CUF, Kauli Yenu Juu ya Asili ya Mapinduzi ya Zanzibar Bado ni Ile Ile? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF, Kauli Yenu Juu ya Asili ya Mapinduzi ya Zanzibar Bado ni Ile Ile?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Jan 12, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Miaka ya nyuma Chama cha Wananchi, CUF kupitia viongozi na wanachama wake mbalimbali kilidai kwamba Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ni UVAMIZI kwa kuwa yalifanywa na watu wasiokuwa wazanzibari. Kulikuwa na mfululizo wa makala kwenye magazeti yaliyoandikwa: "Historia ya Zanzibar iliyopotoshwa" ili kutilia mkazo hoja hizo. Hivi majuzi tumeona kwamba Rais Karume na Maalim Seif wamekutana na kukubaliana kimsingi kutoa tofauti zao na kujenga maelewano zaidi badala ya chuki na migawanyiko, jambo ambalo limeiletea sifa kubwa sana Zanzibar kimataifa mpaka baadhi ya Wazanzibari wanadai kuwa Rais Karume aongezewe muda ili aongoze kwa kipindi kingine na uchaguzi wa Zanzibar, 2010 usiwepo!
  Swali langu ni kwamba, je, bado CUF inayaona mapinduzi haya ni UVAMIZI au wana msimamo ule ule dhidi ya hayo mapinduzi? Na kama mapinduzi hayo ni UVAMIZI (kwa lugha nyingine HAYAKUWA MAPINDUZI) kuna haja ya kuendelea kuyaenzi?
  Naomba kutoa hoja!
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Vipi wanaJF, mko kwenye sherehe za mapinduzi mpaka hamjaweza kupata nafasi ya kuchangia mada hii?
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mmmmh, kathread haka bado hakajapata mchangiaji!
   
 4. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mapinduzi yapi unayokusudia, Zanzibar kumetokea Mapinduzi kama mara tatu hivi.Sasa ungeliweka sawa ni yapi unayokusudia.

  General case mapinduzi yote ni haramu na hayafai kuenziwa.Hiyo ndio general case, sasa labda tuanze na kupeana sababu za msingi za kuyaenzi kama zitakuwepo.
   
 5. O

  Omumura JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  MAPINDUZIIIIIIIII, DAIMAAAAAAAAAAAA! Warogwe waseme ni haramu ili ngwe ya uhasama ianze upya!
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mapinduzi ya Januari 12, 1964! Haya leta hoja sasa!
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  A hungry man is an angry man, is that true? Wakubwa wa upinzania wameahidiwa vijinafasi basi EVERYTHING IS OK NOW!
   
 8. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hayo yatafuata general case kuwa kila mapinduzi ni haramu.Hayo mapinduzi ya 1964, hayajaleta mabadiliko yoyote kwa Zanzibar.Kilichofanyika, ni kubadilisha mkoloni tuu.

  Kaondoka mkoloni wa kiengereza, kaondoka mkoloni wa kiarabu na sasa amekuja mkoloni Tanganyika.Kwa Zanzibar bado inahitaji Mapinduzi mengine ya kumg'oa mkoloni mweusi na kupata uhuru ulio wa kweli na Zanzibar ianze kujiendesha weneyewe...

  Kwangu mimi hayo mnayo yaita mapinduzi ni uvamizi tuu wa Tanganyika ndani ya visiwa vya Zanzibar!!!
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Jan 13, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo mnapoyaenzi hayo mapinduzi ambayo hamna imani nayo kwa sasa ni kutafuta political correctness au vipi? Na mkifanya mapinduzi mengine na mkashindwa kuendelea mtadai tatizo ni Pemba vs Unguja na mnafanya MAPINDUZI tena, maendeleo yakishindwa kupatikana mtadai tatizo ni Wazanzibari vs Wazanzibara, etc, etc! Ndio dhambi ya ubaguzi inavyotafuna! Poleni sana!
   
 10. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nafikiri mambo ya wazanzibar tuwaachie wazanzibar wenyewe na nchi yao, watamalizana wenyewe...wabara tuangalie uhuru wa Tanganyika na matokeo yake.

  Sioni merit yeyote ku-discuss issue ya mapinduzi ya zanzibar
   
 11. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nani anayaenzi Mapinduzi?Unasherehekea mapinduzi wakati kesho yake maji hayatoki, wala umeme hakuna, huna ajira...

