CUF: Jaji Dyansobela, amzuia msajili kutoa fedha za umma (ruzuku) kwa Lipumba na kundi lake

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam mbele ya mheshimiwa jaji Dyansobela katika shauri no. 28/2017 leo tarehe 31/03/2017 imetoa amri dhidi ya msajili wa vyama vya siasa nchini jaji Francis Mutungi kumzuia kutotoa fedha za ruzuku ya the civic united front (cuf-chama cha wananchi) mpaka shauri namba 21/2017 dhidi ya msajili na mwanasheria mkuu wa Serikali kuhusu kutoa fedha za ruzuku shilingi milioni 369 kwa njia za wizi na udanganyifu litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

Amri hiyo ya mahakama kuu imekuja baada ya jopo la mawakili wasomi wa chama wanaoiwakilisha bodi ya wadhamini ya CUF (the registered trustees of the civic united fron (CUF-chama cha wananchi) mhe. Juma nassor, mhe daimu halfani na hashim mziray kuwasilisha maombi hayo mbele ya mahakama kuu kuiomba mahakama kuu kutoa amri hiyo kwa kuwa fedha zilizotolewa awali milioni 369 hazijulikani zimetumika vipi, na hazikuwa katika mikono salama wala hakuna udhibiti wowote wa chama –cuf juu ya fedha hizo ikizingatiwa kuwa lipumba alishavuliwa uanachama.

Wakili msomi Juma Nassor aliyewasilisha maombi hayo aliweka mkazo na kusisitiza kuwa kwa mazingira yaliyopo ni vyema na busara kwa fedha za umma zilizopaswa kutolewa kama ruzuku kwa chama cha CUF kwa sasa ziendelee kubakia Serikalini. Aidha, mawakili wasomi wameiomba mahakama kuu amri hiyo pia ifungamane na kesi ya msingi namba 23/2016 ya kuhoji maamuzi ya msajili kumtambua Lipumba kwa nafasi ya uenyekiti iliyopo mbele ya jaji kihijo ambayo kwa sasa imekatiwa rufaa/maombi ya kufanyiwa marejeo-revision mbele ya mahakama ya rufaa-Tanzania.

Mhe Jaji Dyansobela amekubaliana na hoja zote hizo zilizowasilishwa kwa hati ya dharura(under certificate of urgency) na kutoa amri ya kuzuia fedha za serikali kutolewa kwa maslahi ya umma mpaka hapo mashauri yote yatakaposikilizwa na kuamuliwa ipasavyo.

Katika hatua nyingine ili kuhakikisha kuwa masuala ya kesi yote yanasimamiwa na kushughulikiwa na kumalizwa kwa haraka katibu mkuu, maalim Seif Sharif Hamad ameshakamilisha mazungumzo ya kuongeza nguvu zaidi za utetezi wa kisheria kwa kuwapata mawakili wasomi maarufu sana nchini watano (5) ambao wataungana na kutengeneza jopo la mawakili 9 watakaosimamia kesi zote dhidi ya lipumba na kundi lake.

CUF ni taasisi imara, yenye viongozi makini.

Haki sawa kwa wote

Imetolewa leo tarehe 31/3/2017

Mbarala maharagande
Naibu mkurugenzi wa habari, uenezi
Na mahusiano na umma- cuf taifa
 
. Aidha, Mawakili wasomi wameiomba Mahakama Kuu amri hiyo pia ifungamane na Kesi ya Msingi namba 23/2016 ya kuhoji maamuzi ya Msajili kumtambua Lipumba kwa Nafasi ya Uenyekiti iliyopo mbele ya Jaji Kihijo ambayo kwa sasa imekatiwa Rufaa/maombi ya kufanyiwa Marejeo-REVISION mbele ya Mahakama ya Rufaa-Tanzania.
Hapo pa red, marejeo yanahusu nini?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Naona siku za hivi karibuni muhimili wa sheria umeanza kurejesha makali yake kwa mbaaliiiiiii...baada ya kuwa umesimikwa kwenye kina kirefu cha muhimili ule ulio juu ya muhimili yote, wakienda hivi mpaka mwaka 2020 Mola akitupa
uhai tutayaona mengi sana aiseee.
Big up.mahakama na majaji wote kwa kujitambua.
 
Back
Top Bottom