CUF kuandamana nchi nzima

duh! watu kweli kiboko, habari ambazo hata hazijaandikwa kwenye magazeti watu wanazo, na hao critics wa ccm sidhani kama wangekaa kimya kama wangesikia haya ! so, that cant be !

Nilichosema hapa hakina tofauti na kinachosemwa na hawa wanaodai kuwa wana inside information ya kilichokubaliwa kati ya CUF na CCM ... mwingine ameyaita MOU
 
unajua how tight security ilivyokuwa (kupata hiyo inside info yako ?) katika hicho kikao ? i assume you do. hata hao wapambe hawakuwa na nafasi !
 
unajua how tight security ilivyokuwa (kupata hiyo inside info yako ?) katika hicho kikao ? i assume you do. hata hao wapambe hawakuwa na nafasi !

Kada yaliyosemwa kwenye kikao cha CCM yanafahamika. Ulisoma ile story ya raia mwema? ile ni dondoo tu. Yote yaliyosemwa yako nje na CUF wanayajua na ndio maana wanatoka kwenye meza ya majadiliano.... Kikwete hawezi kutunza siri yoyote, he is so weak to do that
 
CUF wakitaka muafaka wa kweli na CCM, ni lazima wamuondoe Maalim Seif kwanza, kwa sababu to me ni very clear kuwa Seif ana agenda tofauti kabisa na ya wanachama wengi wa CUF,

Sasa hivi Seif is caught up in the middle kati ya mafao ya CCM na handlers wake wa Oman, lakini ninashangaa kuwa mpaka sasa CUF hawajalijua hili na kuendelea kumruhusu Seif kuwachezea akili,

Lipumba ni another waste politician, niliposema huko nyuma mkulu Kitila ukaja juu kuwa unamjua sana na kuna waliokushangilia hapa, kwanza kule UN ameshindwa kazi muda aliopewa kukamilisha ripoti ya UN umepita na hana hiyo ripoti, anataka siasa lakini pia anapenda sana pesa, mkulu Kitila ninakuomba utakapomuona tena umuulize CUF walimpa hela ngapi kuwa mwenyekiti wa kutoka Bara maana sio siri tena kuwa alinunuliwa kwa pesa kutoka Oman!

Nyinyi wanachama wa CUF, huu ni wakati muhimu sana kuanza kuamka kuwa mnachezewa na hawa viongozi uchwara ambao hawana your interest at all na Zanzibar, isipokuwa matumbo yao na wanaowatuma, ni kweli CCM pia tuna matatizo yetu kwenye hiii ishu, lakini ni tatizo pia unapokuwa una-deal na viongozi uchwara unaowajua wazi kuwa hawana nia njema na taifa na hasa Zanzibar kwa ujumla, kuandaa maandamano ya Ijumaaa baada ya kutoka msikitini, ili kuwafurahisha wakubwa wa Oman, hayatafanikiwa hata siku moja kufikisha the intended message kwa CCM na serikali, CUF wanahitaji viongozi wapya wenye nia njema na CUF yenyewe na wa-Zanzibari wote.

Ahsante Wakulu!
 
...

Sasa hivi Seif is caught up in the middle kati ya mafao ya CCM na handlers wake wa Oman, lakini ninashangaa kuwa mpaka sasa CUF hawajalijua hili na kuendelea kumruhusu Seif kuwachezea akili,

.....

FM ES,

Sidhani kama unamaanisha hiki unachokisema hapa. Yaani hapa ndipo tumefikia kuwa matatizo ya Pemba si kwa vile wapemba wengi wametengwa kwa muda mrefu na serikali ya mapinduzi au si kwa vile CUF walishinda uchaguzi na ccm wakiongozwa na Nyerere wakafanya usanii (kama wewe mwenyewe ulivyosema hapa) bali ni kwa vile Seif anatumiwa na wa Oman?

Kama CUF wanatumiwa na wa Oman, hao wanaouza migodi na mali za watanzania wanatumiwa na nani?
 
hii topic ni ngumu, na sasa unapoanza kuchanganya madawa kusema sijui hao wanaouza migodi, unakuwa sio tu umetoka nje ya mada, bali pia kufanya hili suala lionekane gumu zaidi !
 
hii topic ni ngumu, na sasa unapoanza kuchanganya madawa kusema sijui hao wanaouza migodi, unakuwa sio tu umetoka nje ya mada, bali pia kufanya hili suala lionekane gumu zaidi !

