Elections 2010 Cuf chama shindani au chama tawala?

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
wanaJamii,
baada ya serikali ya Umoja wa kitaifa, CUF gani tuitegemee katika bunge na baraza la wawakilishi 2010 - 2015, Je wabunge wa CUF hawatakua rubber stamp tu kwa sababu chama sasa, kwa namna flani, kimeshika dola, ingawa sio kwa asilimia 100
 
Asante kwa kuligusia tena hili suala. Hotuba ya Seif alipokubali matokeo ya uchaguzi akisema hakuna mshindi... tumeshinda wote... ilinipa picha ya makubaliano yaliyofanyika mapema na uchaguzi umekuwapo ili tu kufuata taratibu za katiba kwa namna fulani. Na kwa vile wabunge wa CUF wako visiwani ambako si wapinzani, sidhani kabisa kama CUF ni chama cha upinzani; kitakuwa ni chama kinachoiunga mkono serikali, kama vilivyo vyama vingi kwenye mataifa ambayo bado siasa imegawanyika kwa mlengo wa kulia au mlengo wa kushoto.
 
ikiwa hivi basi hili ni pigo kubwa kwa vyama shindani, na ccm imelamba karata dume, muda wa kuing'oa ccm katika utawala wa nchi ndo kwaaaaaaanza inataka kuanza, yaani tumerudi nyuma, tumevuka hata ule mstari was 'start'
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom