Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 18,961
- 47,828
CUF tangu kuanzishwa kwake imekuwa na nguvu sana Pemba, na idadi ya wabunge wake wakati wote imebakia ile ile kukiwa na mabadiliko kidogo sana. Licha ya kwamba chama hiki kilianzishwa Tanzania bara lakini kilipokewa vizuri zaidi huko Visiwani huki kikikosa nguvu Tanzania bara hadi kufikia leo kuonekana kuwa CUF-bara inaishi kutokana na CUF-Zanzibar.
CUF katika kipindi chake chote tangu kiwe chama cha upinzani chenye wabunge na wawakilishi wengi bungene na kwenye baraza la wawakilishi, jitihada zake zote za kisiasa na kidemokrasia zimekuwa zikionekana huko Zanzibar tu na siyo Tanzania bara. Sikumbuki tukio lolote ambalo chama cha CUF kimekwahi kufanya katika bunge la mwungano kupitia nafasi yake ya kuwa 'chama kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni'. Safari hii baada ya kufikia malengo yake kule Zanzibar, kimeonekana wazi kuwa hakina kitu kinachopiganiia zaidi ya kuunga kila hoja ya umoja wake na CCM.
Swali langu kwa viongozi wa CUF, Je, chama hiki kilikuwa na lengo lolote kwa Tanzania bara? Malengo hayo yalikuwa yapi, na wamewahi kufanya jitihada gani zinazoshabihiana na kule Zanzibar? Umuhimu wa wabunge wa CUF-Zanzibar katika bunge la mwungano ni nini hasa? Nini kitakachokosekana kama wasipokuwepo?
Nafasi ya pekee ya CUF inayoonekana kwa upande wa bara ni chama ambacho kwa kupitia wabunge wake wengi wa kutoka Pemba hakijawahi kupigania kitu chochote kinachokumbukwa kwa maslahi ya Tanzania bara. Nadhani wengi tunachoshuhudia sasa ni kwa chama cha CUF Zanzibar kutumika na CCM kufifisha jitihada za Tanzania bara kupigania haki na demokrasia. Watanzania bara tuna wasiwasi sana kuwa huenda kutumika huku kwa CUF kuvunja nguvu ya upinzani Tanzania bara ni sehemu ya makubaliano kati ya CCM na CUF-Zanzibar katika mwafaka wa Zanzibar.
Ninachojiuliza ni kuwa CUF-Zanzibar kwa kushirikiana na CCM kufifisha harakati za kidemokrasia Tanzania bara, hawajui wanatengeneza hasira ya Watanzania bara dhidi ya CUF-Zanzibar na wabunge wao? Maana kipindi chote walipokuwa na wabunge wengi hawajafanya lolote kuwasaidia wapenda mabadiliko wa bara, leo wabara wamejitahidi kwa nguvu zao binafsi, wao wanawekeza nguvu nyingi kufifisha jitihada hizo. CUF-Zanzibar mmefanikiwa huko Zanzibar katika mambo yanayowahusu katika maisha yenu ya kila siku, huku bara, tafadhali tuachieni wenyewe ambao tunahusika nayo. Makeke yenu, kama mnayo, mkaoneshe kwenye baraza la wawakilishi, huku nafasi yenu kubwa ni kusikiliza. Wasikilizeni wabunge wa CUF wa Lindi mjini na Kilwa maana hao wanatambua watanzania bara katika maeneo yao wanataka nini.