CUF, CHADEMA, NCCR na TLP anzisheni makubaliano sasa mlikomboe taifa letu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF, CHADEMA, NCCR na TLP anzisheni makubaliano sasa mlikomboe taifa letu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mlimbwa1977, Oct 26, 2011.

 1. m

  mlimbwa1977 Member

  #1
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa ujumla hali ya maisha kwa Watanzania walio wengi inaendelea kuwa mbaya kadri miaka inavyokwenda licha ya maliasili zilizopo nchini.Mwaka huu tunasubiri kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika,umri wa miaka hamsini hairandani na maisha duni waliyonayo watanzania walio wengi.Kumekuwa na namna ya kujitetea kwa viongozi wetu kuwa Taifa letu bado changa hivyo kuhalalisha udhaifu uliopo wa maisha duni.Kwamba tunapaswa kuwa na subira mpaka tutakapofikisha labda miaka elfu moja,ndipo tuweze kulingana na wenzetu kimaendeleo kama vile,Africa Kusini,Libya,Misri,Cape verde,Shelisheli,nk.

  Hali mbaya iliyopo nchini ya kiuchumi,kiuongozi,kijamii,Kisiasa,nk.itaendelea kudhoofisha mustakabali wa taifa letu kama mabaliko ya haraka hayatafikiwa.Licha ya kuwa na kila aina ya utajiri tumekosa viongozi,viongozi bora ndio mwarubaini wa matatizo tuliyonayo sasa.Viongozi wanapatikana kwa njia ya kuchaguliwa,hatuhitaji viongozi wanaoshindwa kufanya maamuzi,badala yake wanaishia kulalamika kama ilivyo kwa wasio na mamlaka ya kufanya maamuzi (wananchi wa kawaida).

  Taifa letu litajiendesha kwa ufanisi tutakapoondokana na ukiritimba wa chama kimoja kujiona ndio wenye haki ya kuongozi taifa letu,tunahitaji ushindabni wa vyama vya siasa katika kuwaletea maendeleo wananchi,chama kinachofanikiwa kuongoza vizuri ndicho kinachopaswa kuchaguliwa kuongoza.Chama cha mapinduzi kimeonyesha kwa vitendo kushindwa kuongoza taifa.Angalia viongozi wa serikali za mitaa hakuna wanachofanya,angalia maofisini hakuna kinachofanyika cha maana (wafanyakazi wanafanyakazi kwa mazoea,hakuna kuwajibishana),wananchi
  wameendelea kuishi kwenye nyumba za tembe,matibabu duni,elimu isiyokidhi,miundombinu isiyokidhi,bei za vyakula juu,uzalishaji duni wa bidhaa viwandani,tumeishia kuhemea kutka nje,thamani ya shilingi inaendelea kuanguka,hakuna anaejali.

  Umuhimu wa vyama vikuu vya upinzani nchini kuuanzisha ushirikiano kuelekea uchaguzi mkuu ujao ni muhimu sana sasa kuliko wakati mwingine wowote,chama chochote kitakachojiona ni bora kuliko wenzao na kutarajia kushinda peke yake ni kujidanganya.Ushirikiano ni muhimu sana ili kuiondoa CCM madarakani ili tuanzishe mfumo wa kupokezana uongozi,hii italeta ushindani muafaka katika kuwaletea maendeleo wananchi.Nawaomba Chadema,CUF,NCCR,nk.kuacha kiburi,nchi hii ni yetu sote tunawategemea sana kubadilsha mfumo wa uongozi uliopo sasa katika nchi yetu.mlimbwa1977@yahoo.com.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  CUF ni CCM B hawafai kwenye upinzani
   
 3. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,553
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Si kweli sikubaliani na fikra kama hizi, lete ushahidi wa kina?
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Cuf watakubali kuivunja hiyo ndoa ya danganya toto na magamba hapo zanzibar?
   
 5. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,612
  Trophy Points: 280
  hivi chama makini kama CHADEMA kina weza kukubali kuungana na vibaraka mbatia,mrema,dovutwa na wakina mzirai?tunachoshukuru Mungu ni kwamba CDM imeweza kuungana na watanzania wanao itakia mema Tanzania.hadi 2015 pumba na mchele vitakua vishajitenga.mia
   
