CUF: Hakuna mwingine mwenye sifa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF: Hakuna mwingine mwenye sifa?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by ngoshwe, Jun 6, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  PROFESA LIPUMBA ACHUKUA FOMU KUGOMBEA URAIS: Tokea kuanza kwa mfumo wa vyama vingi wapinzani wamekuwa wakisimamisha wagombea wale wale tu. Hii desturi ya kujaribu jaribu itaisha lini? Hivi huko kwenye vyama vya upinzanii hakuna wengine wenye sifa ya kubadili japo vionjo?


  [​IMG]

  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahimu Lipumba akichukua fomu za kugombea nafasi ya Urais kutoka kwa Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Kinondonio, Mh. Kassim Chogamawano katika ofisi za CUF wilaya ya Temeke jijini Dar leo.
   
 2. TingTing

  TingTing Member

  #2
  Jun 6, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndio changamoto iliyobakia kwetu kuelewa umuhimu wa kujaribu watu mbali mbali toka katika chama wenye uwezo na nia ya kuongoza nchi. Bila hivyo ukuaji wa vyama itabakia kuwa ndoto ambayo haipo.
   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kwani Lipumba kuchukua form ina maana wengine hawaruhusiwi?. Mbona anatekeleza haki yake kikatiba?. Tatizo ni kwamba the more he stays in the race the more popular he is na hicho ndicho kinawatisha critics. Mwache Prof atumie haki yake, kwani at the end ni wanachama wa CUF ndiyo watakuwa na haki ya kusema ni nani wanamuona anafaa kuwakilisha chama chao uchaguzi mkuu, whether Lipumba su somebody else.
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kikwete akichukua fomu CCM unaweza kuuliza kwani hakuna mwingine? Kila Chama kina katiba na utaratinu wake wa kupata wagombea, na sidhani kama Lipumba hata kama ni mwenyekiti anauwezo wa kujiteua kugombea urais kwa niaba ya CUF, na sidhani kama wana CUF hawajui kama wengine wapo. Naamini kuwa wao kuamua kumpa fomu Lipumba ajaribu kugombea si wajinga, wanafahamu wanachofanya ndio demokrasia yenyewe.
   
 5. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  hawaitaji kumpromote mtu mwingine mpaka mwnyekiti atakapo maliza muda wake madarakani?
   
 6. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu mbona kwa CUF mambo 'ize tu' mwanachama yoyote hakuzuiliwa wala "...hatokufa" kama anataka kupambana na Maalim Seif au Prof.Lipumba kila mtu yupo huru, muhimu kufuata taratibu tu.
   
 7. d

  damn JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Yes I agree. But Lipumba ni kupoteza muda. Bora angesimama hata Seif Sharif Hamad kwa Urais wa Jamhuri ya muungano. Lipumba hata akiteuliwa kugombea uenyekiti wa kijiji chake cha ilulangulu-Tabora hachaguliki.
  Kwa miaka 15 tangu aanze kugombea upresidaa, sikumbuki CUF kuwa na wabunge wa kuchaguliwa kutoka bara zaidi ya Rwakatare aliyekuwa mbunge bukoba vijijini 2000-2005.

  He is absolutely of no use. Ana cripple CUF
   
 8. K

  Kumutumbali New Member

  #8
  Jun 8, 2010
  Joined: Jun 5, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haa we ni wa wapi? kwani hujuwi kuwa ni yeye tu ndiye aliyewahi kuwakaribia CCM kwa kura za urais katika chaguzi zote ukiondoa ule wa 1995. halafu sikufichi huyu bwana mkubwa anakubalika sana huku kwetu pwani na chama kinaendelea kuimalika sana mbadala ya sisiem ukanda wetu sisi ni CUF. Hao wengine wa milimani hatuwajui bana hata kwenye kudai uhuru tuliwaita tu hawakushiriki.
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwani huyo Professa hawezi kusema: Mimi basi sasa, mara tatu yatosha, nawaachia wengine wenye damu kali zaidi na mawazo mapya -- na kuwaombea kila la kheri?
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Katika CU hakuna wenye uwezo na elimu zaidi ya wawili hawa - Professor na Maalim. Wengine wote elimu yao ni mpakazo tu
  ---tehe tehe tehe!!!!!!
   
 11. C

  Chuma JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2010
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi kuna mtu kazuiliwa Kugombea...? Kama humpendi Lip tuliza ball wapo wanaoona anafaa...Endelea na Kidumu chako.

  Hivi Hujui CUF walishawahi kuwa na Mbunge Kigamboni...? halafu unasema thinker...!!!
   
 12. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #12
  Jun 10, 2010
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Yale yale aliyosema Dr. Omary (RIP) mpaka mtu apigwe mawe ndio ajue hatakiwi, pisheni watu wanaochagulika tuondoe ubishi.
   
Loading...