Kada nashukuru kuwa unaleta argument nzuri na umeacha yale mambo ya ubishi wako na mwafrika wa kike na kuharibu mada bila sababu.

Katika hili, Huwezi kusema kuwa viongozi wa CUF wanaongozwa na Oman bila kuwa tayari kusema viongozi wa ccm wanaongozwa na nani. Huwezi kusema mambo ya CCM baadhi tu na kuyaacha mengine. Ningesema uongo kuwa ccm wameuza migodi na madini ya watanzania basi ungesema kuwa ninachanganya madawa.

CCM ni ile ile bara na visiwani, je unapinga hili?
 
1.
Sidhani kama unamaanisha hiki unachokisema hapa. Yaani hapa ndipo tumefikia kuwa matatizo ya Pemba si kwa vile wapemba wengi wametengwa kwa muda mrefu na serikali ya mapinduzi

Matatizo ya wa-Pemba na wa-Unguja, ni more than kinachoajdiliwa kwenye muafaka, na kama hiii dhana yako ni kweli basi Pemba na Unguja, zingetakiwa kutenganishwa na kuwa nchi mbili tofauti kwa sababu matatizo yao ni mmore culturally, na politically, sasa kuepusha hayo ndio sababu unatafutwa muafaka, Seif ana interest ya Pemba tu, ambayo ndio hasa agenda ya "Oman"

au si kwa vile CUF walishinda uchaguzi na ccm wakiongozwa na Nyerere wakafanya usanii (kama wewe mwenyewe ulivyosema hapa) bali ni kwa vile Seif anatumiwa na wa Oman?

Huwa kwangu ninayona maaajabu makubwa jinsi walioibiwa ushindi wa uchaguzi wa kura, wanapokubali kukaaa chini na kuongea muafaka kwa kweli sielewi na sijawahi kusikia hilo mahali popote duniani zaidi ya Zanzibar tu!

Kama CUF wanatumiwa na wa Oman, hao wanaouza migodi na mali za watanzania wanatumiwa na nani?

1. CUF hawatumiwi na Oman, ni Seif tu ndiye anyetumiwa na both sides yaaani CCM na Oman,

2. Watanzania, wanaouza migodi yetu, wanatumiwa na hao wanaowauzia ambao sio wananchi wala taifa letu, ndio maana tunawaita mafisadi.
 
1.
Katika hili, Huwezi kusema kuwa viongozi wa CUF wanaongozwa na Oman bila kuwa tayari kusema viongozi wa ccm wanaongozwa na nani.

Seif tu ndiye anyetumiwa na Oman, sio viongozi wote wa CUF, viongozi wa CCM wanatumiwa na mawazo na legacy ya Mwalimu, na pia wanawasimamia wenzetu weusi wa huko hasa Unguja.

CCM ni ile ile bara na visiwani, je unapinga hili?

Ingekuwa kweli Butiama kusingekuwa na tatizo.
 
1.

Matatizo ya wa-Pemba na wa-Unguja, ni more than kinachoajdiliwa kwenye muafaka, na kama hiii dhana yako ni kweli basi Pemba na Unguja, zingetakiwa kutenganishwa na kuwa nchi mbili tofauti kwa sababu matatizo yao ni mmore culturally, na politically, sasa kuepusha hayo ndio sababu unatafutwa muafaka, Seif ana interest ya Pemba tu, ambayo ndio hasa agenda ya "Oman"

Hii statement ni kubwa sana kwako wewe kuitoa kwa kiongozi wa kitaifa wa chama cha siasa Tanzania. Kama kweli CCM wanataka amani na muafaka wa kweli zanzibar, sidhani kama statement kama hizi zinaelekea kwenye amani na muafaka.

Huwa kwangu ninayona maaajabu makubwa jinsi walioibiwa ushindi wa uchaguzi wa kura, wanapokubali kukaaa chini na kuongea muafaka kwa kweli sielewi na sijawahi kusikia hilo mahali popote duniani zaidi ya Zanzibar tu!