 6. M

  MLEKWA Senior Member

  #6
  Oct 26, 2011
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ikiwa CUF ni CCM B na jee Chadema si chama cha Kanisa ! sasa si bora tubaki na huyu marehemu CCM . NCCR ni chama chenye Historia kubwa kwa Tanzania ikiwa Mutakumbuka 1995 ndio chama kilichokua msatari wa Mbele kupigania mageuzi pamoja na CUF ila Chadema kilikua chama cha wachaga na kilikosa startegy hadi recently kilipopata wat uwa kuwaonesha njia ila hao hao wameanza kwuakosesha njia Historia mwalimu Mzuri leo Tunisia uchaguzi umefanyika chama Maarufu cha ELNAHDA hakikuweza kuunda serikali bila ya ushirikiano wa vyama vyengine na hii jeuri ya chedema kuna uwezekano mkubwa kuwa Thirdy party ndio kikawa power Broker wa Ku control Bunge na serikali ya Rais ajae. Ikwia chama Kidogo kule UK kiliweza kuchagua nani aunde serikali ya Uingereza ilikuwa ni Either Conservetive or Labor mmoja wao yoyote alieweza kupata support ya Liberal Democrat Nick Clegg, Leader of the Liberal Democrats - Home huyu ndio aliokuwa na power ya Kumfanya mtu yoyote kwua Waziri mkuu wa UK.
  Tuwaulize Chadema ikitokes kesi hii na uhusiano wao mchafu kwa CUF watafanya nini ?
  Nawashauri wafuasi wa Chadema wajue ku play na Politics sio kujifanya wajanja wa mjini watasota kwenye benchi la upinzani kwa miaka mingi kwa hii style yao ya kutaka kuwabagua Watnznaia na Wazanzibari, Chadema someni alama za nyakati. Huwezi kuanza kuonesha sura ya udikteta kabla hata hujakabidhiwa serikali una Kibri namna hii jee ukikabidhiwa mpini si utawaua watu a na kuanza kuweka watu vizuizini ikiwa leo Vyama vilivyochaguliwa na wananchi havina hadhi kwa chadema je na wapiga kura wa vyama hivyo ikifika wakati Chadema wanahitaji nguvu ya wapinzani wengine kufanikisha ndoto yenu ya kuhika mpini wakisema NO si mutakua munaendeleza ile deni la kuwadhulumu Watanzania kupata mageuzi haraka lakini nyinyi munasema uhuru usije wka vile sisis sio tuatakaopwewa ?
  Chadema waliwahi kubahatika kuwa na kiongozi mwenye Busara na kuona mbali ni Mmoja tu aliweza kukijengea haiba ni BOB MAKANI Chadema ya wakati huo haikua ya kihuni , na ubaguzi licha ya kuwa haikua na nguvu ila ilikua na Busara ubabe utawafundisha kuwa siasa za ubabe wakat i wake umepita any Violent Party kitaendelea kupotea kwenye siasa Duniani. Iko wapi KANU kila siku nawafundisha Historia CCM haitakiwi kuwa madarakani ila wanaoendellea kuiweka madarakani ni Wapinzani kwak u kosa umoja. Siiku chadema mukiweza kumpinga adui huyu turudi jamii forum tupongezane kwa kuweza kuleta mageuzi si hivyo muacheni marehemu CCM siamini kuwa wanchadema munakubali kuongozwa na mzoga huyu alifariki toka 1995 NCCR alipompiga Kitanzi. aendelee Kula kuku kwa mrija . wenu Mlekwa.
   
 7. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hizi ni propaganda za magamba.
  Chadema inahitaji kuungana na umma.
  Chadema haihitaji Hamad Rashid, Lyatonga, Mbatia wana kibaraka mwingine yeyote manayemapigia debe hapa.
  Chadema inahitaji kuungwa mkono na watanzania waliochoshwa na ufisadi na mambomengine kama hayo.

  Kamwambueni huyo aliyewatuma kuwa, nchi itakombolewa kwa nguvu ya umma, wala si kwa kujikomba ili kupata madaraka.

  Solidarity Forever.
   
 8. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,000
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Kwani wewe ni raia wa nchi gani?
   
 9. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wote wabinafsi watupu.
  CCM chama kubwa.
  OTIS.
   
 10. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #10
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hatuwezi kuishirikisha CUF Katika mapambano ya kukataa hali inayoendelea, kwakua CUF imeshiriki kutufikisha hapa.
   
 11. m

  mlimbwa1977 Member

  #11
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inashangaza kuona watu wakiendelea kushabikia mambo wasio na ushahidi nayo.Nani aliye na ushahidi kuwa CUF ni CCM B? Unaposema ni B maana yake ni nini? Nani aliye na ushahidi kuwa CHADEMA ni chama chenye mlengo wa dini ya kikristu,pia chama cha watu wa kaskazini? Achaneni na mawazo mgando lazima tuangalie mustakabali wa taifa letu,mawazo/mtazamo huo unapandikizwa na watu wasioitakia mema nchi yetu,wanataka tuendelee kubishana yule CCM B,wale wakatoliki/wachaga,matokeo yake tunawapa mwanya wa kufanikisha malemgo yao ya kudhoofisha upinzani.Hakuna chama cha upinzani kati ya vilivyopo kinaweza kujihakikishia kushinda uchaguzi mkuu ujao bila kuunganisha nguvu katika kudai mambo ya msingi kwa pamoja.Kukosekana kwa tume huru ya uchaguzi,hamasa ndogo ya wapiga kura ni mambo yanayopaswa kufanyiwa kazi katika ushirikiano utakaoanzishwa.Tunahitaji kuwa na wabunge wengi kutoka kambi isiyounda serikali ili kuimarisha uhai wa mijadala na maamuzi bungeni.Wote mnaopenda kubeza muafaka wa Zanzibar kama kigezo cha kuiponda CUF mtazamo wenu ni mfinyu sana.Yaani hamuwatakii mema wazanzibari waliokuwa wakiuana/kuahasimiana kila kukicha.NAMUOMBA MUNGU AONDOE TAMAA YA UONGOZI NA KIBURI WALICHONACHO BAADHI YA VIONGOZI WA UPNZANI ILI HATIMAYE TUONE WAKISHIRIKIANA NA HATIMAYE CCM ING'OKE MADARAKANI TUFUNGUE ENZI MPYA YA UONGOZI KATIKA TAIFA LETU NAAMINI BAADHI YA MATATIZO YANAYOTUANDAMA YATAPUNGUA.
   
 12. M

  Mgongo wa paka JF-Expert Member

  #12
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 486
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  nawe umenena wapinzani tunajimaliza wenyewe ccm inachekelea tu ukweli ni wakati wakujitazama upya wapinzani
   
Loading...