CUF kuandamana nchi nzima

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,169
Leo Mwenkyekiti wa CUG, Prof Ibrahim Lipumba ameunguruma katika ukumbi wa Diamond Jubilee na kutoa msimamo wa chama hicho kuhusiana na masuala ya muafaka.

Kwanza CUF imempa masharti JK ili kunusuru mwafaka huo. Wamemtaka aidha, CCM isaini makubaliano kama yalivyokuwa kabla haijatumbukiza kipengere cha kura ya maoni, au awakutanishe Maalim Seif na karume wajadiliane la kufanya kama ambayo aliwakutanisha Odinga na Kibaki kule Kenya.

Asuipofanya hivyo, kitakachotokea CUF imesema isilaumiwe.

Kwa kuonyesha nguvu yake, chama hicho kimesema kimeandaa maandamano yatakayofanyika mikoa yote nchini na wanaanzia Z'Bar Jumamosi ijayo wakiwashikirisha viongozi wakuu wa vyama vilivyo kwenye ushirikiano. Wakitoka Zenji, wanahamia mkoa mwingine.
Tujiandae kwa mabomu ya machozi?
 
sawa wakifanya kwa amani watapokewa kwa amani, ndio wakitaka kutumia fursa hio kujipima nguvu sawa tutaona nazi kushindana na jiwe
 
Bado tuna upinzani wa Kisanii zaidi, Barua ya Makamba imeomba kamati za Muafaka zikae chini ziendelee na kazi!
 
Leo Mwenkyekiti wa CUG, Prof Ibrahim Lipumba ameunguruma katika ukumbi wa Diamond Jubilee na kutoa msimamo wa chama hicho kuhusiana na masuala ya muafaka.
Kwanza CUF imempa masharti JK ili kunusuru mwafaka huo. Wamemtaka aidha, CCM isaini makubaliano kama yalivyokuwa kabla haijatumbukiza kipengere cha kura ya maoni, au awakutanishe Maalim Seif na karume wajadiliane la kufanya kama ambayo aliwakutanisha Odinga na Kibaki kule Kenya.Asuipofanya hivyo, kitakachotokea CUF imesema isilaumiwe.
Kwa kuonyesha nguvu yake, chama hicho kimesema kimeandaa maandamano yatakayofanyika mikoa yote nchini na wanaanzia Z'Bar Jumamosi ijayo wakiwashikirisha viongozi wakuu wa vyama vilivyo kwenye ushirikiano. Wakitoka Zenji, wanahamia mkoa mwingine.
Tujiandae kwa mabomu ya machozi?
Ama kweli namkumbuka Marehemu Dr. Omar (aliyekuwa Makamo wa Rais) alikuwa akipanda kiririni husema Balahau umekwisha-- nakwambia huna sera!!!!!! CUF(SEIF NA LIPUMBA) wanataka kulifananisha hili suala na la kina Odinga (Kihadhi na kimtazamo) ili kujilindia status yao kwa wanachama wao, na zaidi kwa watu wa nje.Ile startegy yao ya kupanda viririni na kujitangazia peke yao kuundwa kwa mseto imeshavunjika. Sasa hii ndio ile mnayoiita Plan B waliyokuja nayo. Wamekwisha Bwana, Watarudiu mezani na watakubali Serikali Shirikishi. Wafuasi wao sio watu wasio na ufahamu kama wanavyodhaniwa. Ni watu wenye busara na safari hii lazima watawagomea, kwani wameshashoshwa na usumbufu wa kutengenezwa na viongozi wao.
 
Hivi ni nani aliyekataa serikali ya shirikishi? ni CUF au ni CCM?
 
Wote wamekubali Serikali ya shirikisho!!!

Wanachotofautiana namna ya kutekeleza.

CCM: Wanapendekeza serikali ya shirikisho sawa, lakini hoja lazima irudishwe kwa wananchi kwa kuwa ni suala kubwa/zito na la kikatiba.
CUF: Wanasema kuna mengi yalishafanyika bila ku-consult wananchi na hili pia hakuna haja ya kuwauliza wananchi:

My take!
CUF wanataka implementation ifanyike haraka ikiwezekana kesho!!!
 
Kama wamekubaliana basi kura ya maoni ni ya nini? Je ccm wako tayari pia kupitisha kura huru ya maoni kuhusu muungano wa zanzibar na Tanganyika? au hili sio swala kubwa la kikatiba?
 
Kama wamekubaliana basi kura ya maoni ni ya nini?
Try a little bit to think aloud, ni mfumo wa serikali ya zanzibar unabadilishwa big time, kwa hivyo katiba itabadilika big time;

Mpaka leo hakuna katiba [ya Zanzibar/Tanzania] iliyowahi kubadilishwa kama itakavyobadilishwa ya Zanzibar baada ya Muafaka huu.

Narudia tena, siku zote wananchi waliwahi kushirikishwa kwenye mabadiliko ya Katiba zote kupitia Bunge, hata Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mabunge yalihusishwa.