Wafanye nini kama serikali ya ccm inapeleka jeshi na polisi toka bara na kuuwa watu bila kujali? Unataka waanzishe kajeshi kao kadogo wapambane? CUF wamekuwa wanajaribu kila mwaka kuleta amani zanzibar kuanzia mwaka 1995 lakini inaoneka ccm ndio hawataki kabisa kuwa na amani na sishangai mwiba anaposema hapa kuwa ccm wanapenda kuona damu za wapemba zikimwaga na polisi

1. CUF hawatumiwi na Oman, ni Seif tu ndiye anyetumiwa na both sides yaaani CCM na Oman,

2. Watanzania, wanaouza migodi yetu, wanatumiwa na hao wanaowauzia ambao sio wananchi wala taifa letu, ndio maana tunawaita mafisadi.

Viongozi wa chama ndio chama chenyewe. Huwezi kusema kuwa ni viongozi wa vyama na sio CUF yenyewe, otherwise ingekuwa watu hawapigi kura kutoa vyama na viongozi vyao madarakani kama kuna tofauti kati ya viongozi na vyama vyao.

Ukidai kuwa Seif anatumiwa na Oman ina maana CUF ndio wanatumiwa na Oman. For this case, Kikwete na wenzake ccm wanatumiwa na wazungu kuuza nchi na kusababisha uvunjifu wa amani zanzibar
 
1.

Seif tu ndiye anyetumiwa na Oman, sio viongozi wote wa CUF, viongozi wa CCM wanatumiwa na mawazo na legacy ya Mwalimu, na pia wanawasimamia wenzetu weusi wa huko hasa Unguja.

Ingekuwa kweli Butiama kusingekuwa na tatizo.

Una maana gani kusema kuwa CCM wanawasimamia wenzetu weusi wa huko Unguja? Ina maana hao wengine wasio weusi huko Unguja ni kina nani?

Nilihisi kuwa CCM hawajaacha bado mawazo yao kuwa wapemba sio waafrika weusi. Kikwete ametumia ubaguzi dhidi ya Salmini kuwa si mweusi mwenzetu na naona kuwa ni the same game inaendelea hapa.
 
1.
Wafanye nini kama serikali ya ccm inapeleka jeshi na polisi toka bara na kuuwa watu bila kujali? Unataka waanzishe kajeshi kao kadogo wapambane? CUF wamekuwa wanajaribu kila mwaka kuleta amani zanzibar kuanzia mwaka 1995 lakini inaoneka ccm ndio hawataki kabisa kuwa na amani na sishangai mwiba anaposema hapa kuwa ccm wanapenda kuona damu za wapemba zikimwaga na polisi

I mean Mungu awarehemu wale wote waliomwaga damu zao kule Pemba, lakini baada tu ya damu yao kumwagika, Seif akapewa mafao na serikali ya CCM na kuyakubali, huku Lipumba akienda UN Geneva kufanya kazi, lakini pia kufanya maandamano bila kibali cha serikali ni kuvunja sheria za jamhuri, hili hata US na UK, huwezi kulifanya, ni lazima upate kibali cha serikali.

2.
Viongozi wa chama ndio chama chenyewe. Huwezi kusema kuwa ni viongozi wa vyama na sio CUF yenyewe, otherwise ingekuwa watu hawapigi kura kutoa vyama na viongozi vyao madarakani kama kuna tofauti kati ya viongozi na vyama vyao.

Hapana kuna wakati wananchama wa chama lazima wakae chini kuangalia mwenendo wa kiongozi wao, kama kweli ana nia njema na chama kile, na ni wakati sasa wa CUF kukaa chini na kumuangalia Seif kwa kina, maana hana interest yoyote ya chama na wananchi.

3.
Ukidai kuwa Seif anatumiwa na Oman ina maana CUF ndio wanatumiwa na Oman. For this case, Kikwete na wenzake ccm wanatumiwa na wazungu kuuza nchi na kusababisha uvunjifu wa amani zanzibar

CUF kama chama hakitumiwi na Oman, lakini Seif anatumiwa, Kikwete na CCM wanajaribu kuendeleza mawazo na legacy ya Mwalimu, na kuwasimamia weusi wenzetu huko visiwani, and I am down with that!
 
1.

I mean Mungu awarehemu wale wote waliomwaga damu zao kule Pemba, lakini baada tu ya damu yao kumwagika, Seif akapewa mafao na serikali ya CCM na kuyakubali, huku Lipumba akienda UN Geneva kufanya kazi, lakini pia kufanya maandamano bila kibali cha serikali ni kuvunja sheria za jamhuri, hili hata US na UK, huwezi kulifanya, ni lazima upate kibali cha serikali.

