Kasheshe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2007
- 4,694
- 787
2. Nimesoma neno kwa neno rasimu ya makubaliano ya CUF na CCM ambayo ilishakubaliwa na kamati zote mbili. Suala la serikali ya pamoja linapaswa kutekelezwa kabla ya mwaka 2010.
3. Nimesoma ripoti ya Kamati ya CCM iliyopeleka Butiama kwa ajili ya Kamati Kuu na baadaye halmashauri Kuu; ukweli ni kuwa hoja ya kura ya maoni haikuzuka kikaoni- iliandaliwa kabla kwa pendekezo la Karume na kukubaliwa na wanakamati. Pamoja na uzuri wa dhana ya kura za maoni, lakini nia(motive) yake hapa si nzuri! Kwa serikali ambayo haifanyagi referendum katika masuala muhimu kihistoria kama Muungano, Katiba, Mfumo wa Vyama vingi, kumuundoa Rais wa Zanzibar kama makamu wa Rais(ambalo lilikuwa ni suala katika makubaliano mama ya muungano); inatia shaka serikali kama hiyo itakapo suala la kura za maoni Zanzibar. Ni Kikwete huyu huyu ambaye alipokwenda Kenya hakutaka wakina Raila na Kibaki wafanye kura za maoni, akata wasaini makubaliano na kuyatekeleza. Wakati wa kuibwa kwa kura hakuitishwa kura za maoni, kosa moja haliwezi kuhalalisha kosa, lakini kosa moja linaweza kutoa ishara ya kosa lingine! Kwa ujumla ukiisoma ripoti hii ya Kamati ya CCM; ukisoma na Barua ya Mwisho ya Makamba; utagundua kuwa Makamu Mwenyekiti Msekwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete- hawakusema kweli wakati wakieleza mchakato wa Maazimio ya NEC ya CCM na Matokeo yake!
4. Nilikuwepo Diamond Jubilee jana na nimemsikiliza Lipumba toka mwanzo mpaka mwisho. Nilichokielewa ni kwamba CCM imekuwa ikiwatapeli CUF toka baada ya uchaguzi, ikiwafanyia unafiki wa hali ya juu- CUF nayo kwa upande wake ilikuwabali ku-give in too much; ikakubali ghilba za aina zote ikiwa na matumaini makubwa kwamba Kikwete yuko genuine! Na kwa kiasi kikubwa mambo yote haya yalifanyika kwa siri ya pande mbili; kwa mategemeo makubwa ya CUF kwamba pengine serikali ya mseto ingetokea. Kumbe CCM wakati wote ilikuwa ikiweka kadi chache mezani na nyingine nyingi zaidi kuzificha chini ya meza.Ukiangalia mtiririko wa matukio katika hii miaka mitatu kuhusu Zanzibar utagundua ama Rais Kikwete anafanya unafiki wa hali ya juu wa kisiasa, au ni kiongozi dhaifu katika CCM kama mwenyekiti anayezidiwa nguvu na makundi mengine ndani ya chama chake. Kwa vyovyote vile, hali hii ikiachwa bila panga kuitwa panga na si kisu kikubwa ni ishara mbaya kwa utangamano wetu kama taifa haswa kwa kuwa kwa sasa CCM ndicho chama tawala!
5. Tunaungana mkono na CUF katika hili, kwani kitisho cha demokrasia mahali Fulani ni kitisho cha demokrasia mahali pote. Maandamano ya jumamosi, hayapaswi kuwa maandamano ya CUF, yanapaswa kuwa maandamano ya umma! Ama hakika, uwongo una mwisho- lakini ukweli unapaswa husimama milele, na ukweli hauna itikadi. CUF wanaweza kuwa walijikwaa mahali Fulani katika mchakato huu; lakini sasa ni wakati wa kutazama mbali zaidi, kutazama picha kubwa zaidi- CCM ikiwachwa ikapita katika hili, itandelea kuacha na ufisadi mwingine ukatawala kwenye RICHMOND, BOT nk na hatimaye kuweka misingi ya ufisadi wa kudumu zaidi katika uchaguzi mkuu 2010. Hatupaswi kuacha utadamuni wa ufisadi, usanii wa kisiasa, uchezeaji wa haki, na wananchi kukaaa pembeni kama watazamaji na wanyooshaji vidole kuendelea katika taifa letu. Ni wakati mwingine wa kuandelea kuchukua hatua!
JJ
PS:
• Mwenye Hotuba ya Jana ya Lipumba atuwekee hapa tafadhali
• Mwenye rasimu ya makubaliano ya CUF na CCM iliyokubaliwa na kamati za pande mbili aiweke hapa pia tafadhali
John Mnyika;
Inasikitisha sana kuunga mkono wenzenu kurudi back to sqaure one; wakati walikuwa wanaelekea kwenye makubaliano... Najua hii ni sawa kwako na akina Lipumba kwa sababu hakuna unachokosa tukirudi nyuma tena...! Ni waZanzibar wanatamani mjadala huu uendelee uishe.... wewe na propaganda zako munaona kwamba muafaka utapatikana mtakosa ya kutokea kwenye majukwaa mshindwe kwa jina... na mlegee kabisa...
Ni uzembe wa hali ya juu sana tatizo la miaka mingi kulifanya la emergency kama ilivyokuwa Kenya... I'm sorry there must be a problem of IQ somewhere...
Kenya haikushauriwa kwenda kwa Wananchi kwa kura ya maoni kwa sababu mazingira hayo yangeleta machafuko zaidi...(hili lilisemwa wazi hata sisi tusiokuwa tuna-practise siasa kama wewe tulijua hilo)
Watu kama John Mnyika kweli ndio mwanasiasa wa kukabidhiwa nchi kwa uchambuzi wako dhaifu kiasi hiki.
Ati Kikwete ni dhaifu... unafahamu maana ya Rais na maana ya Mwenyekiti wa Chama... You seem not to be serious at all... Kama munaburuzwa na Mbowe CCM kuna vichwa huwezi buruza tu ndugu yangu... NEC ya CCM imesheheni watu makini mkuu!!!
Narudia tena kwa kuwa hakututumia kura ya maoni huko zamani... hata sasa ambapo demekrasia ni dhana muhimu ya utawala bora tusitumie... huu ni uvivu wa kufikiri...
Alafu ulazima wa kufanya kabla ya 2010 ni upi.... mimi nadhani katiba yes itabadilishwe kabla 2010 ili baada ya uchaguzi serikali ya mseto ndio iundwe...