  Hapo sioni kama kuna kinachoenziwa, ninachokiana mimi ni uongozi mbovu wa SMZ.Ambapo huwezi kuwalaumu wazanzibari kwasababu hawakuuweka wao huo wa CCM hapo madarakani.Ni wazi kuwa Tanganyika kama mkoloni ndio amelazimisha warudi madarakani.

  Kuhusiana na ubaguzi wa Pemba na Unguja, wewe kama si mzanzibari basi huna haki ya kuuzungumzia.Tuachie wenyewe tutadili nao, huo ubaguzi upo.Na ni jambo la kawaida kabisa, ubaguzi upo duniani kote.Na ubaguzi upo kila namna kila corner ya dunia.

  Hili suala kwa ufupi lilikuwepo, na Tanganyika kwa njia moja au nyengine linahusika na kila baya linalofanyika visiwani humo.Salmin, ambae hakutakiwa na wazanzibari aendelee madarakani lakini Nyerere akapindisha demokrasia na kumueka.Mtu ambae hana sifa ya kuongoza, alipandikiza chuki kubwa Zanzibar.Sina uhakika kama alitumwa au ni chuki binafsi hilo hatuwezi kujua...lakini uwezekano upo!

  Chuki hizo ambazo zimepandikizwa katika utawala wa Salmin, hadi sasa zinahitajika kufutwa.Kwa hiyo Tanganyika bado ni tatizo kubwa visiwani humo....sioni sababu ya kusema ubaguzi huo ndio kigezo cha kutoa kibali cha Tanganyika kuendeleza utawala wa kibeberu na kuiburuza Zenji.

  All in all Mapinduzi ni suala la historia, halina dili yoyote katika kuleta maendeleo visiwani humo!
   
 12. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #12
  Jan 13, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nilifikiri jana Mapinduzi yameenziwa kwenye sherehe za Miaka 46 ya Mapinduzi ambapo watu walijaa sana uwanjani huko Pemba! Na huo uongozi mbovu wa SMZ ambao umewekwa na Wazenj wenyewe mbona CUF mmeutambua sasa? Hamuoni kwamba CUF ni wanafiki na hamstahili kuaminiwa?
   
 13. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Sasa ulitaka CUF ifanye nini?Iache wazee wetu waendelee kula kichapo?Hapo hakuna usaliti wowote, nyie mmekaa hapo Dar mnaishi fresh bila bugdha.Wakati Pemba watu wanateswa na kufanyika kila aina ya unyama na vyombo vyenu vya dola.JWTZ na Jeshi la polisi, wanaongoza kwa kuadhibu wananchi huko visiwani Zanzibar.

  Sasa Maalim kuzungumza na Karume na kusema ameitambua SMZ, ni masuala ya lazima.Wewe unajua kama kuna watu Pemba tayari walikuwa wanayakimbia majumba yao nyakati za usiku?

  Unafikiria watu wanapenda kulala chini ya miti na kuacha vitanda vyao?Sasa CUF na Maalim wake, wamefanya jambo ambalo sisi wazanzibari tunajua kabisa linalenga nini.Wewe bora jadili masuala ya kudili na hao mafisadi huko wasiendelee kuiba huko bara.

  Masuala ya Zanzibar waachie wazanzibari wadili nayo, si kama ubaguzi.Tatizo huwezi kufahamu, na utakuwa unazungumza pumba tupu.Ni karibu asilimia 90% ya wazanzibari wameunga mkono hizo jitihada za Karume na Seif.Unafikiria hiyo ni bahati mbaya?Hii ni kwasababu tunajua kwamba hicho kitu ni lazima na tunahitaji wafanye hivyo.

  Tushachoka vizee vyetu na familia zetu kuteswa na majeshi yenu yanayoongozwa na JK.

  P:S
  **Anyways, kitu nilichosoma kutoka kwa watanganyika.Si wengi ambao hupenda kuona maendeleo ya aina yoyote ndani ya visiwa hivyo.Sijaweza kugundua bado ni kwanini?Roho mbaya au kuna mizizi ya kihistoria huko iliyokupelekeeni kuwa hivyo mulivyo.

  **Maana Zanzibar ilihusika na biashara ya utumwa, sasa sijaweza kupata strong evidence ni kwanini.
   
Loading...