Butiama!
 
Mkulu Kasheshe,

Good job, maana elimu nzito sana unayomwaga hapa so far kuhusiana na hii ishu, na you have the command kutokana na ze dataz pia, endelea tu kutuhabrisha yaliyojiri kwenye muafaka,

Wakuu wenzangu wa upande wa pili, si mnakumbuka jinsi Savimbi, alivyokuwa mwiba wa aamani kule Angola, sasa na Seif naye ndiye hasa mwiba wa muafaka.
 
Jamani FMES,

Be fair to the guy. Mimi namheshimu sana Seif kwa vile hajawahi kuanzisha vita huko Zanzibar. Nina hakika kabisa kuwa Seif angekuwa mtu wa vita, angekuwa alishaanzisha vita tokea miaka yote hiyo aliyosumbuliwa na ccm.

Kwa hili sidhani kama Maalim Seif ni kama Savimbi!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom