CUF hali mbaya, wakutana makao makuu kujadili athari za kumfukuza Hamad Rashid

..hakuna athari zozote zile.

..ukifanyika uchaguzi leo hii CUF itashinda Pemba, na CCM itashinda Unguja.

..huku Tanganyika, CUF wako kwa ajili ya kutimiza masharti ya kisheria.
ni kweli mkuu. sioni athari yoyote kwa CUF kumpoteza Hamad Rashid,watadanganyika watu wasiozifahamu siasa za Unguja na Pemba. Sitashangaa kama HR uchaguzi ujao kuogopa aibu ya kushindwa Wawi atagombea ubunge jimbo la bara.
 
Wanajadili nini sasa wakati HR sio mwanachama wao kwa mujibu wao wenyewe. Sikio la kufa halisikii dawa.
 
toeni mapovu humu wee paka mtachoka. Hicho nikikao cha baraza kuu la cuf cha kawaida kuonesha chama kinafanyakazi. Hatusikilizi ***** wenu. Karibuni sana mwembe yanga kwenye mkutano mkubwa. Gazeti limerudishwa kinachofatia sasa radio. Kuonesha cuf tupo kazini rongorongo zenu mpeleke humu jf na zifie humu jf
 
[h=2][/h][h=3]Prof Lipumba Afungua Kikao cha Baraza Kuu la CUF Taifa[/h]

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Uongozi Taifa, huko ukumbi wa Lamada jijini Dar es Salaam.Kushoto yake ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Ismail Jussa.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza katika kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Uongozi Taifa

Na Hassan Hamad OMKR

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba amesema uamuzi wa kumfukuza uanachama mwakilishi wa Jimbo la Wawi Bw. Hamad Rashid Mohd ulikuwa sahihi na wala hayakuwa maamuzi magumu kama baadhi ya watu wanavyofikiria.


Amesema Chama hicho tayari kimefanya maamuzi magumu zaidi kuliko hilo la kufukuzwa kwa Hamad Rashid na kwamba suala hilo lilifanywa kwa lengo la kukilinda chama na wanachama wake ambao wengi wao ni wanyonge.


Prof. Lipumba ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akifungua kikao cha siku mbili cha kawaida cha baraza kuu la uongozi la CUF taifa, kinachofanyika katika ukumbi wa Lamada jijini Dar es Salaam.



Amesema Chama hicho kinazingatia na kutetea maslahi ya wanyonge, na kwamba kitaendelea kufanya hivyo bila ya kujali maslahi ya mtu binafsi.


Prof. Lipumba pia ametoa ufafanuzi wa kiuchumi wa jinsi ya kuwaendeleza wananchi na taifa kwa jumla kwa kutumia vyema rasilimali zilizopo pamoja na teknolojia ya kisasa kwa maendeleo.


Amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi zikiwemo ardhi yenye rutba, madini, gesi asilia, bandari na jiografia yake kwa ujumla ambapo amesema iwapo vitatumika vizuri wananchi wanaweza kunufaika na kupunguza tatizo la umaskini linalowakabili.


Amefahamisha kuwa Tanzania inapaswa kuliingiza suala la maliasili kwenye katiba na kulikabidhi kwa wananchi katika utaratibu ambao wananchi wataona kuwa ni rasilimali zao na hivyo kuweza kuzilinda.


Amesema wananchi wengi wamekuwa wakinyasisika na rasilimali zao kwa kukosa uhuru wa kisiasa na kiuchumi, na hivyo kushindwa hata kumiliki maeneo yao wanayofanyia kazi.


“Wakulima wa korosho kwa mfano hawana umiliki wa mashamba yao, hiki ni kikwazo kikubwa cha kiuchumi kwa wananchi wa vijijini.


Amewaka wazi kuwa maendeleo ya sayansi na teknolojia katika karne ya 21 ni lazima yaendane na uhuru wa kisiasa na kiuchumi kwa wananchi, na kutaka ombwe la uongozi wa serikali iliyopo liondolewe ili kurahisisha maendeleo ya kiuchumi.


“Tunahitaji tulete mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa, na hili halitowezekana ikiwa ombwe hili la utawala wa CCM wa miaka 50 tangu uhuru halijaondoka”, alisema Prof. Lipumba.


Amesema miaka 50 tangu uhuru ni kipindi kirefu ambacho baadhi ya nchi zimeweza kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi tofauti na ilivyo Tanzania, hali iliyotokana na kutokuwepo kwa mikakati madhubuti ya kukuza uchumi.