Hili swala la mafao ya Seif ni kulingana na nafasi yake kama waziri kiongozi mstaafu wa serikali ya mapinduzi. Hizi pesa na mafao sio ya ccm bali ni ya serikali. Kama vile Malecela na EL wanavyopata check nzuri toka serikalini basi hata Seif naye ni mstaafu kwa hiyo mafao ni haki yake.

Hilo la Lipumba ni haki yake, au umesahau wapinzani wengi ni walimu wa vyuo vikuu au wafanyabiashara na huwa wanaendelea na kazi zao maana wao si waajiriwa wa serikali?

2.

Hapana kuna wakati wananchama wa chama lazima wakae chini kuangalia mwenendo wa kiongozi wao, kama kweli ana nia njema na chama kile, na ni wakati sasa wa CUF kukaa chini na kumuangalia Seif kwa kina, maana hana interest yoyote ya chama na wananchi.

Hili ni suala la wana CUF na sio la wanaccm kuamua. Kama wanaccm wamekutana Butiama na kushindwa kuwashughulikia mafisadi kina Mkono na Lowasa, je unategemea wanaccm watawaambia CUF cha kufanya?

3.

CUF kama chama hakitumiwi na Oman, lakini Seif anatumiwa, Kikwete na CCM wanajaribu kuendeleza mawazo na legacy ya Mwalimu, na kuwasimamia weusi wenzetu huko visiwani, and I am down with that!

Unakubali kuwa Kikwete na viongozi wa ccm wanatumiwa na wazungu kuuza nchi ya Tanzania na kuua watanzania wenzetu kule Pemba?
 
1.
Hili swala la mafao ya Seif ni kulingana na nafasi yake kama waziri kiongozi mstaafu wa serikali ya mapinduzi. Hizi pesa na mafao sio ya ccm bali ni ya serikali. Kama vile Malecela na EL wanavyopata check nzuri toka serikalini basi hata Seif naye ni mstaafu kwa hiyo mafao ni haki yake.[/B
]

Ni kweli mkuu, lakini kuanza kupewa mafao baada ya wananchi kupoteza maisha yao kwa kufuata amri iliyotolewa na yeye against serikali ile ile inayompa mafao ni usaliti kwa waliokufa, ingawa ni haki yake, tatizo ni timing ya yeye kuanza kuchukua mafao, yaani baada ya wananchi kupoteza maisha yao wakimsikilza Seif.

2.
Hilo la Lipumba ni haki yake, au umesahau wapinzani wengi ni walimu wa vyuo vikuu au wafanyabiashara na huwa wanaendelea na kazi zao maana wao si waajiriwa wa serikali?[/
SIZE]

Kwenye hili tuko page moja.

3.
Hili ni suala la wana CUF na sio la wanaccm kuamua. Kama wanaccm wamekutana Butiama na kushindwa kuwashughulikia mafisadi kina Mkono na Lowasa, je unategemea wanaccm watawaambia CUF cha kufanya?

Ndio maana nimesema kuwa CCM ni safi, ila kuna viongozi wachache wachafu, lakini tutawaondoa tu pole pole tunasogea, maan karibuni tu tutaingia ndani wananchi wenye mawazo ya kimapinduzi na yenye nia njema kwa taifa letu, wote wataondoka tu!

4
. Unakubali kuwa Kikwete na viongozi wa ccm wanatumiwa na wazungu kuuza nchi ya Tanzania na kuua watanzania wenzetu kule Pemba?

Hakuna mzungu mwenye shida ya Zanzibar, ni Oman ndio wenye shida na mali zao zilizotaifishwa wakati wa mapinduzi ya Karume.
 
1.

Ni kweli mkuu, lakini kuanza kupewa mafao baada ya wananchi kupoteza maisha yao kwa kufuata amri iliyotolewa na yeye against serikali ile ile inayompa mafao ni usaliti kwa waliokufa, ingawa ni haki yake, tatizo ni timing ya yeye kuanza kuchukua mafao, yaani baada ya wananchi kupoteza maisha yao wakimsikilza Seif.

Mafao ya Seif yalitakiwa kutolewa wether kuna matatizo au bila matatizo. Mbona mafao ya wengine wastaafu hayajawahi kuzuiwa. Hii haimake sense kwa mtu ambaye umekuwa mtetezi mzuri wa mafao ya viongozi wakubwa wa serikali

2.

