Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,199
- 1,969
Miaka ya nyuma Chama cha Wananchi, CUF kupitia viongozi na wanachama wake mbalimbali kilidai kwamba Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ni UVAMIZI kwa kuwa yalifanywa na watu wasiokuwa wazanzibari. Kulikuwa na mfululizo wa makala kwenye magazeti yaliyoandikwa: "Historia ya Zanzibar iliyopotoshwa" ili kutilia mkazo hoja hizo. Hivi majuzi tumeona kwamba Rais Karume na Maalim Seif wamekutana na kukubaliana kimsingi kutoa tofauti zao na kujenga maelewano zaidi badala ya chuki na migawanyiko, jambo ambalo limeiletea sifa kubwa sana Zanzibar kimataifa mpaka baadhi ya Wazanzibari wanadai kuwa Rais Karume aongezewe muda ili aongoze kwa kipindi kingine na uchaguzi wa Zanzibar, 2010 usiwepo!
Swali langu ni kwamba, je, bado CUF inayaona mapinduzi haya ni UVAMIZI au wana msimamo ule ule dhidi ya hayo mapinduzi? Na kama mapinduzi hayo ni UVAMIZI (kwa lugha nyingine HAYAKUWA MAPINDUZI) kuna haja ya kuendelea kuyaenzi?
Naomba kutoa hoja!