Prof. Lipumba ambaye ni mtaalamu wa uchumi na ambaye hivi karibuni alirejea kutoka nchini Marekani ambako alijikita na kazi utafiti kuhusu namna na kupanua demokrasia kwa maendeleo ya kiuchumi, amesema atatumia fursa hiyo kuitumia taaluma hiyo kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini.


Amesema inasikitisha kuona bajeti ya umeme ikiongezwa kwa kiasi kikubwa lakini tatizo linabakia pale pale, na kufafanua kuwa hakuna uwajibikaji wa kutosha katika serikali.


Prof. Lipumba pia amekemea siasa za udini ambazo amesema hazina mustakbali mwema katika kuwaunganisha watanzania na kuwaletea maendeleo.


“Watanzania waunganishwe bila kujali dini au ukabila, ili kila mtu aweze kunufaika na mpango huu wa kuwaunganisha Watanzania”, alifahamisha.


Mapema akizungumza katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, amemuhakikishia Prof. Lipumba kuwa Chama kiko imara kama alivyokiwacha kabla ya kuondoka au zaidi ya hapo.


Amesema licha ya kutokea bughudha chache katika siku za hivi karibuni, lakini tayari zimetatuliwa na shughuli za Chama zinaendelea kama kawaida.
 
Lipumba ataka gawio la rasilimali wapewe wananchi
Tuesday, 20 March 2012 20:46


Raymond Kaminyoge na Ibrahim Yamola
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ametaka rasilimali za taifa zikiwamo madini na gesi kugawanywa kwa wananchi ili kuwapunguzia umaskini uliopo.Amesema suala ya wananchi kupewa mgao wa fedha zitakazotokana na rasilimali za taifa , liwekwe kwenye Katiba mpya ambayo mchakato wake umeanza.
Profesa Lipumba alisema hayo jana jijini Dar es Salaam , wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Chama hicho. "Ili kuwapunguzia makali wananchi sehemu ya fedha zinazopatikana kutokana na rasilimali ya taifa igawanywe kwa wananchi," alisema Profesa Lipumba.

Alisema hilo linawezekana kwa sababu nchi kama za Mexico na Brazil zimefanya hivyo na zimefanikiwa na wananchi wake wana maisha yenye matumaini.

Lipumba alisema , inashangaza hapa nchini wakati wanasema uchumi unakua lakini wananchi wake wengi wana utapiamlo kwa sababu ya kula chakula cha aina moja.

Alisema wananchi wakipewa mgao wa rasilimali zao, watakuwa makini katika kuzisimamia rasilimali hizo kwa sababu watakuwa miongoni mwa wamiliki. " Maliasili ni mali ya wananchi, wanapogawiwa sehemu ya mali hiyo watakuwa makini katika kuzisimamia," alisema Profesa Lipumba
Aliongeza kuwa wananchi wakipewa fedha hizo , wataweza kusomesha watoto wao na kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo.

Profesa Lipumba alisema , wananchi watakaonufaika na mgao huo watajulikana baada ya kukamilika kwa zoezi la utoaji wa vitambulisho vya taifa. " Mawazo haya hayataungwa mkono na mafisadi kwa sababu wao wana uchu wa kuchukua rasilimali zote na kuwaacha wananchi wakiwa hoi," alisema.

Umeme Profesa Lipumba ameshangazwa na Serikali ya Rais Jakaya Kikwete , kushindwa kumaliza tatizo la umeme lililodumu tangu alipoingia madarakani. " Nalishangaa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) , wanasema hakuna mgao wa umeme wakati umeme unakatika mara kwa mara, tatizo ni nini," alisema.

Alisema wananchi sasa wamekata tamaa kwa sababu kila siku wanasikia kuhusu mipango ambayo haitekelezeki. CUF ngangali Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad amesema chama hicho kiko ngangali kwa kuwa kimesafisha bughudha zilizojitokeza

" Kulikuwa na bughudha bughudha za hapa na pale lakini tumezimaliza salama na sasa chama kiko ngangali kama zamani," alisema Hamad mbele ya baraza hilo. Alisema ingawa watu walisema sana kuhusu uamuzi uliyofikiwa lakini ukweli ni kuwa kilifanya uamuzi sahihi na sasa chama kiko imara.

Kauli hiyo imekuja baada ya chama hicho kumfukuza uanachama Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na wajumbe watatu wa baraza kuu la chama hicho ambao ni Doyo Hamis Doyo, Juma Saanani na Shoka Khamis Juma.
 
Back
Top Bottom