Kwenye hili tuko page moja.

3.

Ndio maana nimesema kuwa CCM ni safi, ila kuna viongozi wachache wachafu, lakini tutawaondoa tu pole pole tunasogea, maan karibuni tu tutaingia ndani wananchi wenye mawazo ya kimapinduzi na yenye nia njema kwa taifa letu, wote wataondoka tu!

Unajua hata Mugabe amekuwa anawahidi wazimbabwe kuwa mambo yanafanyika polepole ila kuna siku yatakuwa mazuri. Hiyo subira wakati nchi inauzwa kwa wazungu sijui ni kwa manufaa ya nani.

Wewe endelea kusubiri labda utaibadili ccm wakati mikoa yote ya kanda ya ziwa inamilikiwa na wazungu.

4

Hakuna mzunge mwenye shida ya Zanzibar, ni Oman ndio wenye shida na mali zao zilizotaifishwa wakati wa mapinduzi ya Karume.

CCM ni chama cha masilahi ya wazungu na kiongozi wao ambaye Kikwete alimleta Tanzania karibuni na kukaa naye kwa siku nne. Kama Bushi anapigana vita Iraq na kwingine, haishangazi kuwa anamsapoti Kikwete kwenye kumwaga damu ya wapemba, ni juzi tu Kikwete amepeleka jeshi Comoro. Inaonekana kuna mengi sana ya kufanana kwa hawa wawili.

Hawa waomani hatuwasikii zaidi ya wazungu wanaokuja Tanzania kila mwaka na safari za Karume za Ulaya zisizo na mwisho
 
Kada Mpinzani, Field Marshall ES,

Nisaidieni kumuelimisha mwafrika wakulu nimechemsha ngoma haielewei kabisa!!! unatoa hoja analeta vioja. Sijui madarasani ngoma ilikuwa je?
 
CUF wanadai wataandamana nchi nzima?Labda watuambie ni Mikoa ipi watakao andandamana!maana kuna mikoa mingine cuf wanasikika kwenye vyombo vya habari!au labda watawashirikisha chadema na vyama vingine waandamane kwa niaba yao baadhi ya mikoa
 