Pia ikumbukwe kwamba dhana ya utawala bora haikuwa kubwa enzi hizo kama sasa... Serikali yoyote iliyoko madarakani sasa inapenda kushirikisha wananchi!

Je ccm wako tayari pia kupitisha kura huru ya maoni kuhusu muungano wa zanzibar na Tanganyika? au hili sio swala kubwa la kikatiba?
Please do not mix agenda... this is not in the scope...at the moment!!!
 
My take!
CUF wanataka implementation ifanyike haraka ikiwezekana kesho!!!

Kweli wanataka hivyo lakini tatizo ni kuwa CUF hawakuliweka hilo vema katika makubaliano yaliyofikiwa.
Ukisoma makubaliano yao, hakuna sehemu ambayo inaonyesha makubaliano hayo yaanze kutekelezwa lini. Kwa hiyo hata ile kauliya CUF kuwa wanataka kuundwa kwa serikali shirikishi mara moja, haina msingi kwa sababu makubaliano hayajaweka deadline, na ninadhani kuwa CCM walishaiona loop hole hiyo tangu mwanzo wakaacha CUF wajiingize mkenge wenyewe, na sasa wamenaswa
 
Loop hole kama hizi zinamanufaa gani kwa watanzania wa kawaida kama ccm wakileta siasa kwenye jambo zito kama hili?
 
Hivi ni nani aliyekataa serikali ya shirikishi? ni CUF au ni CCM?

Sijui.Labda nikuulize wewe Mheshimiwa. CCM hawajakataa hiyo Serikali. Wametoa mapendekezo ya kuboresha Yale yenye nafasi mbili za Unaibu wa Rais (Makamo wa Rais 1 na Makamo wa Rais 2) pamoja na majukumu yao katika ku-share hayo madaraka. CCM wametaka mapendekezo hayo yapitiwe tena na Kamati ya Muafaka. Na pindi CUF ikiyakubali, basi Muundo huo wa Serikali utumiwe katika utawala wa nchi baada ya uchaguzi wa (2010). Kwa vile jambo hili ni kubwa na litaleta mabadiliko makubwa ya mfumo wa Utawala na shughuli za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Baraza la Wawakilishi, na marekebiosho ya Katiba ya Zanaibar basi ni vyema (CCM imesdhauri)likapatiwa baraka za watu wote wa Zanzibar kwa kura za maoni. Hiyo ndiyo verdict. CUF hawataki kusikiliza chochote, na wataandamana. Sasa nani amekataa?
 
Try a little bit to think aloud, ni mfumo wa serikali ya zanzibar unabadilishwa big time, kwa hivyo katiba itabadilika big time;

Mpaka leo hakuna katiba [ya Zanzibar/Tanzania] iliyowahi kubadilishwa kama itakavyobadilishwa ya Zanzibar baada ya Muafaka huu.

Wakati hii process ya majadiliano ya muafaka ikiendelea kwa miezi 14, je ccm walilijua hili au wamekumbuka leo hii baada ya kuona kuwa kuna miaka mingine miwili wanaweza kuzungushana na CUF kwenye hili hadi ifike 2010?

Narudia tena, siku zote wananchi waliwahi kushirikishwa kwenye mabadiliko ya Katiba zote kupitia Bunge, hata Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mabunge yalihusishwa.
Pia ikumbukwe kwamba dhana ya utawala bora haikuwa kubwa enzi hizo kama sasa... Serikali yoyote iliyoko madarakani sasa inapenda kushirikisha wananchi!

Please do not mix agenda... this is not in the scope...at the moment!!!

Kama bunge linawakilisha wananchi na kama ulivyosema kuwa yote yaliyopita bunge lilishirikishwa, hili la serikali ya pamoja lina tofauti gani na mengine yaliyopita ikiwemo muungano?
 
Sijui.Labda nikuulize wewe Mheshimiwa. CCM hawajakataa hiyo Serikali. Wametoa mapendekezo ya kuboresha Yale yenye nafasi mbili za Unaibu wa Rais (Makamo wa Rais 1 na Makamo wa Rais 2) pamoja na majukumu yao katika ku-share hayo madaraka. CCM wametaka mapendekezo hayo yapitiwe tena na Kamati ya Muafaka. Na pindi CUF ikiyakubali, basi Muundo huo wa Serikali utumiwe katika utawala wa nchi baada ya uchaguzi wa (2010). Kwa vile jambo hili ni kubwa na litaleta mabadiliko makubwa ya mfumo wa Utawala na shughuli za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Baraza la Wawakilishi, na marekebiosho ya Katiba ya Zanaibar basi ni vyema (CCM imesdhauri)likapatiwa baraka za watu wote wa Zanzibar kwa kura za maoni. Hiyo ndiyo verdict. CUF hawataki kusikiliza chochote, na wataandamana. Sasa nani amekataa?

naona unajichanganya hapa...

