CUF: JK punguza safari, tuzalishe umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF: JK punguza safari, tuzalishe umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchakachuaji192, Jul 4, 2011.

 1. mchakachuaji192

  mchakachuaji192 JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Minael Msuya
  CHAMA cha Wananchi CUF, kimemshauri Rais Jakaya Kikwete kuacha kupoteza muda mwingi kwenda nje ya nchi kutafuta wawekezaji na badala yake atafute uvumbuzi wa tatizo la umeme.


  Kwa mujibu wa CUF, Serikali imeshindwa kubuni vyanzo mbalimbali vya kufua umeme na kusababisha nchi kuwa katika hali mbaya kiuchumi kutokana na mgawo wa umeme uliopo na kupunguza ajira nchini.

  Akizungumza na wanahabari mjini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Julius Mtatiro alisema Serikali imeshindwa kueleza ukweli kuhusu tatizo la umeme badala yake inatoa sababu zisizo za msingi na kwamba ahadi za miradi ya kuzalisha takribani Megawati 1,300 za umeme ni uongo na haiwezi kutekelezeka.

  “Mgawo wa umeme ni tatizo la taifa kama wanavyosema viongozi wa Serikali ya CCM, athari zake ni kubwa mno kwa wananchi na hata katika uzalishaji wa uchumi wa nchi,” alisema Mtatiro.

  Alisema: “Hapo hapo Serikali inashindwa kueleza kwamba imezidiwa kutokana na mahitaji makubwa ya huduma ya umeme kuliko uzalishaji badala yake inasema mabwawa hayajajaa, mitambo imeharibika, mafuta yayamekwisha, sababu ambazo hazina msingi wowote kwa nchi inayohesabu miaka 50 tangu kupata uhuru,”.

  Mtatiro alisema tatizo la umeme nchini haliwezi kumalizika kama Serikali haitaweza kubuni vyanzo mbadala vya kufua umeme kwa kuwa mahitaji ya umeme ni zaidi ya Megawati 3,000 na unaozalishwa ni Megawati 800.

  “Kwa maana nyingine Rais anapotafuna fedha za umma kwa safari za nje kila kukicha, kiguu na njia kuonana na wawekezaji na kuwashawishi waje kuwekeza Tanzania anawahadaa na kuwadanganya,” alisema Mtatiro.

  Alisema watendaji walioko ndani ya Serikali wanaogopa kuanzisha vyanzo vipya vya umeme asili kutokana na kukosa miradi ya kukatiwa asilimia 10.


  Mtatiro alisema Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja anapaswa kujiuzulu kutokana na kushindwa kusimamia Shirika la Umeme Tanesco na kazi yake kupewa kiongozi mwingine ambaye ataiondoa nchi katika tatizo la mgawo wa umeme usiokwisha.

  Alisema vipo vyanzo mbadala vinavyoweza kufua umeme na kwamba maeneo ya maporomoko ya maji yanaweza kufua umeme wa megawati 5,000 ukilinganisha na uwezo wa sasa wa megawati 562 .

  “Vyanzo vingine ni makaa ya mawe ambayo yamesgunduliwa na yanaweza kufua umeme wa megawati 1,000 kwa zaidi ya miaka 50 ijayo, Gesi ya Mnazi Bay inaweza kufua pia umeme wa megawati 1,000, Madini ya Uranium na umeme wa jua na upepo vitaweza kupunguza tatizo hili,” alisema.
   
 2. N

  Nkomoji JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa rais wetu amezidi kusafiri!labda yupo kwenye mashindano ya kusafiri ili siku moja tusikie RFA kwenye kipindi cha 'Je wajua?'rais aliyevunja rekodi ya kusafiri nchi za nje huku raia wake wakiteseka sana hawana pa kukimbilia njaa,vitu bei juu,umeme hakuna!
   
 3. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi huyu rais hebu atuambie tu hili tatizo la umeme litaisha lini? mbona yupo kimya?
   
 4. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,847
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Tunamlea sana huyu.
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,375
  Likes Received: 3,138
  Trophy Points: 280
  Aaaahhh.............cuf nao si ndo hao ccm-b?......wao ndo kikwete ndio ccm-a sasa wanalalamika nini badala ya kuongelea kwenye vikao vyao.....................hilo suala la chadema
   
 6. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Mi naona bora Kikwete akatwe miguu ili asisafiri kabisaaaaaaaa, mtu gani asiyetulia kila siku yeye na pipa, pipa na yeye. Ahamie kabisa huko juu ya anga tujie kabisa, kwanza hatumuhitaji akae hukohuko juuu ya anga tena ikiwezekana hata NASA wamsaidie kukaa huko juuu
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,375
  Likes Received: 3,138
  Trophy Points: 280
  pengine itasaidia............
   
 8. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Sasa si mumshauri afanyeje ili kumaliza tatizo; washauri wote wizarani, kamati ya Bunge ya Nishati, wataalamu wa Tanesco na Wabunge kwa ujumla wao wameshindwa kutoa mwelekeo wa kutatua tatizo. Mwenye wazo la kuokoa jahazi alipeleke kunakohusika haraka iwezekanavyo
   
 9. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  jamani kuna dawa gani tumnyweshe raisi wetu aache kuzurura? au tumpeleke samunge? aagh!
   
 10. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  samunge alishaenda!!!!
   
 11. i

  in and out Member

  #11
  Jul 4, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mambo yake kama vasco Da gama.
   
 12. HOYANGA

  HOYANGA Senior Member

  #12
  Jul 4, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  koki ak 47 lenga usawa wa mgongo kwa nyuma hakikisha usalama uko on kabla hujakoki then vuta trigger, tandika kama mkanda mzima usawa huo nyuma ya mgongo, ikishindikana twanga head nusu mkanda......kwisha kabisa pale mambo shwari!!!!!
   
 13. HOYANGA

  HOYANGA Senior Member

  #13
  Jul 4, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hakuna relevance ya ya vikombe na tiba ya huu ujinga wa vasco!!!!!
   
Loading...