1. Sitapenda kujadili historia ya Zanzibar, asili ya mtanziko wa kisiasa huko; lakini mimi naomba nichangia suala la principle tu hapa- kwamba pande mbili zimekaa zimajadiliana na kukubaliana mambo Fulani Fulani; baadaye upande mmoja umeanza kwenda tofauti. It’s a political problem, that needs a political solution.
2. Nimesoma neno kwa neno rasimu ya makubaliano ya CUF na CCM ambayo ilishakubaliwa na kamati zote mbili. Suala la serikali ya pamoja linapaswa kutekelezwa kabla ya mwaka 2010.
3. Nimesoma ripoti ya Kamati ya CCM iliyopeleka Butiama kwa ajili ya Kamati Kuu na baadaye halmashauri Kuu; ukweli ni kuwa hoja ya kura ya maoni haikuzuka kikaoni- iliandaliwa kabla kwa pendekezo la Karume na kukubaliwa na wanakamati. Pamoja na uzuri wa dhana ya kura za maoni, lakini nia(motive) yake hapa si nzuri! Kwa serikali ambayo haifanyagi referendum katika masuala muhimu kihistoria kama Muungano, Katiba, Mfumo wa Vyama vingi, kumuundoa Rais wa Zanzibar kama makamu wa Rais(ambalo lilikuwa ni suala katika makubaliano mama ya muungano); inatia shaka serikali kama hiyo itakapo suala la kura za maoni Zanzibar. Ni Kikwete huyu huyu ambaye alipokwenda Kenya hakutaka wakina Raila na Kibaki wafanye kura za maoni, akata wasaini makubaliano na kuyatekeleza. Wakati wa kuibwa kwa kura hakuitishwa kura za maoni, kosa moja haliwezi kuhalalisha kosa, lakini kosa moja linaweza kutoa ishara ya kosa lingine! Kwa ujumla ukiisoma ripoti hii ya Kamati ya CCM; ukisoma na Barua ya Mwisho ya Makamba; utagundua kuwa Makamu Mwenyekiti Msekwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete- hawakusema kweli wakati wakieleza mchakato wa Maazimio ya NEC ya CCM na Matokeo yake!
4. Nilikuwepo Diamond Jubilee jana na nimemsikiliza Lipumba toka mwanzo mpaka mwisho. Nilichokielewa ni kwamba CCM imekuwa ikiwatapeli CUF toka baada ya uchaguzi, ikiwafanyia unafiki wa hali ya juu- CUF nayo kwa upande wake ilikuwabali ku-give in too much; ikakubali ghilba za aina zote ikiwa na matumaini makubwa kwamba Kikwete yuko genuine! Na kwa kiasi kikubwa mambo yote haya yalifanyika kwa siri ya pande mbili; kwa mategemeo makubwa ya CUF kwamba pengine serikali ya mseto ingetokea. Kumbe CCM wakati wote ilikuwa ikiweka kadi chache mezani na nyingine nyingi zaidi kuzificha chini ya meza.Ukiangalia mtiririko wa matukio katika hii miaka mitatu kuhusu Zanzibar utagundua ama Rais Kikwete anafanya unafiki wa hali ya juu wa kisiasa, au ni kiongozi dhaifu katika CCM kama mwenyekiti anayezidiwa nguvu na makundi mengine ndani ya chama chake. Kwa vyovyote vile, hali hii ikiachwa bila panga kuitwa panga na si kisu kikubwa ni ishara mbaya kwa utangamano wetu kama taifa haswa kwa kuwa kwa sasa CCM ndicho chama tawala!
5. Tunaungana mkono na CUF katika hili, kwani kitisho cha demokrasia mahali Fulani ni kitisho cha demokrasia mahali pote. Maandamano ya jumamosi, hayapaswi kuwa maandamano ya CUF, yanapaswa kuwa maandamano ya umma! Ama hakika, uwongo una mwisho- lakini ukweli unapaswa husimama milele, na ukweli hauna itikadi. CUF wanaweza kuwa walijikwaa mahali Fulani katika mchakato huu; lakini sasa ni wakati wa kutazama mbali zaidi, kutazama picha kubwa zaidi- CCM ikiwachwa ikapita katika hili, itandelea kuacha na ufisadi mwingine ukatawala kwenye RICHMOND, BOT nk na hatimaye kuweka misingi ya ufisadi wa kudumu zaidi katika uchaguzi mkuu 2010. Hatupaswi kuacha utadamuni wa ufisadi, usanii wa kisiasa, uchezeaji wa haki, na wananchi kukaaa pembeni kama watazamaji na wanyooshaji vidole kuendelea katika taifa letu. Ni wakati mwingine wa kuandelea kuchukua hatua!
JJ

PS:
• Mwenye Hotuba ya Jana ya Lipumba atuwekee hapa tafadhali
• Mwenye rasimu ya makubaliano ya CUF na CCM iliyokubaliwa na kamati za pande mbili aiweke hapa pia tafadhali
 
1.
Pamoja na uzuri wa dhana ya kura za maoni, lakini nia(motive) yake hapa si nzuri!

Nia nzuri inaweza kutoka kwa yule aliyekunyanga'anya ushindi kwenye uchaguzi? Hivi kwa nini hata wewe huwezi kuona kuwa hapa kuna usanii kutoka pande zote mbili kuwa hakuna mwenye nia njema na sio upande mmoja tu?

2.
Kwa serikali ambayo haifanyagi referendum katika masuala muhimu kihistoria kama Muungano, Katiba, Mfumo wa Vyama vingi, kumuundoa Rais wa Zanzibar kama makamu wa Rais(ambalo lilikuwa ni suala katika makubaliano mama ya muungano); inatia shaka serikali kama hiyo itakapo suala la kura za maoni Zanzibar.

Mbele ya macho ya wapenda demokrasia duniani, kura ya maoni ni the best alternative kwa matatizo yoyote ya kisiasa, CUF walihitaji kuipa a chance hiii kitu, lakini pia walipaswa kuwaomba watu wa nje kuja kuwsaidia ksimamia kura hizo, lakini kukataa kupigwa kura haukuwa uamuzi wa busra hasa baada ya kukubali kukaa chini kwa miezi 14 na wale waliokunyang'anya ushindi.
 
CUF wanaweza kuwa walijikwaa mahali Fulani katika mchakato huu; lakini sasa ni wakati wa kutazama mbali zaidi,

Anayejikwaa kila wakati ni Seif, sio CUF akitoka tu huyu mkuu basi muafaka utapatikana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom