CUF kuandamana kushinikiza mafisadi EPA kufikishwa kortini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF kuandamana kushinikiza mafisadi EPA kufikishwa kortini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Sep 7, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,209
  Trophy Points: 280
  Date::9/6/2008
  CUF kuandamana kushinikiza mafisadi EPA kufikishwa kortini
  Na Kizitto Noya
  Mwananchi

  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimesema kitafanya maandamano nchi nzima kuishinikiza serikali iwafikishe mahakamani watuhumiwa wa ufisadi wa Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu ya Tanzania (EPA).

  Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba alitangaza maandamano hayo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Temeke Mwisho jijini Dar es Salaam.

  Profesa Lipumba alisema Watanzania wana haki kuihoji serikali sababu za kutowafikisha watuhumiwa hao mahakamani na wataonyesha haki hiyo kwa maandamano yatakayofanyika mwazoni mwa Oktoba mwaka huu.

  "Wito wa CUF kwa serikali ni kutaka iwafikishe mafisadi mahakamani na tumepanga kufanya maandamano makubwa nchi nzima kushinikiza suala hilo katika juma la kwanza la mwezi Oktoba,'"alisea Profesa Lipumba.

  Alisema maandamano hayo ambayo yatawashirikisha watu kada mbalimbali yana lengo la kushinikiza watuhumiwa wa ufisadi wa EPA wafikishwe mahakamani, warejeshe fedha walizoiba na kudai tume huru ya uchaguzi na katiba mpya.

  "Pia tunahitaji tume huru ya uchaguzi ili wananchi wapate fursa ya kumchagua kiongozi wanayompenda na tutadai katiba mpya ili tuishi katika jamii inayoheshimu misingi ya demokrasia," alisema.

  Profesa Lipumba alisema anaamini serikali ya CCM haiwezi kuwa makini katika kuwashughulikia mafisadi kwani imekosa uongozi bora kwa kuwakumbatia wanamtandao ambao ndio mafisadi wenyewe.

  Alisema njia pekee ya kuishinikiza serikali iwashughulikie mafisadi ni maandamano yatakayowashirikisha wananchi wote ili CCM ijue kwamba jamii imechoka na utendaji wake wa kazi.

  Profesa Lipumba alitaja ufisadi wa EPA, rada, Richmond na ununuzi wa ndege ya rais kuwa maeneo machache ambayo serikali imeonyesha udhaifu uwajibikaji.

  Alisema hakuna sababu zinazoelezeka za serikali kuwaongezea muda watuhumiwa wa ufisadi wa EPA kurudisha fedha, kushindwa kumshughulikia mtuhumiwa wa wizi wa ununuzi wa rada na ukosefu wa umakini katika kushughulikia suala la Richmond zaidi ya kuwalinda mafisadi wanaoonekana kuwa na ushawishi mkubwa serikalini.

  Profesa Lipumba alibainisha kuwa fedha za EPA ni za umma tofauti na kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba sio za umma na Watanzania wana haki ya kuhoji ili kujiridhisha juu ya namna zilivyochotwa na zinavyorejeshwa.

  Awali akimkaribisha Profesa Lipumba, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Mbarala Maharagande alisema kama serikali inaona vyema kuwaachia huru watuhumiwa wa EPA baada ya kurejesha fedha, basi iruhusu wafungwa na mahabusu watoke rumande na gerezani wakarejeshe mali walizoiba ili wawe huru.

  Alisema kitendo cha kutaka watuhumiwa EPA warejeshe mali kinakiuka misingi ya demokrasia na utawala wa sheria na kinaligawa taifa katika makundi ya walalahoi na matajiri.


  CUF imetangaza maandamano hayo wiki mbili baada ya kundi la wanaharakati kutoa tangazo la kutishia kufanya maandamano nchi nzima endapo Rais Jakaya Kikwete hatawafikisha mahakamani watuhumiwa watakaoshindwa kurudisha fedha ifikapo Novemba mosi kama alivyoahidi.

  Awali kundi hilo lilipanga kufanya maandamano hayo Agosti 23 mwaka huu kwa lengo la kuishinikiza serikali itangaze majina ya watuhumiwa wa ufisadi wa EPA na hatua iliyochukuliwa dhidi yao lakini ililazimika kuyasitisha baada ya polisi kutoyatambua na kutaka wafuate taratibu za maandamano.
   
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0


  Sawa sawa, this makes a lot of sense bravo CUF on this! I mean finally someone is getting serious!
   
 3. M

  Mtu Kwao JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2008
  Joined: Jan 15, 2008
  Messages: 258
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Jamani mliopo nyumbani haya yasiwe maandamano ya cuf tu,yawe maandamano ya vyama vyote mana sasa sirikali inacheza na wananchi wake jamani.kwa kweli nawapongeza sana hawa CUF kwa mpango wao huu.sirikali inatakiwa kujua watu wamechoka na maigizo yao.
   
 4. M

  MiratKad JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 294
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Better late than never. Hivi ndivyo inavyotakiwa. Vyama vya upinzani vimechelewa sana kutoa shinikizo...
   
 5. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  More power to Lipumba & Co.! Hii inaleta matumaini sana kuhusu mwamko wa kisiasa na utetezi wa haki za binadamu nchini.
   
 6. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Huu ni ule upande mwingine ambao wanasiasa fisadi wamesahau kuwa ndio msingi wa matakwa ya wananchi. Ukichezea mzaha haki ya wananchi hugeuka kuwa kama nyani wagombaniao ndizi shambani. Watapoanza sasa kudai haki katika mali na rasilimali zao ndipo mtu fisadi atashtuka alllah kumbe hawa jamaa wako? Mtu akipewa uwezo na wananchi wa kuamua mambo anapaswa kufanya hivyo na wala wananchi hawatajisikia vibaya ikiwa ataamua vibay kwani wameshampa nafasi hiyo. Ila kutoamua unapopaswa kuamua ni kosa la kikatiba na haki za binadamu. Anyway wananchi wanajua fika kuwa mtu hujifunza kutokana na makosa.
   
 7. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Serikali:Mafisadi wa EPA acheni kukenua

  2008-09-08 09:41:01
  Na Muhibu Said

  Serikali imesema hatua ya mafisadi waliochota mabilioni ya shilingi kwenye Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kurejesha fedha hizo, huenda isiwanusuru na mkono wa sheria kwa vile hatima yao bado inaendelea kushughulikiwa.

  Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba , alipotakiwa na Nipashe kueleza kuhusu hatua ya watu hao kurejesha fedha walizoiba kwenye EPA kuachwa bila kushitakiwa mahakamani kama ni utawala bora.

  Waziri Simba alisema pamoja na kurejesha fedha hizo, hadi sasa hakuna anayefahamu hatima ya watu hao kuhusu tuhuma za kuchota fedha katika akaunti hiyo kwa vile suala lao linaendelea kushughulikiwa na Timu ya Rais, inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Johnson Mwanyika.

  Wengine wanaounda timu hiyo, ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Dk. Edward Hoseah.

  ``Aliyesema hawatashitakiwa ni nani? Je, hukuisikia hotuba ya Rais (Jakaya Kikwete ya hivi karibuni bungeni)?,`` alihoji Waziri Simba alipokuwa akijibu moja ya maswali aliyoulizwa na Nipashe.

  Alipojibiwa kuwa hotuba ya Rais Kikwete iliagiza watu hao washitakiwe mahakamani Novemba Mosi iwapo watashindwa kurejesha fedha walizochota EPA ifikapo Oktoba 31, mwaka huu na si kwa tuhuma za kuiba fedha hizo, Waziri Simba alisema hata yeye hajui hatima ya watu hao kuhusu tuhuma za wizi zinazowakabili kwa vile suala lao bado linaendelea kushughulikiwa na timu hiyo.

  ``Timu ndiyo ita-establish kesi. Kama ni kwenda mahakamani watakwenda, sheria itachukua mkondo wake, kusikiliza pande zote ndio utawala bora. Mimi sijajua kama hapo baadaye itakuwaje,`` alisema Waziri Simba na kuwataka Watanzania waendelee kusubiri ili timu ikamilishe kazi yake.

  ``Naomba tusivuke daraja kabla hatujafika, tuiachie timu ifanye kazi yake, maana bado inaendelea, si unajua iliomba muda?,`` alihoji Waziri Simba.

  Kauli hiyo ya Waziri Simba ilitolewa siku chache baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Eliaza Feleshi, kukaririwa na gazeti hili akisema kwamba hatima ya mafisadi wa wizi wa fedha za EPA iwapo watastahili kushtakiwa au la, iko mikononi mwa Timu ya Rais ya Kuchunguza wizi huo.

  Feleshi alitoa kauli hiyo alipotakiwa kueleza sheria inasemaje iwapo mtu akiiba fedha na kisha akazirejesha.
  Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Jinai namba 258, kuiba ni kosa.

  Hata hivyo, alisema timu hiyo ndiyo yenye wajibu wa kutoa maelekezo iwapo watuhumiwa hao wakabidhiwe kwa Polisi, Takukuru au katika Ofisi ya DPP kwa ajili ya mchakato wa kufikishwa mahakamani.

  Kauli ya Feleshi ilifuatia ile ya Gavana wa BoT, Profesa Beno Ndullu, aliyekaririwa na Nipashe akisema kwamba, watumishi wa benki hiyo waliohusika na EPA, watashitakiwa mahakamani na timu hiyo iwapo itathibitika wana kesi ya jinai ya kujibu.

  Hata hivyo, Feleshi alisema hawezi kuzungumzia suala la watuhumiwa wa wizi wa fedha za EPA kwa madai kwamba, suala hilo halijafika rasmi ofisini kwake na pia, hawafahamu watuhumiwa hao na pia, hafahamu kiasi cha fedha walichoiba.

  ``Hilo lina wasemaji wake, kwani sifahamu ni makubaliano yapi waliyofikia, hotuba ya Rais sina, ripoti ya timu sina, ni kina nani hao na waliiba shilingi ngapi,`` alisema Felesh.

  Timu hiyo ilikabidhi ripoti yake kwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye pia aliitumia kueleza Bunge kwa kirefu hatua alizochukua kutaka makampuni yote 22 yaliyoiba zaidi ya Sh.133 bilioni kwenye EPA, yawe yamekwisha kuzirejesha ifikapo Oktoba 31, vinginevyo, Novemba Mosi, mwaka huu, watafikishwa mahakamani.

  Naye Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk Willibrod Slaa aliiambia Nipashe jana kwamba haoni ni vipi serikali itakwepa kuwapeleka mafisadi wa EPA kortini kwa kuwa hata ukaguzi wa Ernst & Young walishaweka bayana kwamba makampuni 13 kati ya 22 yalipaswa kufikishwa mahakamani na mengine tisa ndio yachunguzwe.

  ``Sioni sababu ya kuacha kuwafikisha mahakamani mafisadi wa EPA, hapa tunapoteza muda tu kufanya uchunguzi mwigine na kupoteza fedha za walipa kodi, ukaguzi tokea awali ulishatoa mapendekezo baada ya kugundua wizi huu,`` alisema.

  * SOURCE: Nipashe
   
Loading...