Kuna sehemu unasema kuwa pande zote mbili zimekubaliana na kuna sehemu pia unasema kuwa ccm wamebadilika na kuamua mambo yaende kwa wananchi. Katika hili aliyekataa makubaliano ni ccm. Sheria za mikataba zinasema kuwa upande mmoja ukibadili vipengele vya mkataba basi hiyo ni sawa na kukataa mkataba.

Kuhusu hii ya kusikiliza wananchi, je ccm iko tayari kuwaruhusu wananchi wa zanzibar watoe maoni yao kuhusu muungano?
 
Loop hole kama hizi zinamanufaa gani kwa watanzania wa kawaida kama ccm wakileta siasa kwenye jambo zito kama hili?

Na hiyo haraka haraka ya kutaka mambo hayo yawe, tena kiholela bila ya umakini itamsaidia nani kama si kuzusha mgogoro mwengine katika uongozi wa Serikali na Nchi ya Zanzibar. Mtapata sifa leo mmesuluhisha mgogoro,lakini kabla ya uchaguzi wa 2010 watu watasusiana tena. Huo,si utakuwa mchezo wa kitoto?
 
Loop hole kama hizi zinamanufaa gani kwa watanzania wa kawaida kama ccm wakileta siasa kwenye jambo zito kama hili?

CUF walipaswa kulifahamu hilo na kuhakikisha kuwa katika makubaliano hakuna loop hole kama hizo ili kufanikisha azma yao. Kama na wao walishindwa kuliona hilo, itabidi wananchi waanze kujiuliza wana maana ganai? Labda nao wanacheza mchezo wa siasa
 
Kwa hiyo kwako wewe hapa wa kulaumiwa ni CUF na sio Kikwete ambaye aliahidi kuwa atahakikisha kunakuwa na muafaka zanzibar bila kujali nani mwenye makosa?
 
Mimi nadhani CUF wapo katika wakati mzuri sana wa kufanikisha majadiliano ya muafaka sasa kuliko wakati mwingine wowote. Kwa kipindi cha miezi 14 majadiliano yalikuwa ni kati ya Vyama tu yaani CCM na CUF na ambayo yalikuwa ni siri kwa walengwa.

Sasa maamuzi yanaombwa yaletwe kwa walengwa ili wayatolee maamuzi ya mwisho, nyie CUF ambao mliona iwe siri hata kwa walengwa wakati huo, leo hii mnakataa wananchi wasishiriki kufanya hivyo, hivi hii ndiyo HAKI SAWA KWA WOTE?

Ninawasihi rudini kwenye mazungumzo ya muafaka yaendelee na hili wazo la kupanua wigo wa kufikia muafaka kwa kuwashirikisha wananchi wote hamna haja ya kulipinga kwani majadiliano hayo ni kwa faida ya wananchi wanaoishi Unguja na Pemba na ndiyo hao wenye kauli ya mwisho ya nini wanakihitaji katika maisha yao ya kila siku na wala siyo Waunguja na Wapemba waishio nje ya visiwa hivyo.

Kusahauliwa kipengele cha kura ya maoni katika majadiliano ya muafaka hayawezi kuathiri mchakato wa majadiliano kwani kipengele hicho kinatoa fursa ya kupanua wigo wa kidemokrasia na kuepusha migongano ya kisheria hapo baadae. Kwa hali ilivyo sasa, endapo Muafaka kati ya CCM na CUF utaingia katika utekelezaji bado mgogoro katika visiwa hivyo hautakuwa umeepukika kwani vyama vilivyo nje ya muafaka vitakuwa na haki ya kufungua kesi ya kikatiba kuupinga muafaka huo, na hili nadhani ndiyo lililokuwa linasubiriwa na vyama vilivyo nje ya muafaka. Kama nilivyosema hapo juu kuwa sasa hivi CUF wana nafasi nzuri ya kuufikisha muafaka pale panapokusudiwa kuliko wakati mwingine wowote.

Hizi kauli zinazotolewa na viongozi wa juu wa CUF zinatia walakini mchakato mzima wa kufikia muafaka. Na pengine kauli hizo zinatufungua macho zaidi ya kutaka kujua kulikoni? mbona hawa wanaosema wanatutetea hawataki tuamue wenyewe? je, ni kwanini wanataka washirikishwe haraka iwezekanavyo katika serikali? Je, huu mwafaka walengwa ni kina nani, ni viongozi ndiyo watakao nufaika au wanachi wa kawaida?

Maalim Seif/CUF wanajibu katika hili.
 
Kamanda wewe una maswali mawili ya kujibu hapa wakati tukiwasubiria hao CUF kujibu maswali yako.

1. Je hiyo kura ya maoni ya muafaka itafanyika mwaka gani?
2. Kama itafanyika mwaka 2009, kuna haya ya kupiga kura kuunda serikali ya mseto mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mwingine ambao unaweza kuwa na matokeo tofauti?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom